Msigwa amlilia mwangosi, asikitishwa na ukimya wa viongozi wa nchi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msigwa amlilia mwangosi, asikitishwa na ukimya wa viongozi wa nchi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamandamakini, Sep 18, 2012.

 1. k

  kamandamakini Senior Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 158
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]

  Mh Peter Msigwa akiongea na wanahabari ofisi kwake leo

  Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini kupitia CHADEMA mh Peter Msigwa amesikitishwa kuona viongozi wakuu wa serikali kukaa kimya kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi.
  Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Msigwa amesema amesikitishwa sana na kifo cha Mwandishi mwangosi kwani hata kilipotokea yeye alikuwa safarini kuelekea Ujerumani lakini kwa kuufahamu mchango mkubwa aliokuwa nao Mwangosi katika kutetea haki kwa wananchi wa Iringa na tasnia ya habari ilimbidi ahairishe ili kuweza kutoa pole kwa familia ya marehemu.
  Ameeeleza kuwa yeye kama mbunge amesikitishwa sana na kuona viongozi wakuu wanchi kama rais kutozungumzia suala hili na haswa kwa viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya ambao marehemu alikuwa akifanya nao kazi kwa karibu sana.
  "Nimesikitishwa sana kuona kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa kuzidi kuwepo ofisini kwa lile lilitotokea, mikono ya kamuhanda na mikono ya Said Mwema imejaa damu, na mimi naungana na wanahabari kuugomea uongozi wa RPC Iringa" alisema.
  Ameongeza kuwa anasikitiswa sana Meya wa manispaa wa Iringa Amani Mamwindi kuhusika katika utoaji wa amri ya kuvunjwa kwa vijiwe vya wananchama wa CHADEMA. "Meya ametoa amri ya kubomoa vijiwe vya chadema akieeza kuwa ni amri ya jiji na kuacha jukumu lake kubwa la kuhakikisha kuwa takataka za mji zinatolewa na kuhakikisha uchumi unaendelea na badala yake kuhusika kubomoa vijiwe vya wanachama pamoja na kutoa bendera na hatutaruhusu hali hii iendelee" aliongeza msigwa.
  Kuhusu yeye kutoonekana kuwajibika jimboni na kuwa na ziara nyingi za nje Msigwa amesema haendi huko tuu kwa maslahi yake binafsi ila anafanya ili kujifunza mambo mengi ambayo yatakuja kuwasaidia wananchi baadae nahii inatokana nayeye kuwepo katika uongozi wa katika wizara mbalimbali ambapo ziara hizo zina maslahi kwa jamii nzima.
  Kutokana na hali hiyo mbunge huyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano utakaofanyika katika eneo la soko kuu kuanzia saa nane kamili na kuongea na wananchi kuhusiana na mambo mengi yanayohusiana na maendeleo ya jimbo.

  chanzo: MH. PETER MSIGWA BLOG
   
 2. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kuhusu kifo cha Daud yameisha semwa na kufanywa mengi sana sio lazima kila kiongozi aseme! ifike mahali tuache hili jambo lishughulikiwe, na majibu ya Msigwa kuhusu kutofanya chochote jimboni kwake kwa kisingizio cha safari za kujifunza anatofauti gani na baba mwanaasha!
   
 3. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huyu mbunge ni mchapakazi sana anastahiki pongezi kwa hakika
   
 4. v

  vangilichuma Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  msigwa hii ndoo tanzania bwana watu tunauwawa kama buzi 2015 ndoo mwisho wa kuuwana ovyoo bwana
   
 5. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala la mwangosi liko mahakamani.
   
Loading...