Msigwa Avumbuwa Dawa Mbadala ya UKIMWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msigwa Avumbuwa Dawa Mbadala ya UKIMWI

Discussion in 'JF Doctor' started by zomba, Jul 30, 2012.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Dr. T. R. Msigwa, baada ya miaka 12 ya utafiti amehitimisha hatua yake ya mwanzo ya utafiti na amevumbuwa dawa mbadala ya UKIMWI kutokana na miti shamba na samaki.

  Kwa mujibu wa Dr. Msigwa, dawa hiyo kwa jina la 4A9 Medicine, anasema imepata baraka zote za Mkemia Mkuu na TFDA.

  Msikilize mwenyewe anasemaje: Dr. Msigwa, Radio Imaan - YouTube
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Habari njema if it real works....nimesikia mataifa makubwa(scientists) huko New York yanahaha na bajeti ingawa wamejipambanua kwamba wamefikia mahala pazuri kufight against virus..

  So let this be good news globally.
   
 3. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  another scammer
   
 4. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,021
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Huyo aangaliwe vizuri asituletee mambo ya kubahatisha kama yale ya Babu wa Loliondo.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyu dawa yake sio ya miujiza kama ya babu wa samunge. Hii anadai kwenye kitabi chake (ambacho nakisoma sasa hivi) kuwa imefanyiwa utafiri kwa miaka 12 na humu kwenye kitabu ana data za utafiti.
   
 6. paty

  paty JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,253
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  ha ha ha ha bibi wa tabora, kijana wa mbeya na babu wa Lo....****o , simaliziii wananchi wasije wakanipiga mawe
   
 7. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Japo tunahitaji sana dawa ya VVU, lakini hawa watu wa mitishamba wanatudanganya sana. Hawajui hata pathophysiology ya HIV na wanaleta uongo wa kuvumbua dawa. Ulaghai tupu. Hata jina la dawa yake linaonesha ushamba wa kung'ang'aniza kuingiza neno la kiingereza. Ni kama vile mvumbuzi wa Quinine, angeiita Quinine, Quinine Medicine. Hakuna kitu hapo.
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kitabu kitabu....hata mimi naweza kuandika kitabu and convince you. Kwanini utafiti huo pia usifanywe na expert wengine ikithibitika na afanye patent ya dawa yake akaokoa mamilioni ya watu duniani.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Amefanya na watafiti wengine wengi tu, sasa kwaa upande wake amemaliza awamu ya kwanza ya utafiti wake na daawa imepimwa na kuonekana mjarab, kwa sasa ni mtu mwenye matatizo anapima, anapewa dawa anaeleza matokeo within the first two weeks (kwa mujibu wa hizo kanda zake kama umezisikiliza).

  Kwanini hauzisikikilizi halafu kama una maswali kaweka namba yake hapo hapo kwenye youtube.

  Excerpts za kwenye kitabu:

  Jaribio la kutibu wagonjwa wenye VVU kwa kutumia dawa hii (4A9 Medicine) lilifanyika kwenye mikoa mbalimbali Tanzania ikiwemo; Kigoma, Dar Es Salaam, Tanga, Iringa, Mtwara, Zanzibar, Morogoro, Shinyanga, Arusha, Mwanza.

  Msikilize: http://www.youtube.com/watch?v=EzLnnwr6EJk&feature=plcp

   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ulitaka lazima awe sawa na aliyevumbuwa Quinine? Tatizo hauna ubunifu, mwenzenu ndio hiyo dawa anayo, kama una matatizo muone tu. Sisi ujumbe tumefikisha, usije kusema hujaambiwa!
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Dk. Msigwa hajapata Baraka ya kutibu Ukimwi – Bodi ya Madawa


  Na Fatma Kassim, MaelezoBODI ya Chakula Dawa na Vipodozi imesema kuwa haijampa Baraka Dk. Msigwa ya kuwa dawa yake inatibu Virusi vya Ukimwi au kupunguza virusi hivyo.Mrajis wa Bodi hiyo Dk Burhan Othman Simai alisema dawa ya daktari huyo imefanyiwa

  uchunguzi na maabara yake na kugundua kuwa haina sumu, na sio kutibu ukimwi.
  Alisema kitengo cha kuitangaza dawa yake hiyo inajulikana 499 medicine kuwa inatibu ukimwi si jambo zuri na linapotesha umma na kuonekana ni mtibabu wa maradhi hayo na wakati

  dawa yake hiyo imeandikwa kuwa inatibu Kisukari, kuondoa uchovu na sumu mwilini.
  Amewataka wananchi kuwa makini na matumizi ya dawa hizo ambazo nyengine hazina viwango na kudai kuwa zinatubu ukimwi jambo ambalo si sahihi kutokana na kuwa dawa ya kutibu VVU

  haijapatikana mpaka sasa.
  Kwa upande wake Mrajis wa Tiba asili na tiba Mbala Mohammed Omar Mohammed alisema kuwa kutokana na Dk Msigwa kudai kuwa dawa yake inatibu Ukimwi baraza hilo limemtaka awapeleke wagonjwa aliwaowapatia matibabu jambo ambalo

  ameshindwa.
  Alifahamisha kuwa baraza lake limemtaka afuate taratibu na asitangaze dawa zake kuwa zinatibu Ukimwi pamoja na kufanya usajili upya na kutibu kwa tiba asili.Aidha baraza hilo la tiba asili limetaka Dk Msigwa kuwa lugha anayotumia katika kipindi chake cha Radio

  Adhana JITAMBUE airekebishe na asiiseme kuwa “dawa yake inatibu Virusi Vya Ukimwi na badala yake aseme kuwa inayopunguza maradhi nyemelezi yanayoambatana na Virusi Vya Ukimwi au dawa inayoongeza kinga ya mwili , CD4”.
  Aidha alifahamisha kuwa hatakiwi

  kuwaachisha wagonjwa walioanza dawa za ARV kwa kutumia dawa yake hiyo ambapo anaweza kuwasababishia madhara makubwa.
  Dk. Msigwa hajapata Baraka ya kutibu Ukimwi – Bodi ya Madawa | Ministry of Health Zanzibar
   
 12. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mara ngapi unamsikia mtu akijenga hoja asikilizwe husema "Katika utafiti wangu nimegundua kwamba...."? Wanajisemea tu mara nyingi, utafiti una nidhamu yake, yeye aandike na jopo la wanasayansi liyapitie na kupitisha maandiko yake tujue utafiti wake ni utafiti kweli. Sio porojo. Hizo tumezisikia nyingi na mbado.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hao ma scientist wanangoja nini? si ndio kina mkemia mkuu waliyoipima hiyo dawa na kusema ni salama? si ndio kina tfda hao? sasa na wewe kwanini usihahakikishe ?
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii ina maana wanaitambuwa rasmi kuwa dawa hii ina manufaa na inaonaongeza CD4. Hata mimi nimesiikiliza mikanda ya huyu Msigwa na nimeona anasema kuwa dawa yake inaongeza CD4 kwa wingi na kwa muda mfupi kuliko dawa nyingine yoyote iliyoko madukani kwa sasa, iwe ya hospital au ya mitishamba.

  MziziMkavu, mbona hiyo taarifa ulyoleta inajichanganya? hivi kuna dawa gani inayotibu VVU? mimi sijawahi kusikia, nnachojuwa anaetibiwa ni mgonjwa wa VVU kwa kumuongezea kinga mwilini CD4 na kupunguza VVU mwilini (viral load). Sasa uanze kutibu VVU ili vishambulie zaidi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Zomba, unaweza usinielewe nasema nini leo hii, lakini kuna siku hapo baadaye utanielewa nasema nini. Hata yule bwana wa Formula one kule ubungo alisema kama alivyosema huyo bwana, lakini haikuchukuwa muda kukawa na ugomvi mkubwa sana na wanasayansi. Unajua, mara nyingi hao mabwana hutumia majinamakubwa sana ili bidhaa zao zipate kuaminika. Sasa kwa kuwa watanzania ninavyowafahamu kutopenda kutafuta majibu sahihi na kwa subira kwa maswali magumu, wanapokea maneno hayo na kuanza kuyafanyia kazi kwa kmtafuta na kujikuta baadaye wamepotea, halafu ndipo wanaanza kulaumu serikali ilikuwa wapi wakati tunasikia kwenye vyombo, rais kwa nini amechagua wasaidizi wabovu, nk. Kumbe ni ujinga wetu unaotumaliza sisi wenyewe, bahati mbaya marehemu harudi tena kuja kutusimulia ilivyotokea akafa kijinga (kama ni kijinga kweli).

  Kuna taratibu na mlolongo mrefu sana juu ya tiba kama hiyo hata ikubalike. TFDA hawana sauti ya mwisho katika hilo. Kwa kweli hata wizara haina sauti ya mwisho, lazima WHO wakubaliane kwanza kufanyia majaribio kwa mwili wa binadamu baada ya kutafiti nje ya mwili na kisha kwa wanyama wanaofanana fanana na mtu, ndipo ipitishwe kwa kujihakikishia kwamba inayo nguvu asilimia ngapi kupambana na ugonjwa na kwa namna gani, athari yake nini kwa matumizi na namna ya kudhibiti athari hizo, na mambo kadha wa kadha. Sasa huyo bwana ametafiti miaka 10 ndio leo tunamsikia yeye, umewasikia TFDA wakitangaza au yeye ndio anakuambia. Unayaamini maneno yake asilimia ngapi? Wangetangaza hao anaowasema kidogo ningekua na chembe ya imani naye. Lakini huenda kweli inatibu, dawa nyingi mbadala zinatibu magonjwa mengi, lakini tunashindwa kufika mwisho sababu ya kukurupuka kwenda sokoni hata kabla ya matokeo ya mwisho. Hata Alovera na Mlonge vinaweza kuongeza kinga mwilini na kwa kufanya hivyo kudhibiti virusi vya ukimwi, hata hivyo mtu akitoka mkuku kututangazia dawa hiyo inatibu sikubaliani mpaka nipate majibu. Tena unaniambia nitafiti mimi, haisaidii, nami nikitangaza sitakuwa tofauti na mganga wa jadi huyo.

  Pale Muhimbili kuna kitengo cha madawa asili, ingawa nao ni wachakachuaji sana na pametokea malalamiko mengi kwa waganga wa jadi wanaopeleka dawa zao pale wanakatishwa tamaa na kuibiwa siri ya dawa hizo kwa sababu ya kutokuwa waaminifu tu. Lakini ndo chombo pekee rasmi inabidi ugangamale, wizi upo kila kona.
   
 16. c

  chomboko New Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  teh! teh!
  sound tu hizo! tumesikia wengi... wakaja wakapita... kisha wakapotea!!!

  chomboko
   
 17. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Dawa akivumbua Mzungu ni Dawa, akivumbua Mwafrika ni Uchawi.
   
 18. kirumonjeta

  kirumonjeta JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 3,075
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Mvumbuzi lazima awe mzungu au,hebu tumpe moyo mwenzetu huyu kuliko kumkandia
   
 19. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hii kali!
   
 20. SASATELE

  SASATELE Senior Member

  #20
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe zomba mbona unatetea sana. Nahisi wewe ndio Dr Msigwa mwenyewe. Haiwezekani ujibu almost kila hoja inayochallenge kama huna maslahi na hii issue!! sema tu kaka!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...