IRINGA: Mbunge Peter Msigwa akamatwa na Polisi baada ya kumaliza mkutano wa hadhara

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
232
260
Mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mch. Peter Msigwa amekamatwa na polisi jimboni Iringa mjini alipokuwa katika mkutano wa hadhara jioni hii.... Sababu za kukamatwa kwake bado hazijajulikana

Tutaendelea kuwaletea kinachoendelea....
=========

========
Vita ya Uchumi ni hii bofya
Listen to Matokeo chanyA+ on TuneIn

=======

"Mchungaji Msigwa amekamatwa na polisi katika mkutano wa hadhara bado anahojiwa, viongozi wamezuiwa kumuona"- Dady Igogo Naibu, Meya Iringa
a7cded25be426da82c3e20484e9d241a.jpg

AACHIWA KWA DHAMANA:

MSIGWA ameachiwa huru kwa dhamana na amedhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Leonce Marto , muda huu saa 4:25 usiku .

Ifahamike kwamba Msigwa ameshushwa jukwaani kwa nguvu akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .

Aidha mikutano ya yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo.

Kesho asubuhi jumatatu Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani .

Hata hivyo Mbunge atazungumza na vyombo vya habari kesho mchana kuweka wazi madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.
 
Mbunge wa Iringa Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mch. Peter Msigwa amekamatwa na polisi jimboni Iringa mjini alipokuwa katika mkutano wa hadhara jioni hii.... Sababu za kukamatwa kwake bado hazijajulikana

Tutaendelea kuwaletea kinachoendelea....
Uchochezi
 
Safi sana na alale Lupango, tangu alivyoidhalilisha nchi yangu kwenye TV za Kenya nimemchukia sana huyu Msigwa!
 
Back
Top Bottom