Msiba wichita - Kansas

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Jamani,

Nimeiiona hii kwa michuzi na nilidhani labda watanzania wenzetu walioko Kansas ambao wanamfahamu zaidi marehemu wangeiweka hapa. Kwa kweli mimi sijui sana kinachoendelea ila nitajaribu kuwasiliana na watu wa Kansas ili nipate habari za huu msiba.

Poleni sana wafiwa na watanzania wote wa Kansas, ughaibuni na popote pale duniani kwa msiba wa mtanzania mwenzetu aliyekufa kifo cha mateso makubwa sana (moto) kwa mujibu wa hii habari.

Dada Janet kama ukisoma hii thread, Unaweza kutoa habari zaidi za namna ya kusaidia familia ya marehemu na mambo mengine.

Kwa habari zaidi soma hapa toka kwa michuzi
 
Inaonekana kuwa tarehe ya mwisho kutoa michango ilikuwa jana lakini nimepata ujumbe kuwa wale wote wanaojisikia kutoa mchango wanaweza kuwasiliana na watu wa Kansas kwenye hili.

Maelezo kwa niaba ya michuzi..

Watanzania,

Kama ambavyo pengine mmesha sikia, Mtanzania mwenzetu Ulimboka Mwaifuna amefariki dunia hapa Wichita.

Marehemu amefariki kwa ajali ya moto nyumbani kwake Jumapili alfajiri May 11, 2008. Kwa bahati, mke na watoto hawakuwepo nyumbani moto ulipotokea.

Marehemu alizaliwa 1978, na ameacha mke na watoto wawili, miaka 4 na miaka 2.

Zoezi linalofanyika sasa ni kuchanga na kukusanya pesa za kutoha ili tuweze kumsafirisha marehemu kurudi nyumbani Tanzania. Tunataka pia kumsafirisha mke na watoto ili waweze kuhudhuria mazishi.

Kwa kuwa nyumba ya marehemu imeungua, nguo za familia na vifaa ndani ya nyumba vimeteketea. Tunaomba watanzania ambao tunaishi hapa Wichita tuweze kukusanya na kuwasaiadia watoto kwa nguo na vifaa mbalimbali ili angalau tuwapunguzie mzigo huo katika kipindi hiki kigumu.

Account maalum imefunguliwa Bank Of America:
Account Number 518002076799.
Name of Acct ni Lunda Asmani.

Kutokana muda mfupi, hatujaweza bado kusajili Memorial Fund ya marehemu. Kwa wale tuliopo Wichita msiba upo nyumbani kwa

Abel Chamriho, 801 S. Christine.

Tunaomba kila Mtanzania atoe $100.00 (minimum), kabla ya Jumatano May 14, 9pm. Kule Tanzania wameshaanza msiba na macho yote yako kwetu sisi marafiki na ndugu tuliopo Marekani ili tuweza kumfikisha mwenzetu nyumbani Tanzania.

Kila siku kutakuwa na kikao saa tatu usiku ( 9pm) hapo msibani.

Tafadhali tunaomba kila Mtanzania ajiandikishe kwenye daftari la michango.

Nashukuru kwa ushirikiano wako.Map and Directions

801 S Christine St

Wichita,

KS 67218-2635
 
Poleni sana na msiba na imani kuwa muliokuwa karibu ni huyo ndugu yetu aliyefariki mungu atawapa nguvu na uwezo ili muweze kuusafirisha mwili wa marehemu
 
Rap
Ully Mwanga Wa Mille Akuangazie Na Raha Ya Milele Akupe Ee Bwana Upumzike Kwa Amani
Amen....tunakusubiri Dar Kwa Majonzi Br
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom