Msigwa anataka Serikali iliyoko madarakani imuoneshe japo kiwanda kimoja

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Leo katika bunge Mh Msigwa anataka serikali iliyoko madarakani imwonyeshe japo kiwanda kimoja kilichojengwa hadi sasa na Serikali ya Magufuli. Waziri wa viwanda akiweza kumwonyesha, atampa landcruiser yake! Du, bonge la hoja, hahahaaaaa!
 
Kha hivi huyo mbunge ana elimu gani??? Hivi anafahamu hadi kiwanda kijengwe na kuisha kina chukua mda gani? Na kabla ya hapi kina pitia mikakati gani hadi uamuzi utolewe? Mtu hukurupuki tu ukasema HAYA HAPA TUNAJENGA KIWANDA.
Angalau ageuliza Mh Magufuli hadi sasa amesha anzisha au kuweka mikakati gani ya maendeleo?
 
Haki ya cjui nani, kuna cku aliniboa kwenye kipindi cha 45 mins cha ITV alipoulizwa swali very simple: "Tangu Serikali ya JPM iingie madarakani na sera yake ya "nchi ya viwanda", ni hatua gani nchi yetu imefikia kwenye hiyo sekta ya Viwanda? Akajibu kuwa: "viwanda vinakuja toka Korea, China, etc! Nilitamani kama ningekuwepo studio nisaidie kujibu kuwa: Tumekutana na Wadau wa Nje na Ndani na wapo kwenye process ya kuanzisha viwanda (wale wa nje) na wengine kurudisha au kuuza share za viwanda walivyo navyo kwa wengine baada ya kushindwa kuviendeleza ili vilete tija iliyokusudiwa. Na kama watashindwa kufanya hivyo basi hatua so & so zitafuata, tumepeana muda wa so & so!"
 
Kwa busara ndogo si vyema kulaumu au kukebehi bila ya kutoa mchango wa jinsi ya kufikia uchumi wa viwanda mapema iwezekanavyo.

Viwanda ndiyo mama wa maendeleo. Nchi zilizoendelea zilipitia kipindi cha "industrialisation or industrial revolution".

Mawazo ya Wabunge yaelekezwe huko - "towards industrialisation" km

1) kuwekeza kwanza kwenye miundo mbinu kuwezesha usafirishaji malighafi, mazao nk kwenye viwanda
2) kuimarisha kilimo kwa ajili ya kutoa malighafi ya viwanda.
3) kupanua elimu ya ugani na stadi za maisha kumudu mahitaji ya kilimo na viwanda
4) na kadhalika
 
Una point, ila ninachomaanisha ni kuwa niliamini kwa mtu mwenye phd tena ya sayansi (kemia) angechagua mtu ambaye ni extraordinary kwenye sekta hii kwa kuwa hiyo ndio ilikuwa slogan yake na naamini ilichangia kwa kiasi kikubwa kumpa credits wakati wa kampeni na sio kutuletea mtu ambaye anajaa kwenye viganja vyetu! Kama ilihitaji na sisi wapiga kura tuingie na kusaidia baada ya yeye kuingia Ikulu angeweka wazi kuwa "nataka tushirikiane kupanga watu kwenye wizara". Kusingekuwa na shida.
 
Kunahitajika viongozi wazalendo na hodari kutekeleza yaliyomo kwenye siasa na sera za maendeleo, kwa kuzingatia sheria. Naamini uteuzi wa Mawaziri umepitia vigezo tosheleza kupata viongozi bora.

Pamoja na hilo, "industrialisation" huenda sambamba na kulinda viwanda vya ndani, bila hivyo nguvu zote zitaishia kwenye karatasi.

Kwa hayo machache, Serikali ya awamu ya tano, iko kwenye njia sahihi. Mimi na wewe unayesoma haya, tutimize wajibu wetu mahala petu pa kazi.

KUPANGA NI KUCHAGUA. WAKATI NDIYO HUU
 
pamoja na hayo si sahihi serikali kufanya biashara... jukumu lake kuu ni usimamizi
 
Aache kusumbua watu, kwanza amepimwa akili au vp
ImageUploadedByJamiiForums1462579217.624507.jpg
 
Kha hivi huyo mbunge ana elimu gani??? Hivi anafahamu hadi kiwanda kijengwe na kuisha kina chukua mda gani? Na kabla ya hapi kina pitia mikakati gani hadi uamuzi utolewe? Mtu hukurupuki tu ukasema HAYA HAPA TUNAJENGA KIWANDA.
Angalau ageuliza Mh Magufuli hadi sasa amesha anzisha au kuweka mikakati gani ya maendeleo?
Huyu Mbunge hana hoja siku hizi!
 
Eti huyu mbunge hana akili! Kama ni rahisi wawekezaji kuanzisha viwanda,mbona tumeua viwanda vingi kwa njia hihii ya uwekezaji?
 
Serikali haina ulazima la kujenga kiwanda.... jukumu lake ni kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kwenye viwanda

Inasikitisha sana kuona washauri wa JPM wanashhindwa kuiweka hii hoja vizuri... role ya serikali si kufanya biashara, bali kusimamia biashara
Inawezekana waziri hafahamu hivyo, na hata huyo msigwa hajui pia, na ndio maana ya uchumi wa soko.
 
Msigwa Msigwa, nlikua nakuheshimu sana aisee ila sasa umeanza kua mpuuzi, umekaa miaka mitano Iringa kama Mbunge wa Chadema lakini ulishindwa hata kujenga ofisi ya Chama ya kueleweka mjini.

Leo hii unataka Rais ndani ya miezi sita awe keshaanzisha kiwanda. Umetia aibu sana, unafikiri kiwanda ni sawa na kuanzisha bustani ya mchicha? Una elimu gani Msigwa tukiachia mbali hyo ya uchungaji?

Daaah, naiona Chadema yangu ileeee, inaanza kosa hoja!! Aya bhana
Huyu Mbunge hana hoja siku hizi!
 
Jana nilimsikiliza huyu msigwa na wabunge wengine wa chadema kusema kweli wanapwaya. Naona sasa hivi hawana hoja wemekua vioja. Nawasihi wapinzani wajipange upya maana hoja ni nzito zipo juu ya uwezo wao.
 
Back
Top Bottom