Msichana ajifungulia chooni katika Hospitali ya Amana

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Msichana wa umri wa miaka 17 ambaye alikuwa katika machungu ya uzazi, amejikuta akijifungulia mtoto chooni baada ya muuguzi mmoja wa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kumtaka aende kuoga na kubadilisha nguo bila ya kujali hali yake.

Msichana huyo, Asha Sudi (17), mkazi wa Tabata Kisiwani, alikutwa na tukio hilo wakati akisubiri kujifungua, na uongozi wa Amana umesema utalishughulikia suala hilo.

Asha alisema alifika hospitalini hapo saa 4:00 asubuhi akiwa anaumwa na uchungu na alipofika mapokezi alikalishwa kwenye benchi.

“Wakati nikiwa nimekaa kwenye benchi alikuja nesi akaniambia niende chooni nikaoge na kubadilisha nguo. Kwa sababu sikujua, nikaenda,” alisema Asha.

Alisema akiwa chooni anajiandaa kuoga, uchungu ulikata ghafla na baada ya dakika chache aliona kitu kinaning’inia sehemu za siri kisha kikadondoka chini.

Baada ya kuona hivyo, alianza kupiga kelele akiita “nesi, nesi” na ndipo alipopita wa kwanza ambaye hata hivyo hakumshughulikia na badala yake akaendelea na kazi zake, lakini baadaye akaenda daktari ambaye hakumtambua kwa jina, akamsaidia.

Nikiwa ninatapatapa sielewi alikuja daktari akamuokota mtoto ambaye alikuwa ameanguka chini karibu na tundu la choo,”alisema.

Baadhi ya wauguzi walitoa ushuhuda wa tukio hilo, wakiwamo daktari aliyemuokoa mama huyo na mwanaye chooni, lakini hawakutaka majina yao yatajwe.

“Nilikuwa wodini. Wakati napita nikasikia mtu anapiga kelele chooni akiita ‘nesi, nesi, mwanangu jamani’. Nilishtuka, ikabidi niende kuona ndipo nikamkuta huyo binti akiwa amesima na kondo likiwa limening’inia na kitoto kichanga kimeanguka chini,” alisema.

Alieleza kuwa alikiokota kichanga hicho na mama yake kisha kuwapa huduma ya kumsafisha mtoto.
Muuguzi mwingine ambaye alikuwa zamu mchana, alisema alipopita kumuangalia mtoto huyo, alikuta akiwa na uvimbe kwenye paji la uso.

“Nikamuuliza mama wa mtoto ndipo akanisimulia. Kwanza nikashangaa huyu nesi ilikuwaje akamruhusu mama ambaye anataka kujifungua kwenda chooni?” alihoji.

Mkuu wa Idara ya Wazazi, Grace Massawe alisema wamelichukua suala hilo na kwamba watalishughulikia, lakini akawataka wazazi na ndugu wa mama huyo kuwa watulivu na kuwasamehe waliofanya tukio hilo.

“Mama tumekuelewa hili suala tutalishughulikia. Aliyefanya kosa hilo tutamuita. Najua alijisahau hasa ukizingatia bado ni mgeni, lakini tutalifanyia kazi,” alisema.

Mkuu wa Idara ya Mama na Mtoto wa hospitali hiyo, Francis Kioweli alisema mtoto huyo hajapata athari ya kiafya na kwamba endapo kutatokea tatizo lolote, basi wazazi hao wasisite kwenda hospitali kwa uangalizi zaidi.
 
miaka 17 !?... hii kesi.

huyo nesi ni kiboko, yaani kaona usafi ndio huduma ya kwanza kwa huyo mama, badala ya kumfanyia vpmo muhimu.
 
mnajua labor iko stage zake! inaweza ikaanza alfajiri mtu akajifungua usiku wa saa mbili, huyu bint wa miaka 17 nadhani ni prime so usually it takes longer ... na haina maana kipindi akiwa na labor basi awe ni mtu wa kulala! akijisikia kukojoa anakwenda ....

anyways tanzania ya magufuli wanasiasa wataanza kukurupuka na fukuzafukuza ... mwisho hizo hospitali mtabaki wenyewe muwatibu hao wagonjwa ... lakini wakumbuke tu hospitali hakuna posho ... utakaa zamu ya masaa 24-48 mshahara mwisho wa mweziiiiiiiiiiii
 
Dah! Ama kweli hapa kazi tu.
Jiandaeni muda is mrefu Waziri was Afya ataibuka hapo.
 
daah, kinachoendelea hapo na ninachokiona ni hao wauguzi wanajaribu kuzunguka zunguka ili kumuokoa mwenzao kibarua kisiote nyasi, na ndo inavotakiwa hata kweny kada zote kulindana ni muhmu ila kiukwel huyo nesi alofanya hvo nadhan anao hata uwez wa kuacha sindano ining'inie takoni ili apokee cm, wauguzi weng ni majipu.
 
Duuuh jamani!
Hawa watoto nao wamezidi kucharuka,miaka 17 ana mtoto?
Maana yake kabeba mimba akiwa na miaka 16!!!!!
Kwa elimu yetu huyu hata form four hajamaliza!
Pole zake,bahati nzuri mtoto hakufa.
 
Asee mkuu najua umesoma kidogo jaribu kupunguza ukali wa maneno please..
sjapenda heading yako
KUJIFUNGURIA CHOONI?
Sawa ndo hali halisi..but imagine ungepost

Dada yangu ajifungulia chooni

Mama yangu ajifungulia chooni

Shangazi yangu ajifungulia chooni

Utaona wazi kuwa ndo baya zaidi asee
Do you think kuna decade nyingne ya kuwaheshimu wamama kama sio hii na zinazofata?
Be intellectual
 
Hii imetokea mwananyamala hospital , mdada kabiwa na nesi akaoge huku akiwa na uchungu.
In short inabidi serikali irudi kwenye vyuo vinavyozalisha manesi.. Kuna walakini katika kile wanachofundishwa.. Huwezi kufundishwa tu jinsi ya kuchoma sindano na kusafisha majipu bila kufundishwa mambo ya customer relationship na watu gani unaoenda kuwahudumia nao huko kazini. Kuna tatizo kubwa sana, sijui wanafundishwa nini huko vyuoni.
Manesi labda wamelazimishwa kufanya hii kazi?
Hapana kuna elimu wanaikosa hapa.
 
Hakuna kitu kigeni hapo kwani ktk labour process inaweza kutokea kitu kinaitwa "exagerated Labour" sasa hivi unapima na kukuta cervix ni CM 4 na baada ya saa moja anakuwa fully dilated, hapo ajabu hakuna mbona hata Yesu alizaliwa kwenye zizi la ng'ombe?
 
Hii imetokea mwananyamala hospital , mdada kabiwa na nesi akaoge huku akiwa na uchungu.
In short inabidi serikali irudi kwenye vyuo vinavyozalisha manesi.. Kuna walakini katika kile wanachofundishwa.. Huwezi kufundishwa tu jinsi ya kuchoma sindano na kusafisha majipu bila kufundishwa mambo ya customer relationship na watu gani unaoenda kuwahudumia nao huko kazini. Kuna tatizo kubwa sana, sijui wanafundishwa nini huko vyuoni.
Manesi labda wamelazimishwa kufanya hii kazi?
Hapana kuna elimu wanaikosa hapa.
Acha kulalama kila kitu mnalalama
 
Hakuna kitu kigeni hapo kwani ktk labour process inaweza kutokea kitu kinaitwa "exagerated Labour" sasa hivi unapima na kukuta cervix ni CM 4 na baada ya saa moja anakuwa fully dilated, hapo ajabu hakuna mbona hata Yesu alizaliwa kwenye zizi la ng'ombe?
mkuu hata mimba yake ilitungwa kwa njia ya ajabu kwa hiyo hata kuzaliwa kwake si jambo la kushangaza.. huwezi fananisha Yesu na na sisi binadamu wenye dhambi
 
Inategemea hapo ilikuwaje mpaka akazaa chooni ni kwasabab ya uzembe au imetokea kikawaida n.k. uchunguzi ufanyike ndo tuanze kuongea. mana baadhi ya manurse wetu nao sio wa kuwatetea, wana tabia za ajabu mno.
 
Back
Top Bottom