Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amesema baadhi ya mawaziri wameshindwa kuwa wabunifu na kupoteza uwezo wao wa kufikiri, jambo lililomfanya mmoja wao kushangaa Bakhresa kuwa na makontena 70 ya sukari bandarini.
Msigwa alitoa kauli hiyo juzi usiku wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya matumizi kupitisha bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jinsia, Jamii, Wazee na Watoto kwa mwaka 2016/17.
Msigwa alisema Tanzania imekuwa ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na watu waliodumaa, na akaitaka Serikali kueleza mikakati iliyonayo katika kuhakikisha kuwa Tanzania inaondokana na tatizo hilo.
"Na madhara ya udumavu ni watu kupoteza uwezo wao wa kufikiri, ubunifu wakulima na wafanyakazi hawawezi kufanya kazi zao. Mfano mzuri wa udumavu katika nchi hii ni pale Watanzania hata mawaziri wanashangaa eti bandarini kuona kuna makontena 70 yako bandarini."alisema na kuongeza:
"Hawaoni mtu kama Bakhresa kuwa na makontena 70 ya sukari kulingana na vitu anavyovitengeneza ni kitu cha kawaida."
Hata hivyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alikosoa uchangiaji huo ambapo alisema hoja iliyotolewa na mbunge huyo ni nzuri, lakini haiwezi kutolewa kwa vijembe na lugha ya kebehi.
"Ni waziri gani alishangaa kukamatwa kwa makontena hayo? Ama ni waziri gani amesema ana udumavu? Tukimwambia alete huo uthibitisho kwamba kuna waziri alikuwa na huo udumavu anaweza akauleta hapa," alisema.
Alisema lishe ni kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Tano kama ilivyokuwa Serikali ya awamu zilizopita, na kwamba wataendelea kutoa elimu na kujenga uwezo wa wananchi katika kuhakikisha wanapata lishe bora.
Source: Mwananchi