Msifurahie CHADEMA kupotea

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Na Thadei Ole Mushi

#Ni masikitiko makubwa sana kuwa CHADEMA nayo inataka kupotea kwenye Ramani ya Siasa za Tanzania.

[HASHTAG]#Chadema[/HASHTAG] kwa sasa ipo kwenye wakati mgumu kuliko nyakati zote katika historia yake.

[HASHTAG]#Kila[/HASHTAG] kukicha afadhali ya jana leo kaondoka tena mwenezi wa wilaya ya Hai yaani kila siku ni watu wanaondoka tu.

[HASHTAG]#Sitaki[/HASHTAG] kuzungumzia sababu za wao kutaka kufa ziwe ni za ndan ya chama au njee ya chama ila kama taifa lazma tukisaidie kisipotee kabisa.

[HASHTAG]#Kila[/HASHTAG] baada ya Muongo mmoja lazma cha kimoja kikubwa cha upinzani kife. Zilipita enzi za NCCR zikaja enzi za CUF sasa ni wakati ambao CHADEMA ilikuwa ikimeremeta lakini nacho kinakumbwa na ugonjwa ule ule waliougua wenzake.

[HASHTAG]#Kuna[/HASHTAG] wanaofurahia kufa kwa vyama hivi ila mimi nitakuwa tofauti kidogo na wao. Kufa kwa vyama hivi ni hasara kwetu sisi wananchi.

[HASHTAG]#Niliwahi[/HASHTAG] kusema kuwa hata kipindi cha Nyerere viongozi wetu walikuwa wanatumia mali za umma vibaya. Ila kulikuwa hakuna fursa ya kujua hayo.

[HASHTAG]#Uwepo[/HASHTAG] wa vyama vya upinzani ni kuwanyima viongozi wanaotuongoza kutokufanya makosa, tusifurahie kufa kwake bali tuvijenge viwe taasisi Imara.

#Ni Kweli kuwa Mh. Rais Magufuli kwa sasa anafanya mengi makuu na kujali kodi za wananchi ila tukumbuke kuwa muda wake ukiisha tunaweza kumpata mtu mbovu kabisa. Bila vyama hivi vya upinzani tutarudi kule kule kwenye makashfa makubwa.

[HASHTAG]#Itakuwa[/HASHTAG] ni kujidanganya kabisa kama bado utaamini kuwa CHADEMA ya sasa itaweza kudumu kwenye siasa kwa miaka mingine 2 ijayo. Yaani kufikia 2020 CHADEMA itakwa hoi bin taabani kama hali ya mambo itaendelea kiwa hii ninayoiona.

Ole Mushi.
 
Na Thadei Ole Mushi

#Ni masikitiko makubwa sana kuwa Chadema nayo inataka kupotea kwenye Ramani ya Siasa za Tanzania.

[HASHTAG]#Chadema[/HASHTAG] kwa sasa ipo kwenye wakati mgumu kuliko nyakati zote katika historia yake.

[HASHTAG]#Kila[/HASHTAG] kukicha afadhali ya jana leo kaondoka tena mwenezi wa wilaya ya Hai..... yaani kila siku ni watu wanaondoka tu.

[HASHTAG]#Sitaki[/HASHTAG] kuzungumzia sababu za wao kutaka kufa ziwe ni za ndan ya Chama au njee ya chama ila kama taifa lazma tukisaidie Kisipotee kabisa.

[HASHTAG]#Kila[/HASHTAG] baada ya Muongo mmoja Lazma cha kimoja kikubwa cha Upinzani kife. Zilipita Enzi za NCCR zikaja enzi za CUF sasa ni wakati ambao Chadema ilikuwa ikimeremeta lakini nacho kinakumbwa na ugonjwa ule ule waliougua wenzeke.

[HASHTAG]#Kuna[/HASHTAG] wanaofurahia kufa kwa vyama hivi ila mimi nitakuwa tofauti kidogo na wao. Kufa kwa vyama hivi ni hasara kwetu sisi wananchi.
[HASHTAG]#Niliwahi[/HASHTAG] kusema kuwa hata kipindi cha Nyerere Viongozi wetu walikuwa wanatumia mali za Umma vibaya. Ila kulikuwa hakuna fursa ya kujua hayo....

[HASHTAG]#Uwepo[/HASHTAG] wa Vyama vya Upinzani ni kuwanyima viongozi wanaotuongoza kutokufanya makosa, tusifurahie kufa kwake bali tuvijenge viwe taasisi Imara.

#Ni Kweli kuwa Mh Magufuli kwa sasa anafanya mengi makuu na kujali kodi za wananchi ila tukumbuke kuwa Muda wake ukiisha tunaweza kumpata mtu mbovu kabisa. Bila vyama hivi vya Upinzani tutarudi kule kule kwenye makashfa makubwa.

[HASHTAG]#Itakuwa[/HASHTAG] ni Kujidanganya kabisa kama bado utaamini kuwa Chadema ya Sasa itaweza kudumu kwenye siasa kwa miaka mingine 2 ijayo. Yaani kufikia 2020 Chadema itakwa hoi bin taabani kama hali ya mambo itaendelea kiwa hii ninayoiona.

Ole Mushi.
Chadema ngoja ife, hapa CCM mbele kwa mbele
 
Thats good lets go back to one political party system ndo watanzania wanataka since aliyepo hatotoka Leo wala kesho
 
Kama CCM tu inawanunua itakavyo tukiwapa Nchi si mtanunuliwa na Wazungu? Maana mnapenda kununuliwa
Siyo kila mtu ana sifa ya kununuliwa na ukiangalia mfumo (Pattern) ya "wanaonunuliwa" ni wale ama wenye asili ya kuamini bila ya kuwa kwenye nafasi huwezi kufanya siasa ama wenye tabia za kuamini ukiwa karibu na watawala utafaidika.

Sisi tulio kwenye siasa muda mrefu hakuna ambaye hajawahi kushawishiwa na CCM "kurudi nyumbani" ama kujiunga na "timu ya ushindi" kwa ahadi kemkem. Tatizo ni mtizamo wa mtu binafsi.

Kwa yaliyotokea kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani wengi wenye tabia hizo watajiunga CCM ili "waunge mkono" juhudi za serikali ya awamu ya tano.
 
Chadema hakuna democrasia kwenye uongozi wao wa juu wamejazana watu wa mkoa fulani ambao walidominate TRA kipindi fulani
 
Siyo kila mtu ana sifa ya kununuliwa na ukiangalia mfumo (Pattern) ya "wanaonunuliwa" ni wale ama wenye asili ya kuamini bila ya kuwa kwenye nafasi huwezi kufanya siasa ama wenye tabia za kuamini ukiwa karibu na watawala utafaidika.

Sisi tulio kwenye siasa muda mrefu hakuna ambaye hajawahi kushawishiwa na CCM "kurudi nyumbani" ama kujiunga na "timu ya ushindi" kwa ahadi kemkem. Tatizo ni mtizamo wa mtu binafsi.

Kwa yaliyotokea kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani wengi wenye tabia hizo watajiunga CCM ili "waunge mkono" juhudi za serikali ya awamu ya tano.

Mimi tangu Chadema waliponiambia Katibu Mkuu wao Dkt Slaa kanunuliwa naamini kila Mtu ndani ya Chadema anaweza kunuliwa!

Hata Mbowe mkimuweka mbali na Fuko la Ruzuku la Chama anaweza kurudi CCM
 
Mimi tangu Chadema waliponiambia Katibu Mkuu wao Dkt Slaa kanunuliwa naamini kila Mtu ndani ya Chadema anaweza kunuliwa!
Hata Mbowe mkimuweka mbali na Fuko la Ruzuku la Chama anaweza kurudi CCM
kununuliwa nasema ni tabia. Vyama vya upinzani vinatakiwa viwapate wagombea wao mapema na wawe wametokana na vyama vyao na wajifunze kuwasimamia kila wakati!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Watajua baada ya upinzani kufa na kubakia kuendeshwa jinsi watu wapendavyo ndipo watakugutuka hakuna wa kusemea tena ubaya wowote akiumizwa mwananchi kimya, haki ikiporwa kimya...

Ndipo.kilio na kusaga meno kitakapoanzia.. mwenye akili na aanze kujitafakari..
Kitaibuka chama pinzani chenye nguvu tena
 
Back
Top Bottom