Msichana wa kazi za ndani anahitajika haraka

Anakula bure,kulala bure, nguo ananunuliwa hiyo pesa kwann isimtosh kuna watu wanalipwa laki nne kwa mwezi ila mpak mwisho wa mwezi hana pesa, saa nyie mna dharau pesa eti ndogo
Uko serious anakula bure? Hii ndio kasumba yenyewe, mlipe mshahara ajinunulie chakula, kulala bure? Kwani hawezi kujitafutia makazi yake. Hivi mdogo wako unaweza kukubali afanye hiyo kazi kweli? Hawa watumishi wa majumbani ni muhimu sana tuwalipe vizuri ili waangalie watoto wetu na kizazi kijacho tuache, hii tamaa ya kupenda dezo zaidi. Kama taifa tunatakiwa kusonga mbele na kuwatendea haki Watanzania wenzetu hasa ambao wananyanyaswa kwenye kazi zao. Nafahamu hawa wanafanya kazi zaidi ya masaa 24 ni amri tu, hebu tuwe serious kidogo kwa hawa wafanyakazi wa majumbai. Tukiliwza hilo mengine yote yatakuwa sawa tuwalipe kwa saa za kazi kama watumishi wengine, baada ya hapo ni kazi ya mama/baba.
 
Iv mnajua waajir wengi wa ma house girl..ni ma nurse, walimu na Askari..sa Sijui hayo ma laki watayatoa ya kuwalipa.. Na full Accomadation.. Kula, kulala na mavaz plus matibabu.. Ambayo huwez kata kwenye mshahara wake...
 
ni mshahara mdogo sana huu ila inawezekana pia muajiri ni mlipwa kima cha chini cha serikali, ndiyo maana tunailaumu tucta kwa kushindwa kutetea maslahi ya wanachama wao.
 
Ila kuna mdada namfahamu anafanya kazi balaa.ila ni mkubwa yani binti.aisee hana makuu.Ila kanyanyaswa sehemu mpaka kaamua kurudi kwao
 
Anakula bure,kulala bure, nguo ananunuliwa hiyo pesa kwann isimtosh kuna watu wanalipwa laki nne kwa mwezi ila mpak mwisho wa mwezi hana pesa, saa nyie mna dharau pesa eti ndogo
Upo sawa mkuu. Tena kuna mda mwingine hadi nauli na sadaka za chachi, kuna vitu vingi sana. Kwa mfano binti inabdi umpatie hadi pedi wife akamnunulie. Unaweza ukampa laki kwa mwezi lakini usimjari
 
huo si mshahara jaman hapo ni kuasaidiana tu unamsaidia pa kukaa na kula na kumpa nyongeza ya pesa kidogo na yeye anakusaidia kazi za ndani bas hakuna aloajiriwa hapo jaman maisha ya vijijini ni magumu sana wanatafuta pa kujistir tu
 
Back
Top Bottom