Msigwa: Mangula ni ndege chichidodo

Msigwa ni mwalimu wa sekondari tu hana jipya yule. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within it unless your employ armed revolution. Mangula kuwemo ndani ya wala rushwa ndo first step ya kuikomesha. Wote mliochangia humu semeni how many times mmekula rushwa au kutoa rushwa? To me Mangula is Odili Samalu and Chadema Leaders are Chief Nangas.

unacho jaribu ni kukimbizana na ukweli lakini ukweli ni kama kivuli chako hauwezi kuuacha hata kama hauutaki
 
Msigwa ni mwalimu wa sekondari tu hana jipya yule. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within it unless your employ armed revolution. Mangula kuwemo ndani ya wala rushwa ndo first step ya kuikomesha. Wote mliochangia humu semeni how many times mmekula rushwa au kutoa rushwa? To me Mangula is Odili Samalu and Chadema Leaders are Chief Nangas.

kinda la Chichidodo.
 
Msigwa: Mangula ni Chichidodo
ameyasema hayo akimlinganisha na ndege aliye tumika kwenye kitabu cha beutiful once are not yet born ambaye alikuwa anakataa kula kinyesi lakini anakula funza wanao kula kinyesi.
sawa sawa na mangula aliye chaguliwa na walarushwa lakini anasema atawatimua walarushwa ndani ya chama, ndani ya miezi 6 tu .
hapo ktk nyekundu una maanisha neno gani?
 
Umenikumbusha mbali sana! Chichidodo kwa mujibu wa riwaya ya The beutiful ones are not yet born kilichoandokwa na Kwei Amei anachukia sana kinyesi lakini ni kutoka kwenye kinyesi hicho hicho alikuwa anapenda saana kula funza wanaotoka kwenye kinyesi hicho!
BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA. Sipendi kinyesi lakini funza wala kinyesi watamu sana. we unajua alacho nyuki. Huyo mchungaji mpiga kelele tu hana jipya.
 
Watu wanakula nguruwe wakati nguruwe anakula mavi halafu wala nguruwe hawataki hata kuyagusa mavi...ha haa haaa.
 
Nimesoma Gzt la Raia Mwema la Tarehe 28Nov 2o12 na kushangazwa sana na Kauli ya Mangula kuwa Waziri Gerdon Lwenge ni Mwaadilifu Wakati Taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi wa NJOMBE imemtaja kuwa ametoa Rushwa na tarifa zipo TAKUKURU watu wanaendelea kutoa Ushahidi hadi sasa.

Hata hivyo taarifa za TAKUKURU NJOMBE zinaonyesha kuwa Kamanda wa PCCB aitwaye Richard Samila alimukamata Gerson Lwenge katika mazingira ya Rushwa na kuhojiwa kwa masaa kadhaa mnamo tarehe 31/7/2010.
Pia Kamanda huyo wa PCCB alifanikiwa kuwakamata Wafuasi wa Waziri Gerson Lwenge (SAMSON KIWEHELO,BENITO MSOVELA,HENNRY MAWATA) wakiwa na gari T542 AUJ mali ya Waziri Gerson Lwenge.

Wafuasi hao walikamatwa wakiwa na mipira ,nguo,fedha ambapo walikuwa wanagawa kwa wapiga kura ili Waziri Lwenge apite. Picha zinaonyesha wazi katika magazeti ya Mwananchi . Sasa ni kwa Vipi Philipo Mangula aseme kuwa Gerson Lwenge ni muadilifu wakati hata vyombo vya habari vimeandika kuwa alikamatwa na Rushwa?? Mangula anashughulika na Rushwa Ipi ??;

Mangula anasema alimushuhudia YONO KEVELA kwa macho yake akitoa Rushwa lakini hakutoa taarifa PCCB. Lakini pia Mangula huyo huyo ambaye ni muumini wa Nyerere alishindwa kumushuhudia GERSON LWENGE akitoa Rushwa na wala hana taarifa kuwa alikamatwa na rushwa wala hajasoma magazeti ya Mwananchi yaliyo andika habari za Rushwa.
Mimi nimefuatilia habari katika magazeti na hata PCCB hakuna taarifa zinazo onyesha kuwa Nyimbo na Kevela wametoa Rushwa au wamekamatwa na Rushwa!!!

Kama Kweli Mangula anataka kusafisha Wala Rushwa basi ni bora anze na Nyumbani kwake Njombe ambako na yeye ni Mtuhumiwa.
Nyaraka kadha za Malalamiko zinamtaja Mangula katika kashifa.
Mangula ondoa kwanza Kibanzi kwenye jicho lako Kumbuka usafi lazima uanzie nyumbani kwako Njombe na Si Arusha kama unavyo elekezwa na Summaye.

Hiii Ni habari ya mahojiano ya Mangula katika Raia Mwema:

Mwaka 2010, jimboni kwangu kwenyewe, Njombe Magharibi. Kulikuwa na wagombea watatu; Thomas Nyimbo, Kevela (Stanley Kevela ‘Yono’) na Mhandisi mmoja(Gerson Lwenge), ambaye alikuwa ni mgeni kabisa katika siasa za chama chetu, lakini Mhandisi Msomi. Nyimbo na Kevela ni wazoefu, na Nyimbo alikuwa anatetea kiti chake.

Wawili hawa (Nyimbo na Kevela) walitumia fedha nyingi kuhonga ili wapate ushindi. Ni jimboni kwangu, nami niliviona kwa macho yangu vitendo vile vya rushwa. Watu wakalalamika, chama kikajiridhisha kwamba kweli wawili hawa wameshinda kwa sababu ya rushwa. Nyimbo ndiye aliyeongoza kwa kupata kura zaidi ya 7,000, akanyang’anywa ushindi.

Baada ya kunyang’anywa ushindi, baadhi ya viongozi wetu walionufaika na fedha zake za rushswa, wakamshawishi aende upande wa pili. Wakasema NEC ya CCM yenye wajumbe wasiofika 2000 imeshindwa kuheshimu uamuzi wa viongozi wake wa ngazi ya jimbo pamoja na wanachama wake wanaofikia 7,000, kwamba hiyo ni kuwadharau viongozi na wanachama, wakamshauri (Nyimbo) agombee kupitia chama kingine.

Chama kikarejesha jina la yule Injinia. Kwa kweli alikuwa hawezi hata kumiliki jukwaa wakati wa kampeni kwa hiyo walichokuwa wakifanya wapiga debe wake, ni wao kumsemea kwa muda mrefu na kisha yeye kupewa muda mfupi tu wa kusalimia wapiga kura. Nilisema jimbo langu haliwezi kuongozwa na mbunge mtoa rushwa ili kupata uongozi. Tulipambana na Nyimbo na hatimaye tukashinda kwa asilimia zaidi ya 70, yeye akaambulia asilimia 26. Kwa hiyo, ninaposema walioingia madarakani kwa njia ya rushwa katika uchaguzi wetu huu wa ndani watanyang’anywa ushindi namaanisha hivyo, hatutanii. Tayari tumepokea malalamiko kibao hapa, tutayachambua, tutawaita wahusika wajieleze, na ikithibitika kweli kwamba ushindi wao ulipatikana kwa sababu ya rushwa, watanyang’anywa.

Raia Mwema: Suala la rushwa umelizungumza kwa mifano. Wasiwasi wangu uko kwenye kumaliza makundi, na hasa makundi ya kwenye mbio za urais 2015. Miongoni mwa wanaotajwa kuongoza makundi hayo, wanadaiwa kuwa na nguvu nyingi ndani ya chama chenu kiasi kwamba endapo mtawagusa tu, basi huo unaweza ukawa ndiyo mwisho wa CCM kushika dola. Tuambie; mtatumia njia gani kuwabaini vinara wa makundi hayo na wapambe wao, na kisha kuchukua hatua dhidi ya watu kama hao wenye nguvu ya fedha na ufuasi mkubwa ndani ya chama chenu?

Mangula: Hakuna mtu yeyote anayeweza kuchukua nguvu ya kikao. Vikao ndivyo vina uwezo usio na kikomo. Chama ni vikao. Kwa hiyo, kama kuna mwanachama yeyote ndani ya CCM au mpambe wake anayejiona ana nguvu kuliko vikao vya chama, huyo anajidanganya. Ilani ya sasa ya CCM, utekelezaji wake unaishia 2015. Utaratibu wa Chama chetu ni kwamba ikifika Mei, 2015, mwanachama yeyote anaweza sasa kuanza kutangaza nia yake ya kugombea urais, ubunge na udiwani. Lakini kuweka nia leo ya kugombea urais, ubunge na udiwani ni kuvuruga utaratibu wa Chama.

Mikakati au mechanism ya kuwabaini vinara wa makundi haya tayari tunayo. Ni kuwafungulia faili hapa ofisini na kuanza kufuatilia nyendo zao na matendo yao watakayoyafanya kuanzia sasa, na endapo mtu huyo (aliyefunguliwa faili na kufuatiliwa) atachukua fomu ya kuomba uongozi, tutamwita ndani ya vikao vyetu vya kuchuja wagombea na kumsomea madhambi yake aliyoyafanya katika harakati zake za kusaka nafasi aliyoomba kabla ya wakati.

Kamati zetu za Maadili na Usalama zitamfuatilia mhusika, na si wale tu walioko kwenye makundi ya kusaka urais, bali hata wanaosaka ubunge na udiwani kabla ya wakati nao tutawafungulia mafaili hapa. Mbunge akilalamika kwetu moja kwa moja, au kupitia vyombo vya habari kwamba kuna mwanachama mwenzake anamfanyia faulo jimboni kwake kipindi hiki cha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015, tunafungua mafaili mawili, na juu tunaandika jina la Jimbo na wahusika, halafu tunaanza kuwafuatilia nyendo zao.

Haiwezekani mbunge, badala ya kutumia muda wake kutekeleza Ilani ya Chama chetu jimboni kwake, aanze kupoteza muda wake huo kuhangaika na mwanachama mwenzake anayelitaka jimbo husika. Vivyo hivyo kwa urais 2015. Wote hao wanaotajwatajwa kuutaka urais, wanakabiliwa na majukumu ya kutekeleza Ilani ya CCM kwa sasa. Ilani yetu ndio mkataba baina ya chama chetu na wananchi, tusipoitekeleza watatuhukumu kwa kutukataa 2015.

Kwa hiyo, haiwezekani leo, mtu mwenye matamanio ya urais wa 2015, aanze kuhangaika na mbio hizo na kusahau wajibu wake wa msingi wa kutekeleza yale tuliyoahidi 2010, halafu mtu huyo ategemee kushinda. Ili 2015 wananchi waendelee kutuamini watupe tena ridhaa yao, lazima kila kiongozi na kila mwanachama atumie nguvu na uwezo wake wote kutekeleza Ilani yetu.

Msingi wa yote haya ni mmoja tu. Ili tuweze kuandika Ilani ya 2015 hadi 2020 ambayo tutainadi kwa wananchi, lazima kama Chama tufanye kwanza tathimini ya utekelezaji wa Ilani iliyopita, kwa maana ya 2010 hadi 2015 kwa sababu Ilani hiyo ndiyo itakayokuwa hukumu yetu 2015. Kuanzia sasa, lazima vikao vyetu vyote, kuanzia ngazi ya shina, tawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hadi taifa vijielekeze katika kuangalia utekelezaji wa Ilani na ahadi zetu tulizoahidi.

Ilani itakayofuata (2015-2020) ieleze ni wapi tulishindwa kutekeleza ahadi yetu na ni kwa sababu gani. Yale ambayo utekelezaji wake umekwama katikati tuwe na majibu nayo. Kazi hii ya utekelezaji wa Ilani iliyopo sasa ni kazi ya muda mrefu na ni kazi ya kudumu.

Raia Mwema: Una ujumbe gani kwa wanachama na viongozi wenzako. 2015 watarajie ushindi chini ya Sekretarieti yenu mpya hii?

Mangula: Ujumbe wangu ni mmoja tu, si kwa wanachama na viongozi wenzangu tu, bali hata kwa wapinzani wetu na Watanzania kwa ujumla. Jeshi letu (wanachama wa CCM) tunafika milioni sita. Hili ni jeshi kubwa mno ukilinganisha na majeshi ya vyama vingine vinavyoshindana nasi. Kila mmoja katika jeshi hili akitimiza wajibu wake na akafanya kazi zake za kichama kwa umahiri na umakini, mwaka 2015 tutapata ushindi wa kishindo!

Sehemu ya Waraka wa Tathimini ya Uchaguzi wa CCM NJombe 2012 :

TATHIMINI YA UCHAGUZI WA MKOA WA NJOMBE 2012
CHAGUZI ZA WILAYA
Chaguzi za Wilaya ziliingiliwa na Wimbi la rushwa kutoka kwa baadhi ya Viongozi waliopo Madarakani kwa sababu ya kupanga Safu ya Mwaka 2015 wakiwemo wabunge Wafuatao:
Mhe Gerson Lwenge(Waziri) amepanga safu katika jimbo la Magharibi ambalo limo katika Wilaya ya Wanging’ombe kwa Jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi bila kujali aliyepata nafasi ana uwezo katika nafasi hiyo au la kwa kutumia fedha nyingi ikiwemo jumuiya ya wanawake(UWT) wakishirikiana na Mhe. Diwanai wa kata ya Mdandu ANNA UPENDO GOMBELA ambaye ni rafiki yake wa Kimapenzi (nyumba ndogo) wakati pia ni mke wa Mhe CHAMBILE .

Mhe Jofrey Nyagawa ambaye ni diwani ambaye ni diwani wa kata ya Wanging’ombe na pia ni katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Wanging’ombe alihusika kugawa fedha za rushwa kupitia mtandao wa Gerson Lwenge.
Nafasi nyingine iliyogharimu fedha nyingi za rushwa ni ya Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC) na katika RUSHWA hiyo Mzee Philipo Mangula hakuwa na uwezo wa kutoa hivyo akajiondoa katika kinyang’anyiro hicho kwa kuhofia Kuangushwa vibaya.
Mhe Gerson Lwenge alikuwa anatoa Rushwa kwa wapiga kura ili NEBCHARD CHARLES MSIGWA achaguliwe katika nafasi hiyo na baadaye Mzee Philipo Mangula aliungana na Gerson Lwenge katika Mtandao huo wa Rushwa ili kumwangusha Yono Kevela ambaye ana ugomvi wa mda mrefu na Mzee Mangula.

Taarifa kutoka kwa Madereva wa magari ya waliowachukua wajumbe wa CCM Wilaya ya Wangng’ombe wajumbe walipata Shs 25,000/= kila Mjumbe Wakiwemo Kwenye magari ya USALULE TRANS na Magari matatu yaliyochukua wajumbe kwa siku ya Uchaguzi.Taarifa zaidi zimebaini kuwa Magari yaliyokithiri kwa ugawaji Rushwa huku Mzee Philipo Mangula akipewa taarifa hizo ni pamoja na

1.Dreva wa Amani : ERASTO MNYONGA (T 377ADA)
2.Dreva wa Sikinde :Fred (T481 BVJ)
3.Dreva Usalule: Bonny Kadege (T329 BED & T573ASL)
Wahusika waliokuwa wanatoa rushwa ndani ya magari hayo walikuwa wanaelekeza yafuatayo:
1. Nafasi ya Mwenyekiti achaguliwe Msigwa (asichaguliwe Hamis Nurdin)
2. Nafasi ya NEC achaguliwe NEBCHARD MSIGWA
3. Nafasi ya uenezi achaguliwe JEOFREY NYAGAWA.
Waliokuwa wanatoa fedha hizo walieleza bayana kuwa zimetoka kwa Mhe Gerson Lwenge (Waziri) na taarifa hizo zipo TAKUKURU na wanaendelea na Uchunguzi.
 
Mzee chichidodo hapa kwa wala rushwa amejitia kitanzi na trip hii akienda kuuza nyanya asishangae zitakavyomdodea...ha ha haaaaa
 
.. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within..

Itabadi utupatie vigezo zaidi ya umri wa kitabu maana kuna vitabu vya zamani ambavyo bado vimebeba kweli zenye nguvu. Mfano Biblia ni kitabu cha kale kabisa bado kinaongoza maisha ya watu wengi kwa usahihi hadi leo, Koran vile vile inaaminiwa na kuongoza maisha ya waislamu wengi hata kama ni ya zamani. Vitabu kama the wealth of the nations cha Adam Smith bado ni mama wa misingi ya uchumi wa dunia leo. Hata vitabu kile cha Darwin bado kinaaminiwa na wanasayansi juu ya asili ya viumbe. Sasa wewe unatumia vigezo vipi ku discredit The beautyful ones are not yet born?
 
Msigwa ni mwalimu wa sekondari tu hana jipya yule. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within it unless your employ armed revolution. Mangula kuwemo ndani ya wala rushwa ndo first step ya kuikomesha. Wote mliochangia humu semeni how many times mmekula rushwa au kutoa rushwa? To me Mangula is Odili Samalu and Chadema Leaders are Chief Nangas.

sazani kama ulishirikisha ubongo wako ktk kuandika haya.
Wanaojua fasihi andishi watanielewa.
 
Nyie kidhungu chenu mmejifunzia kwenye sekondari za kata au?, hiyo ni Beautiful na sio Beautyful

Usikashfu ilhali huna uhakika na unachokiandika, jina la kitabu kile ni THE BEAUTYFUL ONES ARE NOT YET BORN hiyo BEAUTIFUL unayoisema wewe sio iliyomaanishwa katika kitabu kile,hutaki unaacha, saronga mkubwa wee!
 
Last edited by a moderator:

watu wanakosea mpaka kukosoa..
Ujuaji mbaya sana!!!
 
Last edited by a moderator:
Msigwa ni mwalimu wa sekondari tu hana jipya yule. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within it unless your employ armed revolution. Mangula kuwemo ndani ya wala rushwa ndo first step ya kuikomesha. Wote mliochangia humu semeni how many times mmekula rushwa au kutoa rushwa? To me Mangula is Odili Samalu and Chadema Leaders are Chief Nangas.

hivi hapo kwenye nyekundu huoni unajizalilisha kuwa umesoma lakini hukuelimika?

nikuulize hivi bila walimu wa sekondari ungesoma chuo?

hivi kama old books ni irrellevant basi law of floatation ni irrellevant kwenye dunia ya leo.
 
Msigwa ni mwalimu wa sekondari tu hana jipya yule. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within it unless your employ armed revolution. Mangula kuwemo ndani ya wala rushwa ndo first step ya kuikomesha. Wote mliochangia humu semeni how many times mmekula rushwa au kutoa rushwa? To me Mangula is Odili Samalu and Chadema Leaders are Chief Nangas.

hujaelewa..
sasa soma hiii:

the Chichidodo is a bird. The Chichidodo hates excrement with all its soul. But the Chichidodo only feeds on maggots, and you know the maggots grow best inside the lavatory. This is the Chichidodo.’

In my opinion, the man is a hypocrite who pretends to be noble and integral by refraining from accepting bribes and yet he does not realize that his honestly earned money has its origins really in corruption.

big up Mchungaji Msigwa
 
Msigwa ni mwalimu wa sekondari tu hana jipya yule. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within it unless your employ armed revolution. Mangula kuwemo ndani ya wala rushwa ndo first step ya kuikomesha. Wote mliochangia humu semeni how many times mmekula rushwa au kutoa rushwa? To me Mangula is Odili Samalu and Chadema Leaders are Chief Nangas.

refference is made always, sio dhambi ku-reffer. kusema ni outdated hayo ni ya kwako, hayo ambayo ni modern yanayotumiwa na chama yatuondoe shidani ni yepi?
 
Msigwa ni mwalimu wa sekondari tu hana jipya yule. Beautiful Ones are not yet BORN ni old book irrelevant to the modern times. U can not change the system if u are not within it unless your employ armed revolution. Mangula kuwemo ndani ya wala rushwa ndo first step ya kuikomesha. Wote mliochangia humu semeni how many times mmekula rushwa au kutoa rushwa? To me Mangula is Odili Samalu and Chadema Leaders are Chief Nangas.

nani aliye kuambia kua ukiwa mwalimu wa secondary unakosa jipya au ndio ukilaza unakusumbua?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom