Msiba: WoS afiwa na babake

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Waungwana,

Nachukua nafasi hii kuwataarifu msiba mkubwa uliomfika mwenzetu, Woman of substance, wa kufiwa na Baba yake mpendwa. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN na pia awape nguvu, subira na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao. Pole sana kwa msiba mkubwa WOS.
 
WOS,

Pole kwa hayo yaliyo kukuta, mungu akujalie nguvu na faraja wakati huu mgumu kwako na familia yanu kwa kumpoteza mpendwa wenu. Amen
 
Pole sana Woman of Substance , Tunamuomba Mwenyezi Mungu akuzidishie utulivu na ponyo la moyo katika kipindi hiki kigumu AMEN
 
Pole sana WOS na Mungu akupe uvumilivu kwenye hali hii ya huzuni na majonzi. Amini wote njia yetu ni moja hakuna kitakachobakia
 
Ametangulia sisi tupo nyuma tunakuja kwani ndio njia kwenda makazi ya Milele a.k.a kwenye Haki .Pole sana...........tuliumbwa kwa Udongo tutarudi kwa Udongo
 
Dearest WoS

My deepest and most heartfelt sympathy for the family concerning loss of your father. May God give you all comfort and strength

Masa
 
POLE SANA WoS. Mlimpenda Mpendwa wenu lakini Mungu amempenda zaidi. Pumziko la Milele amuangazie nanyi awape amani ya Moyo katika kipindi hiki kigumu sana kwenu.
 
Pole sana Mpendwa wetu kwa kuondokewa na mzazi,Mungu akutie nguvu na uwe na amani moyoni.:(
 
Poleni sana wafiwa na Mola awape nguvu na faraja katika kipindi hiki.

Mleta habari: Msiba uko wapi? inawezekana ni mtu tunamjua (marehemu) in one way or another, tukaenda kuhani msiba..if and when possible.
 
Poleni sana wafiwa na Mola awape nguvu na faraja katika kipindi hiki.

Mleta habari: Msiba uko wapi? inawezekana ni mtu tunamjua (marehemu) in one way or another, tukaenda kuhani msiba..if and when possible.

Pole sana WoS. Mungu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.

Masanja ukiishamjua baba yake itabidi WoS abadili jina hapa jamvini tena, maana WoS itakuwa haina maana tena.
 
Pole sana WOS pamoja na wanafamilia wote. Tunawaombea Mungu awape nguvu za kukabiliana na huu msiba mkubwa wa kumpoteza mpendwa wenu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.
 
Nimpokea taarifa za msiba kwa huzuni na masikitiko makuu .Rambirambi zangu ziwafikie ndugu,jamaa na rafiki wa marehemu popote walipo. Mungu amweke marehemu mahali pema (amin)
 
Pole sana WoS. Mungu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.

Masanja ukiishamjua baba yake itabidi WoS abadili jina hapa kijiji tena, maana WoS itakuwa haina maana tena.

Issue ya anonymity hapa JF inakuwa ngumu kupata habari zaidi maana tungeliweza hata piga simu ama unaweza kukuta ni mtu tunayejua na kufahamiana!
 
Issue ya anonymity hapa JF inakuwa ngumu kupata habari zaidi maana tungeliweza hata piga simu ama unaweza kukuta ni mtu tunayejua na kufahamiana!

Yah ni kweli kabisa, Ila kila mtu anahaki ya kutumia jina analoona linafaa. Sidhani kama ni policy ya JF kuwa na majina fictitious. Ukisubmit jina lako litaonekana lako Mbona kina Dr. Slaa na Zitto wanatumia majina yao halisi?. Nafikri ni kuchagua tu. Ila kwa kuwa haya majina ndiyo tumeyazoea kwa sasa ni kumtakia mzee wa WoS apumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom