Msigwa wa Chadema aambiwa athibitishe kuwa serikali inaua watu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msigwa wa Chadema aambiwa athibitishe kuwa serikali inaua watu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Safety last, Jun 17, 2011.

 1. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Katika kikao cha leo bungeni asubuhi mh P.msigwa ameambiwa athibitishe serikali inaua watu na amesema anaoushahidi !ni baada ya Lukuvi kutoa taarifa kwa mwenyekiti.
   
 2. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kazi ndogo! Ila wasijeufukia kama ule wa Lema wa " Waziri mkuu kulidanganya bunge"
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hawa cdm wataacha lini kukurupuka?? Waige mfano wa wenzao CUF!
   
 4. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Umesoma taarifa ya haki za binadamu ya mwaka 2009/2010?
   
 5. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh,,, Kahawa ni tamu.
   
 6. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
   
 7. gwino

  gwino JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [h=3]Vyombo vya dola vimeua watu 73[/h]
  *Ripoti ya LHRC mwaka 2009/2010 yabainisha
  *Polisi yaongoza uvunjaji haki za binadamu


  Na Tumaini Makene (gazeti la Majira)

  WAKATI sakata la mauaji katika Mgodi wa North Mara likiwa halijapoa, Jeshi la Polisi limezidi kuingia katika tuhuma za uvunjaji wa
  haki za binadamu kwa kufanya mauaji kinyume cha sheria, Ripoti ya Haki za Binadamu nchini kwa mwaka 2010 imesema kuwa kwa mwaka huo pekee, vyombo vya dola vyenye wajibu katika kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi, vimeua wananchi 52.

  Kutokana ripoti hiyo kubainisha suala la mauaji ya raia yanayofanya na polisi kuwa ni moja ya ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi uliofanywa mwaka uliopita, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambacho huandaa ripoti hiyo kila mwaka, Bw. Francis Kiwanga ametoa wito, 'polisi sasa waache kuwa vinara wa mauaji', akisema kuwa wanapaswa kuwa mfano bora wa kulinda sheria badala ya kuzivunja.

  Ripoti hiyo ambayo imeandaliwa kwa kufuata taratibu za utafiti wa kisayansi, kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama vile kuwahoji watu (5,000) kutoka wilaya 30, taarifa za vyombo vya habari na taarifa za wawakilishi wa LHRC walioko katika kila wilaya nchini, imesema kuwa vitendo vya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya raia kinyume cha sheria vimeongezeka kutoka asilimia 15 kwa mwaka 2009 ambapo watu 21 waliuawa, mpaka asilimia 72 (2010) ambapo watu 52 waliuawa.

  Ikizungumzia sababu za mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola, ripoti hiyo imezitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa askari wenye utaalamu wa kutosha na maadili ya kazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, mfumo dhaifu wa utoaji haki, uchunguzi wa matukio ya namna hiyo kufanywa na polisi wakati wao ni watuhumiwa, hivyo kutoa maamuzi au taarifa zinazoegemea upande mmoja na serikali 'kuwalinda' wale wanaohusika katika uvunjaji huo wa sheria na haki za binadamu, kwa kutochukua hatau stahili.

  Ikitoa mifano ya ukiukwaji wa haki ya kuishi nchini kwa mwaka 2010, ripoti hiyo ambayo ilisomwa jana na Bw. Patience Mlowe, Bi. Haurus Mpatani na Bw. Onesmo Ulengurumwa, ilisema 'vyombo vya dola vinavyoongoza kwa mauaji ya raia kinyume cha sheria ni polisi, wanamgambo, askari magereza na walinzi wa kampuni binafsi za ulinzi. Utafiti wa LHRC unaonesha kuwa kati ya Januari hadi Desemba mwaka 2010, watu 52 walikufa wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola.

  "Katika Mgodi wa North Mara polisi waliua watu 10 kati ya hao 52 waliouawa (mwaka 2010)...bado kuna vifo vingi vya namna hiyo vinatokea (maeneo mbalimbali) lakini havijapata nafasi ya kuripotiwa...chati yetu inaonesha kuwa mauaji haya yamekuwa yakiongezeka kila mwaka ambapo kwa mwaka 2010 yameongezeka kwa kasi mno ikilinganishwa na mwaka 2008 na 2009," imesema sehemu ya ripoti hiyo na kuongeza;

  "Utafiti wetu juu ya mauaji katika Mgodi wa North Mara uliofanywa Juni, 2010 unaonesha kuwa takribani watu 19 wameuawa tangu mwaka 2009 hadi 2010.

  "Pia tumebaini kuendelea kuwepo kwa matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi na kuua watuhumiwa hasa katika maeneo ya miji mikubwa, Kanda ya Ziwa na mikoa ya Kusini.

  "Kati ya mwaka 2007 hadi 2010 jumla ya vituo nane vya polisi (Hedaru, Chato, Mbarika, Katoro, Kongowe, Makananga, Ilondele) vimevamiwa na makundi ya watu na vingine kuchomwa moto, kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

  Mbali ya vyombo vya dola, ripoti hiyo pia imebainisha uvunjaji mwingine wa haki ya kuishi, ikisema, "Utafiti wa LHRC unaonesha kuwa haki ya kuishi imeendelewa kuvunjwa kwa namna mbalimbali kama vile kuendelea kuwepo kwa hukumu ya kifo ambapo mahakama zimeendelea kutoa hukumu hiyo. Pia mauaji ya imani za kishirikina, watu kujinyonga, uhalifu wa majumbani, watu kujichukulia sheria mkononi na kuua, na ajali za barabarani.

  "Watu waliohojiwa wameeleza sababu ya kuendelea kuwepo kwa matukio ya watu kujichukulia sheria ni pamoja na ukosefu wa uelewa katika masuala ya sheria, ukosefu wa vituo vya kutosha vya polisi, watu kutokuwa na imani na jeshi hilo na serikali kutovipatia uzito stahili vitendo hivyo...mauaji ya kishirikina yameendelea kuwepo lakini jambo nzuri ni kuwa mauaji dhidi ya albino kwa mwaka 2010 hayakuwepo kabisa ingawa usalama wao bado haujawa imara kwani kuna matukio ya kuvamiwa na kutishiwa maisha yao."

  Katika ripoti hiyo, Jeshi la Polisi pia ambalo pia limetuhumiwa kuongoza kwa kuvunja haki kwa kuwatesa raia wanapokuwa rumande, kiasi cha askari mmoja kuwahi kumchoma machoni sindano ya tindikali mmoja wa watuhumiwa, limetajwa kuwa ni taasisi inayoongoza kwa tuhuma za rushwa nchini, ikifuatiwa na mahakama.

  Ripoti imesema kuwa katika taasisi zote za nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zilizofanyiwa utafiti kwa mujibuwa Ripoti ya Rushwa mwaka 2010, jeshi hilo limeshika nafasi ya tano likiwa na alama zipatazo asilimia 65.1.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mbunge wa Mhambwe (NCCR-Mageuzi). Bw. Felix Mkosamali ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa ripoti hiyo ambayo imezungumzia masala yote ya ukiukwaji wa hazi zote za binadamu nchini kwa mwaka 2010, inapaswa kufanyiwa kazi na kila mdau nchini, akisema kuwa mfumo wa utoaji haki nchini bado ni mfinyu hivyo mashirika kama LHRC yanahitajika kusaidia.

  Alisema ni wakati mwafaka sasa wakati wa mjadala wa katiba mpya, Watanzania wahakikishe kuwa haki zote zikiwemo zile za kijamii na kiuchumi zinapata nafasi ili ziweze kudaiwa mahakamani iwapo itatokea zimeminywa katika mfumo wa utoaji haki nchini.

  Mapema, Bw. Kiwanga alisema kuwa mwaka 2010 yameendelea kuwepo matukio yanayodhihirisha kuwa Tanzania bado inayumba katika utekelezaji wa kusimamia upatikanaji wa haki za binadamu, akitoa mfano kuwa wananchi wengi bado hawaridhishwi na utoaji wa haki kwa upande wa mahakama, hasa katika kuchelewa kusikilizwa na kuamuliwa.

  Alisema pia kuna ongezeko la ukatili wa majumbani dhidi ya wanawake na watoto, yakiwemo kuc homwa moto, kukatwa mikono, kunyongwa, huku pia akilaani polisi kuendelea kujichukulia sheria mikononi kwa kuua au kujeruhi raia bila kufuata sheria, akisema 'polisi wasiwe vinara wa kuua, wanapouwa wanafundisha nini kwa jamii.

  Alitoa madai mazito kuwa haki za binadamu nchini zinaendelea kuminywa wakati serikali imeshindwa kuteua au kuongeza muda wa makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ambao karibu wote muda wao umeisha tangu Desemba mwaka jana. "Haki za binadamu zitaendelea kupotea na hakuna pa kukimbilia...tangu mwka jana hizi habari ni za uhakika makamishna wote wamemaliza muda wao na hakuna appointment wala aliyeongezwa muda na hawa ndiyo wanafanya kazi za tume," alisema Bw. Kiwanga.
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wafunge ndoa na CCM?
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenifurahisha na jibu - swali lako..
   
 10. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Mbona wewe unachekesha. Kuna CUF na CCM? hujui hawa walifunga ndoa siku nyingi. Unamsikia KAF ana la kusema siku hizi? Chama kilichobaki kuwa cha upinzani ni kimoja tu. Nao wakifika mahali wakiolewa na CCM kama walivyofanywa KAF ndiyo tumekwisha watanganyika maana nchi inakwenda pumba pumba pumba tu utafikiri watu hawakwenda shule.
   
 11. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kuthibitisha ni rahisi sana. Wale walio uawa Zanzibar, Mwembechai, Arusha na Tarime waliuawa na askari, askari waliokuwa na bunduki waliwayatulia risasi raia wasiokuwa na bunduki. Askari polisi, bunduki na risasi zote ni mali ya serikali. Hivyo serkali iliuwa watu na inaendelea kuua.
   
 12. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa,wenzao CUF wametulia baada ya kuunda 'parity' na CCM,walichokuwa wakililia wamekipata so why can't they keep mum!
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  uwe unajijengea mazoea ya kusoma reports sio unatangulia mbele ku comment kama lipua lako..
   
Loading...