Msidanganywe eti sasa hivi hali ya maisha ughaibuni ni rahisi

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,677
28,991
Mzuka wanajamvi!

Nitasema tu ukweli. Hali ya maisha sasa hivi ughaibuni / ulaya ama mamtoni ni ngumu sana.

Maisha yamekuwa Magumu sana hasa kwaanzia mwezi wa tatu mwaka jana baadaya hii Corona.

Maelfu na Maelfu wamepoteza kazi zao na kujiandikisha kwenye employment benefits.

Kazi za kubeba boksi ni za kugombania. Mfano mzuri tu Denman Norway na Sweden. Nayosema haya ni kweli kwaanzia kufagia kazi za jikoni hotelini usafi na ujenzi yani kuna uhaba. Na ukipata hizo kazi basi sana sana ni mara mbili kwa wiki au tatu tena kwa masaa machache machache.

Kingine usidanganywe eti ni rahisi tu sasa hivi ukapata visa halafu uje huku ukafanikiwa mara moja l.

Sasa kuna ushindani mkubwa kwenye hizi kazi za kubeba boksi kutoka kwa mataifa ya eastern European Polish, Ukrainians, Estonians na wengine. Pia jamii ya kihindi Nepalese, bangladeshi, pakistani na wahindi wanapewa sana kipaumbele hasa kwenye kusafisha meli na huko napo wamepunguzwa wengi safari za meli sasa hivi zimepungua.

Sasa hivi hadi baadhi ya marubani na flight attendants wa SAS Scandinavia airline wanafanya food delivery kusambaza msosi majumbani ndo angalau angalau sasa hivi ndo kazi ya boksi inayolipa.

Ni wale tu wanaofanya kazi kwa wazee ndo hawajaathiriwa na wanaingiza hela ndeefuuu kichiz nawaona mabinti wadogowadogo wanaendesha ndinga za hatarii. Kozi za kutunza wazee nizakugombaniwa kwasababu unakuta wote wenye degrees masters hadi phd za uchumi, biashara computer sayans wanagombania hizi kozi za unesi za kutunza wazee ambazo ziko kwenye level za VETA za huku.

Denmark kuna ile GreenCard yao sasa waliopata wakobmatatani kuderpotiwa kwasababu hawana kazi wamepunguzwa haki za binadamu wanajitahidi kuingilia kati kuwasaidia kwasababu ni janga limesababisha na hali hadi itulie ni mwanzoni 2023. Ila immigration policy ya Denmark siyo rafiki kabisa kwa wahamihaji. Na sasa vyama vyenye mrengo wa far rights ndo zinasomba Scandinavia. Norway ni center right kitatoka, Sweden ni left kitatoka, fina land ni left nacho kitatoka na vyote agenda ni immigeation. Na hivi viko serikalini nao wanakaza hili kuwafurahisha Wananch.

NASEMA UKWELI HAMNA KAZI ZA KUMWAGA ZA KUBEBA BOKSI SASA HIVI ULAYA. NA MSIDANGANYWE ETI UTASAIDIWA KUJA HUKU MAMBO YA KAENDA VIZURI.
 
Toka 2009 sa si ustaafu tu!
Nilistaafu April mwaka jana. Ila napiga sasa part time food delivery na kababy walker changu Toyota yaris. Halafu bibi mabibi wakubwa nao wananitunza. Mmoja majuzi nilimtishia nitajiua kama asiponipa hela nikashtukizia kitu kimeingia kimiani kwenye account yangu nikamuambia asante nitaendelea kuishi.
 
Hata Bongo hakuna kaz Mkuu, degree holder bongo amekua baamed anafungulia walezi pombe salary laki 2 , jua Kali hatari, Bora mamton uta enjoy hata Hali ya hewa, msoto wa bongo ni hatari Bora wa huko mamton.
Hali ya maisha imekuwa ngumu sana kuna sehemu wanatoa msosi wa bure 2019 ukienda hamna watu sasa hivi mstari unaenda hadi zai ya kilomita moja na nusu. Kugawiwa msosi inaanza saa nne asubuhi lakini watu wameshawahi tangu saa moja na watasimama kwa masaa matatu.
 
Kaka bongo nyoso Mara tozo ujakaa sawa msituzalie wtoto kama hamza ,shida tu bongo
 
Kwahiyo unawashauri wenzio waende wapi?

Maana Hadi kwenye vyama sasa hivi wamekaza tigo😂😂
 
Nilistaafu April mwaka jana. Ila napiga sasa part time food delivery na kababy walker changu Toyota yaris. Halafu bibi mabibi wakubwa nao wananitunza. Mmoja majuzi nilimtishia nitajiua kama asiponipa hela nikashtukizia kitu kimeingia kimiani kwenye account yangu nikamuambia asante nitaendelea kuishi.
Hahaa We muyebusi una mabalaa sana
 
Nilistaafu April mwaka jana. Ila napiga sasa part time food delivery na kababy walker changu Toyota yaris. Halafu bibi mabibi wakubwa nao wananitunza. Mmoja majuzi nilimtishia nitajiua kama asiponipa hela nikashtukizia kitu kimeingia kimiani kwenye account yangu nikamuambia asante nitaendelea kuishi.
trick kama hiyo hadi huko inafanya kazi sema mtonyo wake ni kidogo sana
 
Back
Top Bottom