Msichana Witness Obedi aliyefariki na kuzikwa atokea nyumbani kwake na kusimulia mkasa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
IMAG0914.jpg Witness Obedi aliyefariki IMAG0933.jpg Kaburi lake baba.jpg Akiwa na wazazi kisha tukio IMAG0917.JPG Majirani walioomboleza msiba wake wafika kushangaa tuko hilo

Tukio la pekee ambalo linaonekana ni la kishirikina huko Arumeru/Arusha ni pale msichana Witness Obed ambaye inaelezwa alifariki na kuzikwa mara mbili ametokea nyumbani akiwa hai kwa wazazi wake na kisha kusimulia mkasa wa tukio ulivyomtokea. Mkasa huo ulitokea baada ya binti huyo kurudi toka chuo na kufika nyumbani saa mbili jioni akiwa amechelewa ndiyo iliyokuwa sababu ya kugombezwa na familia yake hasa babake mzazi.

Mzazi wake anasema alimgombeza, hivyo binti akatoroka. Binti huyo hakurudi na siku iliyofuata wakatoa tangazo la kumtafuta kupitia vyombo mbalimbali vya habari na sheria. Baadaye walisikia katika kijiji kingine walimwokota msichana aliyefariki. Walipoenda kuuliza waliambiwa alishazikwa.

Wakaenda kuomba kibali polisi cha kufukua kaburi ili kubaini kama ni binti yao, baada ya kupata kibali na kufukua kaburi waliitambua maiti kutokana na alama ambazo aliwa nazo wakati akiwa hai. Wakauchukua mwili huo na kwenda kufanya matanga kwao na kuuzika upya kwenye kaburi jingine.

Baada ya kuondoka alifika kwenye nyumba moja na kumkuta mama mmoja, aliomba maji ya kunywa. Alipewa na alipokuwa anakunywa mama yule alikuwa anamsimamia, lakini alipoonja na kuona machungu alikataa, lakini mama yule alimlazimisha kwa kumnywesha hadi akamaliza kisha akapoteza fahamu na hakujua nini kinaendelea na wapi aliko hakujitambua.

Anasema baadaye hajitambui amefikaje nyumbani, na mama yake alipomwona mara ya kwanza akifika alikimbia kufikiria anaona mzuka. Lakini baadaye alijipiga moyo konde na kumjongea binti yake.

Kuna matukio kadhaa yametokea siku za karibu huko kanda ya Ziwa na kwingineko kwa matuko kama haya, kuna kila dalili ya mchezo wa kishirikia.

Polisi wamesema wanataarifa juu ya tukio hilo na wanalifanyia uchunguzi wa kina.

Source: Global Publishers.
 
I was about to start commenting and then, hapo chini nikaona source. No comment!!

Jaribu kutoka kwenye box, kama uko nje ya box, basi hakikisha kama uko chumbani unafungua pazia mwanga uingie. Polisi wamethibitisha tukio hilo na kwamba wanalifanyia upelelezi, chombo gani ambacho wewe kinaweza kukupa habari unazotaka?

Yesu alipowatokea mitume na wafuasi wake baada ya ufufuko Tomas hakuwepo katika tukio hilo. Aliporudi na kusimuliwa na wenzake kuhusu kutokewa na Yesu Mfufuka alikataa katakata kwamba asipotia kidole chake kwenye makovu ya misumari na kuutia mkono kwenye tobo ubavuni mwake kamwe hawezi kuamini. Yesu akawatokea tena mitume na wafuasi wake Tomas akiwamo chumbani pamoja na wenzake.

Yesu akamwambia,
"Tomas njoo tia kidole chako kwenye matundu ya misumari viganjani mwangu na tia mkono wake kwenye tobo ubavuni mwangu.?
Tomas akasema:
"Bwana wangu na Mungu wangu."
Yesu akamwambia,
"Tomas kwa kuwa umeniona umesadiki, waheri wale wasioona wakaamini!"
 
Huyo hakufariki.

Proof:

aliondoka nyumbani baada ya kugombezwa na hakurudi muda muafaka na sasa amerudi hai na ameandaa sababu ya kumfanya asiadhibiwe na wazazi kwa kosa la kutoroka kwa muda mrefu.

Maiti waliyoifukuwa na kuizika upya haikuwa yake.
Mtu(maiti) aliyezikwa siku nyingi baada yakuokotwa amekufa kwa siku kadhaa unaziona wapi hizo alama alizozaliwa nazo, unaziona kwenye mifupa au? Ngozi inakuwa imeshaharibika.
 
Huyo hakufariki.

Proof:

aliondoka nyumbani baada ya kugombezwa na hakurudi muda muafaka na sasa amerudi hai na ameandaa sababu ya kumfanya asiadhibiwe na wazazi kwa kosa la kutoroka kwa muda mrefu.

Maiti waliyoifukuwa na kuizika upya haikuwa yake.
Mtu(maiti) aliyezikwa siku nyingi baada yakuokotwa amekufa kwa siku kadhaa unaziona wapi hizo alama alizozaliwa nazo, unaziona kwenye mifupa au? Ngozi inakuwa imeshaharibika.

Wazazi walianza kumtafuta siku iliyofuata baada ya kupotea jioni iliyotangulia, na kwa kusoma mazingira inaonekana ndani ya siku hizo mbili maiti iliokotwa na kuzikwa na ni katika siku hizo binti huyo alipotoroka toka nyumbani. Kwamba maiti iliharibika nisingeweza kuamini maana alama alizosema mama yake mzazi asingeweza kuzibaini, ujuavyo sura ya mtoto si rahisi kupotea toka kwa wazazi wake.

Vile vile maiti haiwezi kuharibika vibaya ndani ya siku mbili, kwa kawaida maiti huanza kuharibika ndani na umbile la nje hubaki kama lilivyo kwa siku kadhaa kwa sababu ya kulindwa na ngozi. Sehemu ambazo huanza kuharibika ni zile ambazo zina mashimo ya hewa (pua), mdomo, masikioni na machoni. Dalili za kuanza kuharibika maiti huanza siku ya tatu ambapo harufu huanza kuwa kali ingawa umbile la nje huwa halijaharibika.

Matukio kama hayo si kwa Tanzania tu, nimewahi kushuhudia kwenye vyombo vya habari matukio mawili ya aina hiyo nilipokuwa nchini Marekani, ingawa huko watoto waliopotea na kisha kufika nyumbani wakiwa wamepoteza uwezo wa ufahamu na utambuzi baada ya miaka mitatu au minne hadi walipopelekwa hospitalini kwa matibabu, lakini mazingira ni yayo hayo. Mhusika alishikwa na sijui baadaye kilichoendelea. Mambo haya yapo tusijaribu kutelezesha ukweli.
 
Habari hizi ni za kweli ingawa mwandishi ameongeza chumvi ila tukio limetokea maeneo ya moshono arusha, na baba wa marehemu ni mwinjilisti wa makanisa ya KKKT usharika wa Mara. wakati binti huyu amepotea kulikuwa na mvua kubwa sana zikinyesha mkoani Arusha na binti huyu alikuwa ni mlokole na alipenda sana kwenda kwenye maombi radio safina kwa wale wakazi wa arusha na moshi wanafahamu, kutokana na tatizo lake la kurukwa na akili muda mwingine alitoka safina na kwenda kwa ndugu zake maeneo ya nduruma na wakati akirudi akaendele na safari zake hakufika nyumbani hali ilioinua taharuki kubwa nyumbani kwao. baada ya kutomuona kwa muda wa siku nne wakaamua kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na ndipo walipopata taarifa kuwa kuna maiti maeneo ya nduruma ya msichana imekutwa mtoni na ikiwa imeharibika na wakazi wa huko hawaitambui na hakuna mtu kapotea maeneo hayo, baada ya kusikia hayo familia ya binti huyo iliamua kufunga safari mpaka huko na kukuta wakazi wa nduruma wameshaizika kwenye mfuko wa sulphate(kwa wakazi wa arusha na moshi) na kuoma ifukuliwe na polisi waliwaonyesha picha wakiwa wameitoa maiti hiyo ndani ya maji baba mzazi wa binti huyokutokana na binti yake kutoonekana kwa muda mrefu na taarifa kwamba binti yae alienda nduruma moja kwa moja alisema huyu ni binti yangu ingawaje mama alikataa na kusema binti yangu sio mnene hivi baba akasema kwa sababu imekaaa kwenye maji mda mrefu imevimba. kilichofuatia ni kuifukua maiti na kuiweka kwenye jeneza ikiwa kwenye mfuko wa huo wa sulphate na kwenda kijiji cha moshono kwa mazishi. Habari hizi si za kishirikina ila ni makosa tu yalifanyika na mpaka so watu waache kupotosha.mto nduruma ni mto mkubwa sio mferegi so maiti hiyo huenda imetoka mbali sana coz mpaka sasa hivi hakuna mtu mkoani arusha ameripoti kupotelewa na ndugu na polisi wanaendelea na uchunguzi kwa kuwasiliana na mikoa mingine.kaburi limeng'olewa tu msalaba na kuachwa kama lilivyo mpaka hapo uchunguzi wa polisi utakapo kamilika ila ndugu wa baba wa binti wanasema walisawazishe coz ni mkosi.source ni mimi mwenyewe coz nlikuwa mpaka eneo la tukio.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom