Synonyms MP
JF-Expert Member
- Jun 4, 2024
- 234
- 255
Karibu tena CCM Cde Msigwa.
Nimekusikia eti unataka chama kikupe pesa uzurule nchi nzima kunadi mabaya ya CHADEMA wenzako,
Je, hii ni habari ya kweli?
Kwanza, Mch, lazima ufahamu Watanzania na sisi wana-CCM tunajua sababu zilizokukimbiza CHADEMA kuwa ni uroho wako wa madaraka na ugumu wa maisha ya familia yako kama ipo nyingine mimi siijui.
Pili, Mch, hata hivyo wewe mwenyewe unafahamu kuwa hata wewe si mwadilifu kiasi cha kuanza kuwananga wenzako wa CHADEMA ukijua huna hiyo sifa ya kunyooshea wenzako kidole kwa lolote.
Tatu, Mch,Labda nikukumbushe hitaji la Taifa hili sio mabaya ya CHADEMA hitaji la Taifa hili ni maji, madawa, shule, zahanati ,barabara na mengine mengi ambayo mama Dkt Samia Suluhu ameyafanya Kwa kiwango kikubwa nenda kayaseme haya nitakuunga mkono kwa lolote.
Nne, Mch, Usidhani CCM tumesahau matusi uliyotutukana hivi majuzi kule SINGIDA na rafiki yako LISSU acha kututonesha kwani mmembagua sana Rais kwa Uzanzibar wake inatuuma.
Tano, Mch, hebu kaa kwa kutulia na hakuna UDC Wala Ubunge tutakupa kwa sababu hata sisi pamoja na kukipigania chama chetu hatuna hizo nafasi mpaka Sasa, hivyo tulia.
Sita, Mch. kaa kwa kutulia tunakufahamu vizuri pengine kuliko unavyojifahamu tuache tuone kama kweli wewe sasa ni CCM au bado ni rangi mbili tu.
Saba, Mch, kumbuka hii sio CCM ya Magufuli lazima utambue kisha ukae kwa kutulia kwani mama anazo 4R zisome uzielewe.
#Kidumu Chama Cha Mapinduzi.