Msichana aliyepooza mwili mzima adaiwa kubakwa Mkoani Mara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Fd02BRQX0AExTp0.jpg
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Juma Ligamba (45), mkazi wa Kijiji cha Kibubwa, Kata ya Butuguri wilayani Butiama mkoani Mara anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni mlemavu aliyepooza mwili mzima tangu kuzaliwa kwake.

Akisimulia kwa masikitiko tukio hilo la kubakwa kwa binti yake mama mzazi wa mtoto huyo anasema binti yake ana ulemavu huo unaomfanya muda wote kulala tu kwani alipooza mwili akiwa na wiki tatu tangu alipozaliwa kwake.

Nae Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Butiama, Devotha Paschal, amesema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wilayani humo huku mwanaasheria kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya ATFGM Masanga Irene Assey, akikemea vikali juu ya vitendo hivyo vya ubakaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibubwa anasema alipata taarifa ya tukio hilo la ubakaji na kushirikiana na familia katika kumkamata mhalifu ambaye yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi kwa sasa na uchunguzi unaendelea.

Naye, Adventina Victor ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya amekiri kumpokea mhanga wa tukio hilo aliyefikishwa hospitalini hapo baada ya tukio hilo la kikatili na kusema kuwa anaendelea na matibabu.

Chanzo: EATV
 
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Juma Ligamba (45), mkazi wa Kijiji cha Kibubwa, Kata ya Butuguri wilayani Butiama mkoani Mara anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni mlemavu aliyepooza mwili mzima tangu kuzaliwa kwake.

Akisimulia kwa masikitiko tukio hilo la kubakwa kwa binti yake mama mzazi wa mtoto huyo anasema binti yake ana ulemavu huo unaomfanya muda wote kulala tuu kwani alipooza mwili akiwa na wiki tatu tangu alipozaliwa kwake.

Nae Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Butiama Devotha Paschal, amesema kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wilayani humo huku mwanaasheria kutoka asasi isiyo ya kiserikali ya ATFGM Masanga Irene Assey, akikemea vikali juu ya vitendo hivyo vya ubakaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibubwa anasema alipata taarifa ya tukio hilo la ubakaji na kushirikiana na familia katika kukamata mhalifu.


Chanzo: EATV
Kamilisha taarifa Yako. Amekamatwa huyo Taahira aliyembaka Mlemavu?
 
Humu duniani kuna watu wana majaribu sana. Kuna muda nakaa pekee yangu na kutafakari kwanini Mungu amenipa mimi afya njema, naweza amka kitandani mwangu na kwenda kazini? Mimi ni nani hadi kunipa uzima? Angalia huyo Binti toka amezaliwa hadi umri huo amelala tu chini? Mungu amtie nguvu huyo binti na wazazi wake ila cha ajabu jamaa linakuja mbaka akiwa amelala chini? Aiseeee, Mungu atusaidie kwa kweli.
 
Dah roho imeniuma mno unajua mtaan kwetu apa kuna msichana kapooza miguu yote,,sasa nnavomuonaga nmerelate na alivobakwa huyo nhee..YAN WENGINE KWA MUNGU HATUNA DHAMBI WALLAH
 
Back
Top Bottom