Msigwa ameshanasa kwa Nyalandu

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
16,207
7,570
Jambazi ni jambazi, fisadi ni fisadi, tapeli ni tapeli tu. Madhara ya vitendo vya watu hawa kwa jamii ni yale yale bila kujali kuwa wanatoka
chama tawala au upinzani. Madhara ya vitendo hivi hayaangalii kuwa mtu huyu anajifanya mchungaji, askofu au sheikh.

Hayaangalii kwamba mtu huyu anapenda kuuza sura kwenye runinga kiasi gani. Na wala hayazingatii kuwa mtu huyu anapiga kelele bungeni kiasi gani au anajua matusi kiasi gani.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho chama kikuu cha upinzani nchini. Matarajio yao ni kushika dola, na ndiyo maana siku zote wako mbele kuanika udhaifu na upungufu uliomo ndani ya chama tawala.

Ndiyo maana karata dume inayochezwa na Chadema na vyama vingine vya upinzani sasa hivi ni UFISADI wa ESCROW unaonasibishwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Sina mgogoro na hilo. Ni wajibu wao na kama kweli wana nia ya dhati kututoa hapa tulipo na kutupeleka katika nchi ya asali na maziwa, basi wajitahidi kuhakikisha hili la Escrow na ufisadi mwingine yanafikia mwisho.

Inatosha sana kwa uongozi wa juu wa Chadema kutafakari juu ya hatua waliyochukua wana-Chadema wa Iringa kwa kumuengua Msigwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea uenyekiti wa wilaya. Sababu zilizotolewa kwa kuenguliwa Msigwa ni kujifanya msomi na mjuaji wa kila kitu; mtu aliyejaa dharau na mchache wa kukubali kushauriwa, miongoni mwa sababu nyingine.

Msigwa hajataka kujifunza chochote na bado anajihesabu kuwa na mvuto kwa wananchi wa Iringa! Nitahadharishe kuwa kama Chadema wamelichoka Jimbo la Iringa Mjini, basi wampe Msigwa kijiti.

Kupitia mikutano iliyo rasmi na ile ya vijiweni, upinzani unaonekana kuwa na ajenda nzuri na nia ya dhati kutukwamua kutoka hapa tulipo.

Hata hivyo, upinzani utafanya makosa makubwa kama wataamini kuwa wananchi tunawapima kwa maneno yao matamu tu. Wananchi wanaona vitendo vyao au vya baadhi ya viongozi wa upinzani.

Peter Msigwa (nasita kumwita mchungaji au mheshimiwa), ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Ni mmoja wa viongozi wa Chadema, chama kinachoonekana mbadala wa CCM.

Komredi Freeman Mbowe amempa Msigwa kazi kuhakikisha kuwa anachunga rasilimali zetu zisifujwe na kuharibiwa hovyo. Naamini kwamba Komredi Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hakumtuma Msigwa kwenda kuunda genge la ulaji na mafisadi; kwenda kutetea uhuni unaofanywa na baadhi ya watu na wala kwenda kutafuta utajiri kwa kutumia kofia ya uwaziri kivuli.Hiyo ni dhamana na lazima aitunze na aipe heshima yake.

Naomba nisitafune maneno kwamba kama Chadema kweli inataka kuendelea kuaminika mbele ya Watanzania, basi ingeonesha mfano kwa kuwawajibisha watu ambao wanaonekana kukitia najisi chama kama mchungaji huyu.

Katika kipindi cha runinga ya ITV kinachojulikana kama ‘Dakika 45' Desemba 8,mwaka huu, Msigwa ndiye aliyekuwa mgeni wa kipindi.

Katika maswali aliyoulizwa ni pamoja na baadhi ya kashfa zinazomhusu Lazaro Nyalandu na James Lembeli.

Kwanza, mtangazaji alitaka kujua kulikoni, kwani siku za nyuma Msigwa alikuwa akipigia sana kelele Wizara ya Maliasili na Utalii, lakini siku hizi amekuwa bubu.

Jibu la Msigwa likawa eti Waziri Nyalandu ametumia ‘approach' nzuri tofauti na wenzake ambako anamwalika katika shughuli na hafla mbalimbali na hivyo hana sababu ya kuongea!

Hivi mtu mwenye akili anaweza kutoa jibu la kipuuzi kama hili? Ukweli ni kwamba hii haina tafsiri nyingine zaidi ya ukweli kwamba Msigwa anakiri kuingizwa kwenye ulaji, kwa hiyo hawezi tena kupiga kelele!

Vinginevyo, atuambie kwamba unapofadhiliwa unapata wapi ‘moral authority' ya kumkemea mfadhili wako.

Jibu jingine lililotia kichefuchefu ni utetezi wake juu ya matumizi mabaya ya Leseni ya Rais iliyoruhusu kuuawa wanyamapori zaidi ya 700.

Msigwa anadai kuwa si kweli kwamba eti marafiki hawa wa Nyalandu wameua wanyama 700, bali waliua nyati watano tu na pundamilia wawili.

Akadai kuwa picha za watoto wadogo waliokuwa wanawinda zilizotoka katika gazeti la JAMHURI hazikuwa zao! Huyu mbunge ni wa ajabu kabisa!

Mchungaji gani mwongo namna hii? Ambacho hakusema kuwa hakikuwa cha kweli ni juu ya nakala za vibali na nyaraka zilizokuwa gazetini.

Halafu akawafagilia Wamarekani hawa kuwa ingawa hawakutakiwa kulipa,waliamua kulipa pesa nyingi sana serikalini! Kwa mara nyingine, nashangaa ni vipi mtu anayejiita mchungaji anaweza kuwa mwongo kiasi hiki!

Kwanza, Msigwa ameupotosha umma kwa makusudi kuwa eti JAMHURI iliripoti kuuawa wanyama 700. Hamna aliyeripoti kuwa wanyama 700 wameuawa. Tulichoandika ni juu ya Leseni ya Rais iliyoruhusu kuuawa wanyama 700.

Na ni baada ya JAMHURI kuripoti uhuni huu ndipo Wamarekani hawa walipoamua kutimka na kurudi kwao huku wakiwa wameua nyati watano.

Jibu alilotakiwa kujibu kibaraka huyu wa Nyalandu na Wamarekani ni endapo kulikuwa na uhalali wa kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Friedkin (je, wana sifa hizo?) Leseni nane zilizotolewa ziliruhusu wanafamilia wanane kuwinda wanyama 49 kila mmoja. Kwa hesabu za msomi Msigwa jumla ya wanyama wote itakuwa saba!

Kwa kuwa Msigwa ameamua kuwa kuwadi wa Nyalandu na Wamarekani, basi angetusaidia zaidi kujibu maswali mengine tuliyouliza yakiwamo yale ya uhalali wa Nyalandu kugawa vitalu kinyume cha sheria kwa marafiki zake hawa.

Itakumbukwa kuwa mara tu baada ya kuibuka kashfa hii ya matumizi mabaya ya Leseni ya Rais, tulitabiri kuwa si Msigwa wala Lembeli ambaye angenyanyua mdomo kukemea ufisadi huu. Tuliweka wazi kuwa hili lisingewezekana kutokana na kujengeka kwa mtandao wa ulaji kati ya wawili hawa na Nyalandu.

Uswahiba wa kampuni za Friedkin na Nyalandu na Lembeli unaeleweka. Tuna taarifa juu ya ufadhili wa ndege alizokuwa anapanda Nyalandu kwa shughuli zake binafsi.

Kwa upande wa Lembeli, mfano mmoja ni ile hadidu ya rejea aliyojitengenezea kwenye ripoti ya Operesheni Tokomeza akitaka Mkurugenzi wa Wanyamapori awajibishwe kwa kuwa eti rafiki zake hawa wamekosa kitalu walichokuwa wanakitaka huko Makao WMA!

Ingawa suala hili halikuwa na uhusiano kabisa na ujangili, Lembeli hakuona soni kuliweka kwenye ripoti ili kuwafurahisha Nyalandu na mawakala zake Wamarekani.

Huhitaji akili nyingi kugundua kuwa Msigwa naye ameingizwa kwenye ulaji wa kampuni hizi; na kuingia kwake humo kumekuja kutokana na haja ya kumtumia kufanikisha unyang'anyi wa kitalu cha Green Miles ambacho Nyalandu kawakabidhi Wamarekani bila kufuata sheria za nchi.

Katika hali kama hiyo ambako Msigwa tayari kageuka bidhaa, tunatarajia angethubutu vipi kusema lolote kuhusu uharamia wa Wamarekani hawa kuruhusiwa kuua wanyama wetu 700?

Ujasiri huo atautoa wapi? Ni kwa sababu hiyo hiyo Msigwa aliamua kuufyata ghafla juu ya ile kashfa ya Nyalandu kuamua kurefusha msimu wa uwindaji ili kuwafurahisha Wamarekani hawa waliotaka waruhusiwe kuwinda mwaka mzima.

Awali, Msigwa alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kulaani kitendo kile akikiita ufisadi. Lakini huhitaji akili nyingi sana kugundua kuwa
baada ya kuingizwa kwenye ulaji, hakuwa na ujasiri wa kusema chochote na ndiyo maana hata kwenye hotuba yake ya bajeti aliipotezea.
Atasemaje wakati kusema ina maana kugusa maslahi ya waajiri wake?

Swali juu ya mpango wa Nyalandu na Lembeli kuuza mbuga na hifadhi za Taifa, Msigwa anawatetea maswahiba wake hawa akidai kuwa ni upuuzi mtupu na kwamba eti tulitaka kuuza gazeti tu!Afadhali basi Msigwa angeamua kukaa kimya kuliko kuropoka upuuzi huo.

Lakini kwa kuwa ameamua kuwa kuwadi na msemaji mkuu wa mabwana hawa,basi angejibu maswali ya msingi yaliyojitokeza kwenye makala zetu kadhaa kuhusu kashfa hii.

Atuambie rafiki zake hawa walifuata nini Afrika Kusini hata baada ya kupata ushauri wa kitaalamu juu ya hatari ya African Parks Network
(APN)? Atuambie ilikuwaje Lembeli ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Bodi ya APN (asasi inayotaka kukabidhiwa mbuga zetu) aiwakilishe Serikali kwenye mapatano na asasi hiyo.

Kama akili ya Msigwa haiwezi kuyaona hayo, basi hatuna budi kurejea kuhoji ule utata wa kupata ‘division zero form four' na hatimaye kutunukiwa digrii ya uchungaji!Lakini wakati tunashangaa majibu ya kipuuzi ya Msigwa kwa maswali ya Emmanuel Buhohela wa ITV, kuna haja ya kurejea historia yake kwa ufupi ili tujue kuwa huyu ni mtu wa namna gani.

Peter Msigwa amekuwa akijipambanua kama kiongozi wa dini msomi mwenye digrii (graduate),ingawa wapo wanaohoji uchungaji wake na kutaka kujua kuwa ni chuo kikuu kipi ambacho hupokea wanafunzi waliofeli. ‘Mtumishi huyu wa Mungu na msomi' ndiye Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii.

Alhamisi, Februari 13, mwaka huu, Nyalandu alipomjibu Martin Fletcher kutokana na makala yake kuhusu ujangili kwenye gazeti la Daily Mail,Msigwa alimjia juu huku akimtuhumu kuwa anawabembeleza majangili ambao wanafahamika kwa majina na wapo mitaani wakiendelea na ujangili.

Msigwa alibainisha kuwa mara nyingi Nyalandu amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akidai kuwa mtandao wa ujangili unafahamika na ni mpana unaohusisha watu wenye nguvu za pesa na huku akiwaomba wanaojihusisha na biashara hiyo waachane nayo mara moja.

Akasema kuwa kauli hizo za Nyalandu zinaonesha dhahiri kuwa kuna watu hawaguswi na sheria na wapo juu ya sheria.

Msigwa akasema: "Majibu haya ya Waziri (Nyalandu) yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaolalamikiwa na kuogopwa ndiyo unaohusisha Ikulu, wanasiasa, watumishi wa Serikali, maafisa wanyamapori, maafisa usalama, polisi, wanajeshi, pamoja na wafanyabiashara wakubwa, ambao wamekuwa wakijihusisha na Serikali ya CCM."

Akaendelea kumponda Nyalandu kuwa anatumia hisia badala ya vielelezo kujibu hoja. Akatuhumu kuwa Serikali haichukui hatua kwa wahusika ambao wanajulikana kwa majina na wako mitaani wakiendelea na biashara hiyo haramu kwa kuwa wanatafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Machi 23, mwaka huu, Msigwa alitoa taarifa kwa umma iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosema: "Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mazingira ya rushwa na ufisadi katika sekta ya uwindaji nchini." Katika taarifa hiyo, Msigwa alisema: "Ndugu wanahabari, kati ya mambo yanayoashiria mazingira ya rushwa katika sekta ya uwindaji hapa nchini ni kitendo cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kurefusha, kinyume cha sheria, muda wa msimu wa uwindaji kuanzia tarehe 1 Julai hadi 31 Machi kila mwaka tofauti na muda wa kisheria ambao ni kuanzia tarehe 1 Julai hadi 31 Desemba kila mwaka.

Waziri Nyalandu ametoa agizo la kurefusha msimu wa uwindaji tarehe 19 Machi, 2014 akiwa na wamiliki wa vitalu na makampuni ya uwindaji." Aidha katika taarifa hiyo Msigwa akasema: "Ndugu wanahabari, jambo linaloashiria mazingira ya rushwa zaidi ni kwamba wenye makampuni ya uwindaji wamemmwagia sifa waziri na kusema kuwa ni mtu makini na msikivu.

Jambo hili la wenye makampuni kufurahia uamuzi wa waziri linaonesha japo kwa mazingira kwamba wenye makampuni hao walikuwa wakitafuta kubatilisha sheria iliyoweka ukomo wa msimu wa uwindaji kuwa miezi sita na badala yake wanataka wawinde bila ukomo kwa ajili ya kujinufaisha wao wenyewe."

Mwisho akamuonya Nyalandu na kumtaka abatilishe uamuzi wake mara moja huku akisema: "Wafanyabiashara ni wadau muhimu sana, ila ni hatari kuwaruhusu waiburuze wizara kiasi cha kuhatarisha maslahi ya uhifadhi wa wanyamapori."

Mei 13, mwaka huu, wakati anawasilisha hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, Msigwa alianika udhaifu wa Nyalandu huku akimlaumu kwa kukiuka kwa makusudi sheria na taratibu za utumishi wa umma, kutumia vibaya pesa za umma kumwalika Martin Fletcher wa Daily Mail nchini kama njia ya kumhonga n.k.

Msigwa akasema: "Si mara ya kwanza kwa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhoji juu ya usafi wa Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maliasili na Utalii, na mara kadhaa tumeonesha kwa kiasi kikubwa udhaifu wake na kutoa vielelezo mbalimbali vinavyotilia shaka utendaji wake kabla na hata baada ya kukabidhiwa wizara hii nyeti!" Ndugu msomaji, taarifa hizo za Msigwa kwa umma na hotuba yake bungeni, achilia mbali kauli nyingine ambazo si rasmi, zinaonesha mtazamo wa Msigwa kwa Nyalandu katika kipindi cha miezi michache tu iliyopita. Hapa kuna vimelea vya rushwa.

Chanzo: Jamhurimedia.co.tz
 
Msigwa anamvimbisha kichwa Nyalandu badala ya kumpa changamoto,utadhani matatizo yameisha!hailewi kwa nini watu kunafukunyua kila siku,serikali ikiweza hiki unaibua lingine.
 
Binafsi sioni tatizo hapo pengine ni kweli kwa ss msigwa hajaona tatizo,jamani kama katika hicho kipande Nyalandu kafanya vyema Kwanini msigwa asiseme ukweli,au ndio kwa Sababu u mpinzani basi kila kitu upinge?
Msigwa Anajua anachokifanya,ni binadamu Najua na binadamu tuna yetu madhaifu Ila Kwa Hili Najua siku Nyalandu akiteleza Mch.Msigwa Hawezi kumnnyamazia Lazima atafyatuka tu.
 
mkuu uwe unapanga maandishi,hii style kama ya kuchukua maharage na kuyamwaga kwenye gunia lingine inaboa
 
Unaweza kuwa una hoja ...lakini hoja yako ingesimama vizuri kama usingeonesha chuki zako za wazi kwa Msigwa
 
Binafsi sioni tatizo hapo pengine ni kweli kwa ss msigwa hajaona tatizo,jamani kama katika hicho kipande Nyalandu kafanya vyema Kwanini msigwa asiseme ukweli,au ndio kwa Sababu u mpinzani basi kila kitu upinge?
Msigwa Anajua anachokifanya,ni binadamu Najua na binadamu tuna yetu madhaifu Ila Kwa Hili Najua siku Nyalandu akiteleza Mch.Msigwa Hawezi kumnnyamazia Lazima atafyatuka tu.

Ninaogopa sana watu wanaotaka nyekundu iitwe nyeusi au nyeupe iitwe blue. Karidhika na hilo kwa nini asiseme kuwa karidhika?
 
Maneno mengi, ujumbe sifuri.
Jambazi ni jambazi, fisadi ni fisadi, tapeli ni tapeli tu. Madhara ya vitendo vya watu hawa kwa jamii ni yale yale bila kujali kuwa wanatoka
chama tawala au upinzani. Madhara ya vitendo hivi hayaangalii kuwa mtu huyu anajifanya mchungaji, askofu au sheikh.

Hayaangalii kwamba mtu huyu anapenda kuuza sura kwenye runinga kiasi gani. Na wala hayazingatii kuwa mtu huyu anapiga kelele bungeni kiasi gani au anajua matusi kiasi gani.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho chama kikuu cha upinzani nchini. Matarajio yao ni kushika dola, na ndiyo maana siku zote wako mbele kuanika udhaifu na upungufu uliomo ndani ya chama tawala.

Ndiyo maana karata dume inayochezwa na Chadema na vyama vingine vya upinzani sasa hivi ni UFISADI wa ESCROW unaonasibishwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Sina mgogoro na hilo. Ni wajibu wao na kama kweli wana nia ya dhati kututoa hapa tulipo na kutupeleka katika nchi ya asali na maziwa, basi wajitahidi kuhakikisha hili la Escrow na ufisadi mwingine yanafikia mwisho.

Inatosha sana kwa uongozi wa juu wa Chadema kutafakari juu ya hatua waliyochukua wana-Chadema wa Iringa kwa kumuengua Msigwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea uenyekiti wa wilaya. Sababu zilizotolewa kwa kuenguliwa Msigwa ni kujifanya msomi na mjuaji wa kila kitu; mtu aliyejaa dharau na mchache wa kukubali kushauriwa, miongoni mwa sababu nyingine.

Msigwa hajataka kujifunza chochote na bado anajihesabu kuwa na mvuto kwa wananchi wa Iringa! Nitahadharishe kuwa kama Chadema wamelichoka Jimbo la Iringa Mjini, basi wampe Msigwa kijiti.

Kupitia mikutano iliyo rasmi na ile ya vijiweni, upinzani unaonekana kuwa na ajenda nzuri na nia ya dhati kutukwamua kutoka hapa tulipo.

Hata hivyo, upinzani utafanya makosa makubwa kama wataamini kuwa wananchi tunawapima kwa maneno yao matamu tu. Wananchi wanaona vitendo vyao au vya baadhi ya viongozi wa upinzani.

Peter Msigwa (nasita kumwita mchungaji au mheshimiwa), ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Ni mmoja wa viongozi wa Chadema, chama kinachoonekana mbadala wa CCM.

Komredi Freeman Mbowe amempa Msigwa kazi kuhakikisha kuwa anachunga rasilimali zetu zisifujwe na kuharibiwa hovyo. Naamini kwamba Komredi Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hakumtuma Msigwa kwenda kuunda genge la ulaji na mafisadi; kwenda kutetea uhuni unaofanywa na baadhi ya watu na wala kwenda kutafuta utajiri kwa kutumia kofia ya uwaziri kivuli.Hiyo ni dhamana na lazima aitunze na aipe heshima yake.

Naomba nisitafune maneno kwamba kama Chadema kweli inataka kuendelea kuaminika mbele ya Watanzania, basi ingeonesha mfano kwa kuwawajibisha watu ambao wanaonekana kukitia najisi chama kama mchungaji huyu.

Katika kipindi cha runinga ya ITV kinachojulikana kama ‘Dakika 45' Desemba 8,mwaka huu, Msigwa ndiye aliyekuwa mgeni wa kipindi.

Katika maswali aliyoulizwa ni pamoja na baadhi ya kashfa zinazomhusu Lazaro Nyalandu na James Lembeli.

Kwanza, mtangazaji alitaka kujua kulikoni, kwani siku za nyuma Msigwa alikuwa akipigia sana kelele Wizara ya Maliasili na Utalii, lakini siku hizi amekuwa bubu.

Jibu la Msigwa likawa eti Waziri Nyalandu ametumia ‘approach' nzuri tofauti na wenzake ambako anamwalika katika shughuli na hafla mbalimbali na hivyo hana sababu ya kuongea!

Hivi mtu mwenye akili anaweza kutoa jibu la kipuuzi kama hili? Ukweli ni kwamba hii haina tafsiri nyingine zaidi ya ukweli kwamba Msigwa anakiri kuingizwa kwenye ulaji, kwa hiyo hawezi tena kupiga kelele!

Vinginevyo, atuambie kwamba unapofadhiliwa unapata wapi ‘moral authority' ya kumkemea mfadhili wako.

Jibu jingine lililotia kichefuchefu ni utetezi wake juu ya matumizi mabaya ya Leseni ya Rais iliyoruhusu kuuawa wanyamapori zaidi ya 700.

Msigwa anadai kuwa si kweli kwamba eti marafiki hawa wa Nyalandu wameua wanyama 700, bali waliua nyati watano tu na pundamilia wawili.

Akadai kuwa picha za watoto wadogo waliokuwa wanawinda zilizotoka katika gazeti la JAMHURI hazikuwa zao! Huyu mbunge ni wa ajabu kabisa!

Mchungaji gani mwongo namna hii? Ambacho hakusema kuwa hakikuwa cha kweli ni juu ya nakala za vibali na nyaraka zilizokuwa gazetini.

Halafu akawafagilia Wamarekani hawa kuwa ingawa hawakutakiwa kulipa,waliamua kulipa pesa nyingi sana serikalini! Kwa mara nyingine, nashangaa ni vipi mtu anayejiita mchungaji anaweza kuwa mwongo kiasi hiki!

Kwanza, Msigwa ameupotosha umma kwa makusudi kuwa eti JAMHURI iliripoti kuuawa wanyama 700. Hamna aliyeripoti kuwa wanyama 700 wameuawa. Tulichoandika ni juu ya Leseni ya Rais iliyoruhusu kuuawa wanyama 700.

Na ni baada ya JAMHURI kuripoti uhuni huu ndipo Wamarekani hawa walipoamua kutimka na kurudi kwao huku wakiwa wameua nyati watano.

Jibu alilotakiwa kujibu kibaraka huyu wa Nyalandu na Wamarekani ni endapo kulikuwa na uhalali wa kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Friedkin (je, wana sifa hizo?) Leseni nane zilizotolewa ziliruhusu wanafamilia wanane kuwinda wanyama 49 kila mmoja. Kwa hesabu za msomi Msigwa jumla ya wanyama wote itakuwa saba!

Kwa kuwa Msigwa ameamua kuwa kuwadi wa Nyalandu na Wamarekani, basi angetusaidia zaidi kujibu maswali mengine tuliyouliza yakiwamo yale ya uhalali wa Nyalandu kugawa vitalu kinyume cha sheria kwa marafiki zake hawa.

Itakumbukwa kuwa mara tu baada ya kuibuka kashfa hii ya matumizi mabaya ya Leseni ya Rais, tulitabiri kuwa si Msigwa wala Lembeli ambaye angenyanyua mdomo kukemea ufisadi huu. Tuliweka wazi kuwa hili lisingewezekana kutokana na kujengeka kwa mtandao wa ulaji kati ya wawili hawa na Nyalandu.

Uswahiba wa kampuni za Friedkin na Nyalandu na Lembeli unaeleweka. Tuna taarifa juu ya ufadhili wa ndege alizokuwa anapanda Nyalandu kwa shughuli zake binafsi.

Kwa upande wa Lembeli, mfano mmoja ni ile hadidu ya rejea aliyojitengenezea kwenye ripoti ya Operesheni Tokomeza akitaka Mkurugenzi wa Wanyamapori awajibishwe kwa kuwa eti rafiki zake hawa wamekosa kitalu walichokuwa wanakitaka huko Makao WMA!

Ingawa suala hili halikuwa na uhusiano kabisa na ujangili, Lembeli hakuona soni kuliweka kwenye ripoti ili kuwafurahisha Nyalandu na mawakala zake Wamarekani.

Huhitaji akili nyingi kugundua kuwa Msigwa naye ameingizwa kwenye ulaji wa kampuni hizi; na kuingia kwake humo kumekuja kutokana na haja ya kumtumia kufanikisha unyang'anyi wa kitalu cha Green Miles ambacho Nyalandu kawakabidhi Wamarekani bila kufuata sheria za nchi.

Katika hali kama hiyo ambako Msigwa tayari kageuka bidhaa, tunatarajia angethubutu vipi kusema lolote kuhusu uharamia wa Wamarekani hawa kuruhusiwa kuua wanyama wetu 700?

Ujasiri huo atautoa wapi? Ni kwa sababu hiyo hiyo Msigwa aliamua kuufyata ghafla juu ya ile kashfa ya Nyalandu kuamua kurefusha msimu wa uwindaji ili kuwafurahisha Wamarekani hawa waliotaka waruhusiwe kuwinda mwaka mzima.

Awali, Msigwa alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kulaani kitendo kile akikiita ufisadi. Lakini huhitaji akili nyingi sana kugundua kuwa
baada ya kuingizwa kwenye ulaji, hakuwa na ujasiri wa kusema chochote na ndiyo maana hata kwenye hotuba yake ya bajeti aliipotezea.
Atasemaje wakati kusema ina maana kugusa maslahi ya waajiri wake?

Swali juu ya mpango wa Nyalandu na Lembeli kuuza mbuga na hifadhi za Taifa, Msigwa anawatetea maswahiba wake hawa akidai kuwa ni upuuzi mtupu na kwamba eti tulitaka kuuza gazeti tu!Afadhali basi Msigwa angeamua kukaa kimya kuliko kuropoka upuuzi huo.

Lakini kwa kuwa ameamua kuwa kuwadi na msemaji mkuu wa mabwana hawa,basi angejibu maswali ya msingi yaliyojitokeza kwenye makala zetu kadhaa kuhusu kashfa hii.

Atuambie rafiki zake hawa walifuata nini Afrika Kusini hata baada ya kupata ushauri wa kitaalamu juu ya hatari ya African Parks Network
(APN)? Atuambie ilikuwaje Lembeli ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Bodi ya APN (asasi inayotaka kukabidhiwa mbuga zetu) aiwakilishe Serikali kwenye mapatano na asasi hiyo.

Kama akili ya Msigwa haiwezi kuyaona hayo, basi hatuna budi kurejea kuhoji ule utata wa kupata ‘division zero form four' na hatimaye kutunukiwa digrii ya uchungaji!Lakini wakati tunashangaa majibu ya kipuuzi ya Msigwa kwa maswali ya Emmanuel Buhohela wa ITV, kuna haja ya kurejea historia yake kwa ufupi ili tujue kuwa huyu ni mtu wa namna gani.

Peter Msigwa amekuwa akijipambanua kama kiongozi wa dini msomi mwenye digrii (graduate),ingawa wapo wanaohoji uchungaji wake na kutaka kujua kuwa ni chuo kikuu kipi ambacho hupokea wanafunzi waliofeli. ‘Mtumishi huyu wa Mungu na msomi' ndiye Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii.

Alhamisi, Februari 13, mwaka huu, Nyalandu alipomjibu Martin Fletcher kutokana na makala yake kuhusu ujangili kwenye gazeti la Daily Mail,Msigwa alimjia juu huku akimtuhumu kuwa anawabembeleza majangili ambao wanafahamika kwa majina na wapo mitaani wakiendelea na ujangili.

Msigwa alibainisha kuwa mara nyingi Nyalandu amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akidai kuwa mtandao wa ujangili unafahamika na ni mpana unaohusisha watu wenye nguvu za pesa na huku akiwaomba wanaojihusisha na biashara hiyo waachane nayo mara moja.

Akasema kuwa kauli hizo za Nyalandu zinaonesha dhahiri kuwa kuna watu hawaguswi na sheria na wapo juu ya sheria.

Msigwa akasema: "Majibu haya ya Waziri (Nyalandu) yanadhihirisha kuwa mtandao huu unaolalamikiwa na kuogopwa ndiyo unaohusisha Ikulu, wanasiasa, watumishi wa Serikali, maafisa wanyamapori, maafisa usalama, polisi, wanajeshi, pamoja na wafanyabiashara wakubwa, ambao wamekuwa wakijihusisha na Serikali ya CCM."

Akaendelea kumponda Nyalandu kuwa anatumia hisia badala ya vielelezo kujibu hoja. Akatuhumu kuwa Serikali haichukui hatua kwa wahusika ambao wanajulikana kwa majina na wako mitaani wakiendelea na biashara hiyo haramu kwa kuwa wanatafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Machi 23, mwaka huu, Msigwa alitoa taarifa kwa umma iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosema: "Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mazingira ya rushwa na ufisadi katika sekta ya uwindaji nchini." Katika taarifa hiyo, Msigwa alisema: "Ndugu wanahabari, kati ya mambo yanayoashiria mazingira ya rushwa katika sekta ya uwindaji hapa nchini ni kitendo cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, kurefusha, kinyume cha sheria, muda wa msimu wa uwindaji kuanzia tarehe 1 Julai hadi 31 Machi kila mwaka tofauti na muda wa kisheria ambao ni kuanzia tarehe 1 Julai hadi 31 Desemba kila mwaka.

Waziri Nyalandu ametoa agizo la kurefusha msimu wa uwindaji tarehe 19 Machi, 2014 akiwa na wamiliki wa vitalu na makampuni ya uwindaji." Aidha katika taarifa hiyo Msigwa akasema: "Ndugu wanahabari, jambo linaloashiria mazingira ya rushwa zaidi ni kwamba wenye makampuni ya uwindaji wamemmwagia sifa waziri na kusema kuwa ni mtu makini na msikivu.

Jambo hili la wenye makampuni kufurahia uamuzi wa waziri linaonesha japo kwa mazingira kwamba wenye makampuni hao walikuwa wakitafuta kubatilisha sheria iliyoweka ukomo wa msimu wa uwindaji kuwa miezi sita na badala yake wanataka wawinde bila ukomo kwa ajili ya kujinufaisha wao wenyewe."

Mwisho akamuonya Nyalandu na kumtaka abatilishe uamuzi wake mara moja huku akisema: "Wafanyabiashara ni wadau muhimu sana, ila ni hatari kuwaruhusu waiburuze wizara kiasi cha kuhatarisha maslahi ya uhifadhi wa wanyamapori."

Mei 13, mwaka huu, wakati anawasilisha hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, Msigwa alianika udhaifu wa Nyalandu huku akimlaumu kwa kukiuka kwa makusudi sheria na taratibu za utumishi wa umma, kutumia vibaya pesa za umma kumwalika Martin Fletcher wa Daily Mail nchini kama njia ya kumhonga n.k.

Msigwa akasema: "Si mara ya kwanza kwa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhoji juu ya usafi wa Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maliasili na Utalii, na mara kadhaa tumeonesha kwa kiasi kikubwa udhaifu wake na kutoa vielelezo mbalimbali vinavyotilia shaka utendaji wake kabla na hata baada ya kukabidhiwa wizara hii nyeti!" Ndugu msomaji, taarifa hizo za Msigwa kwa umma na hotuba yake bungeni, achilia mbali kauli nyingine ambazo si rasmi, zinaonesha mtazamo wa Msigwa kwa Nyalandu katika kipindi cha miezi michache tu iliyopita. Hapa kuna vimelea vya rushwa.

Chanzo ni Jamhurimedia.co.tz
 
Jamhuri..........Lini mmeanza chuki binafsi na Msigwa?
uandishi umeanza na mambo ya Msigwa asigombee tena Iringa, ...Msigwa alienguliwa kugombea Uwenyekiti wa CHADEMA wilaya Iriga......then unaanza kuhamishia mada yako kwa Nyalandu na Msigwa.

Who will take this Shi.t serious? Waandishi wetu hawa!!
 
Deodatus Balile at work, kaonyesha chuki binafsi kwa Msigwa. Ooh hafai kugombea Iringa, ooh alizungusha shuleni, oooh CDM mchunguzeni...! Haya yote yanatoka wapi? Unapitia mlango wa shutuma za Nyalandu ili kuivuruga CDM?

Inaonekana Gazeti la Balile linatumiwa na mafisadi kutaka kuivuruga CDM ili wamuondoe Msigwa ambaye ni mwiba kwao! CDM hayumbishwi na taarabu za Jamhuri.
 
mtoa mada ulifikiri chadema wapo kwa maslahi ya wananchi wanyonge?

kwa taarifa wapo kwa ajili ya matumbo yao tu walipewa na sabodo kusaidia kwenye majimbo ya visima vya maji hakuna hata kisima cha maji mzee wa watu kanawa mikono
 
Kuna hoja kubwa sana hapa tena ya msingi...hata mimi nimeshangaa sana kwanini msigwa siku hizi yupo kimya sana kuna nini???
 
Mleta mada ana hangover za kupigwa uchaguzi wa serikali za mitaa..... haamini macho yake
 
Ikiwa mpinzani kazi yake ni kupinga kila jambo jema basi siasa za kidemokrasia bado sana kwa afrika!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom