MSIGWA: Tanzania tunafanya vibaya kwa kukosa WANADIPLOMASIA wenye uwezo

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa ameliambia Bunge kwamba nchi ya Tanzania imekosa wanadiplomasia wanaokidhi vigezo kwenda nje ya nchi, na tunashindwa kufanya vizuri katika uchumi wetu kwa kutegemea pia watu wanaokwenda nje ya nchi.

Amesea hayo kipindi akichangia Bajeti ya Wizara ya mambo ya Nje na Afrika Mashariki ambayo ilikuwa na bajeti ya takribani billion 150, huku billion 142 zitatumika kwa matumizi ya kawaida na billion 8 kwa matumizi ya maendeleo.

Lissu kila mara analalamika nakutoa ushauri,tena mzuri,nyie mnawapuuzia kisa ni wapinzani,akisema hilohilo JPM,mnaunga mkono,be serious bhana.
Hao anaosema hawafai ndio tulio nao , kwenye ukawa kuna mtu anaweza kuwa mwanadiplomasia ?
 
Hao anaosema hawafai ndio tulio nao , kwenye ukawa kuna mtu anaweza kuwa mwanadiplomasia ? Wote vilaza na mwenyekiti wao
Wachovu kutoka kwa wachovu miaka 50! Huoni hata aibu? Hebu jaribu kuwalinganisha wabunge wote wa ccm na mmoja tu wa cdm uone ni wa upande gani unampa credit. Cdm kumejaa vichwa tena vya maana vyenye hekima na busara. Na hata wanajf walio cdm wana michango jenzi inayoelimisha na kuongoza vema kuliko wa upande huo wako wa kichovu usiokuwa na hoja za kufikirisha.
Kama sio unafiki na ulafi wenu mwenyekiti wenu angelijaza baraza LA mawaziri na watendaji wengine kutoka cdm.
Ona madudu ya mikataba mbalimbali iliyopigiwa kelele na wabunge Wa cdm inavyowasumbua leo. Laiti mngewasikiliza na kuchukua ushauri wao kipindi kile, uasingewakuta haya ya kung'ang'ania michanga huku mkiachia matofali ya dhahabu kwa shilingi 4/= kwa kila 100/=!
Endeleeni kugonga meza za bungeni lakini IPO siku meza hizo zitawagonga ninyi kwa dhuluma mliwafanyia watanzania.
Haya tuambie; ilikuwa sahihi kumpeleka ubalozi yule jamaa wa nssf au yule mnadhimu Wa .....aliyekwapua nyingi na kwenda kuzificha nedbank ya bondeni?
Tunayajua mengi ila tunawachunia tu na Msigwa kawaambia ukweli.
 
Ona sasa na wewe umenaswa na mtego wa uvyana. Hapa ndipo tatizo kubwa lilipo. Badala ya kuangalia watu wenye uwezo mnaangalia vyama. Ccm na ukawa wote ni watanzania. Kila kitu mnajadili kwa ushabiki wa vyama. Mmefanya kila kitu kama Simba na Yanga. Hatutafika ng'oo
 
Tatizo la upinzani wetu ni kulalamika badala ya kushauri.
Ninyi ndio mlioshangilia mikataba ya kifisadi huku mkiwaita akina Lissu ni walalamikaji halafu rais baada ya kuona rais anatofautiana na mikataba mliyoipigia makofi na mkasahau ni ninyi ndio mlioikubali mikataba hiyo ya kitapeli. Acheni kuwa bendera fuata upepo.
 
Wachovu kutoka kwa wachovu miaka 50! Huoni hata aibu? Hebu jaribu kuwalinganisha wabunge wote wa ccm na mmoja tu wa cdm uone ni wa upande gani unampa credit. Cdm kumejaa vichwa tena vya maana vyenye hekima na busara. Na hata wanajf walio cdm wana michango jenzi inayoelimisha na kuongoza vema kuliko wa upande huo wako wa kichovu usiokuwa na hoja za kufikirisha.
Kama sio unafiki na ulafi wenu mwenyekiti wenu angelijaza baraza LA mawaziri na watendaji wengine kutoka cdm.
Ona madudu ya mikataba mbalimbali iliyopigiwa kelele na wabunge Wa cdm inavyowasumbua leo. Laiti mngewasikiliza na kuchukua ushauri wao kipindi kile, uasingewakuta haya ya kung'ang'ania michanga huku mkiachia matofali ya dhahabu kwa shilingi 4/= kwa kila 100/=!
Endeleeni kugonga meza za bungeni lakini IPO siku meza hizo zitawagonga ninyi kwa dhuluma mliwafanyia watanzania.
Haya tuambie; ilikuwa sahihi kumpeleka ubalozi yule jamaa wa nssf au yule mnadhimu Wa .....aliyekwapua nyingi na kwenda kuzificha nedbank ya bondeni?
Tunayajua mengi ila tunawachunia tu na Msigwa kawaambia ukweli.
Toa kibanzi kwenye jicho lako kwanza! Kama kibanzi Lowasa na kibanzi Sumaye. Maana hawa wote walikuwa mawaziri wakuu pindi mikataba yote ya hovyo hovyo ilipokuwa inasainiwa.
Au hawana hata kasoro kwa sababu wapo CHADEMA? fanya fearplay ndiyo haki inavyotamka, sio kuegemea upande mmoja
 
Ccm walishaurika lini. Hata mikataba walishauriwa hawakusikia. Labda Muongo awashauri kwa kua ni blofeza
 
Toa kibanzi kwenye jicho lako kwanza! Kama kibanzi Lowasa na kibanzi Sumaye. Maana hawa wote walikuwa mawaziri wakuu pindi mikataba yote ya hovyo hovyo ilipokuwa inasainiwa.
Au hawana hata kasoro kwa sababu wapo CHADEMA? fanya fearplay ndiyo haki inavyotamka, sio kuegemea upande mmoja
hiyo fearplay u amaanisha nini? Au ulitaka kuandika Fair play? Ngumbaro Wa kugha za watu! Si muache kuandika kwa lugha hiyo Kama huijui? Cheti fake au Elimu fake mini?
 
Huna hoja ya msingi ila ni mshabiki mbuzi! Au hujui shida ya smartphone.
 
Back
Top Bottom