Msichana auwawa kikatili na mumewe Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msichana auwawa kikatili na mumewe Dar

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  MSICHANA Khadija Daudi (22), mkazi wa Mbagala Charambe aliuawa kikatili na mumewe kwa kuchomwa na kisu mgongoni kwa kile kilichodaiwa kuwa ni baada ya kukataa kuamka usiku kwenda kuokota embe.

  Tukio hilo la kusikitisha lilitoka mwishoni mwa wiki huko Mbagala jijini Dar es Salaam.


  Ilidaiwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni mume wa msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Shariff Kondo alimuamsha marehemu kumtaka aende nje ya nyumba yao majira ya saa kumi kasoro usiku, aende akaokote embe lakini marehemu aligoma na kudai kwa kuwa ni usiku asingeweza kwenda nje kufanya kazi hiyo.  Inadaiwa kuwa kutokana na majibu hayo mumewe alikasirika na ndipo alipochukua kisu na kumchoma nacho mgongoni.

  Baada ya kuchomwa kisu hicho alipiga kelele na majirani walijitokeza kumpa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Temeke huku akiwaambia kilichomtokea kwa mumewe huyo.


  Kwa bahati mbaya msichana huyo alipoteza fahamu na kufariki mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo.


  Wakithibitisha tukio hilo baadhi ya majirani wa marehemu huyo, wamedai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada katika chumba cha mpangaji mwenzao na mara baada ya kuingia ndani kwake kujua kilichotokea ndipo walipokuta kitanda chake kimelowa damu na huku akiugulia maumivu.

  Majirani hao wamesema kutokana na hali hiyo walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na baadhi yao walijaribu kumtafuta mumewe lakini hakupatikana ndipo walipokwenda kumwamsha baba mzazi wa msichana huyo anayeishi Charambe na kumuelezea yaliyompata binti yake.


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabasi, amesema kuwa, tayari mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo tayari ameshakamatwa yuko katika kituo cha polisi cha ChanÂ’gombe na anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3556198&&Cat=1
   
 2. kui

  kui JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 6,478
  Likes Received: 5,146
  Trophy Points: 280
  This's screwed up!
   
 3. M

  Matumaini Member

  #3
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Jamani kiswahili kimenichanganya kidogo..! Hivi neno msichana maana yake nini? Ni umri? Ni kuolewa? Au?? Chombo cha habari kinaposema "Msichana auwawa kikatili na mumewe Dar" ni sawa kweli? Haikupaswa kuwa "Mke auwawa na mumewe kikatili.."?
  Naombeni ufahamisho
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  wasichana wote ni wanawake, lakini wanawake wote si wasichana
   
 5. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  hiki kisa kina jambo ndani yake na sio embe tu.. ni mtazamo wangu tu!
   
Loading...