Msiba wa sharo: Wema afunika mastaa wenzake

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

Wema-Sepetu-Akipozi.jpg
Wema Sepetu
Msanii nyota wa filamu nchini na aliyekuwa MissTanzania 2006/07 Wema Isack Sepetu katikati ya wiki iliyopita alilitia aibu kundi la bongo muvi kwa kufanya kitu cha kipekee kwenye msiba wa mwanamuziki na msanii wa komedi aliyefariki kwa ajali Mkoani Tanga Sharo Milionea.

Wema Sepetu ambaye siku za hivi karibuni amepumzika skendo kwenye vyombo vya habari alipongezwa na watu kwa uungwana aliounonyesha baada ya kutoa mchango mwingi kuliko msanii yeyote wa kundi hilo linalosifika kwa kashfa za ngono.

Habari zilizothibitishwa na mmoja wa ndugu wa marehemu ambae aligoma kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji wa familia alisema kuwa "Ni kweli wasanii mbalimbali walijitolea kwa kuja huku Tanga lakini Wema ndiye aliyetoa mchango mkubwa sana kwa kutoa shilingi laki mbili peke yake 200,000/= huku wasanii wengine wakiishia kutia aibu” Alisema mtu.

Aidha ilidaiwa Wema ndiye aliyeonekana kuwa na uchungu wa dhati toka moyoni ambapo licha ya mchango huo pia alionekana kujishughulisha na kazi za kusaidia majukumu msibani hapo bila kujali ustaa wake aliokuwa nao

 
Kama ni kweli SAFI SANA WEMA SEPETU... Sababu Wasanii Wengine tuliwaona kwenye PICHA wamekaa kwenye ZULIA wakicheka kama VILE hakuna kilio...
 
Wema, wema, wema!
Hivi hakuzimia? Manake she is a crying proffesional drama queen.
 
Ni ngumu wakati mwingine kupima kuguswa na kifo in relation na amount ya hela aliyotoa mtu, kuna ambao huwa wameguswa sana ila hawana cha kutoa na kuna ambao wanacho ila hawapendi kuonekana though wanajitolea sana. Na kuna wengine wanatumia misiba kama sehemu ya kujionesha. But all in all pongezi kwa mdada kwa kujitoa kwa moyo wote katika msiba wa Sharo
 

...pia alionekana kujishughulisha na kazi za kusaidia majukumu msibani hapo ..
Kwa hili anastahili pongezi (hata kama pengine ilikuwa ni namna nyingine ya kutafuta attention!). Wengi wetu tunajisahau sana tunpoenda msibani, badala ya kusaidia wafiwa mara nyingi tunakuwa mzigo kwao kwa kusubiri watuhudumie.
 
Ni jambo jema kama mtu anaamua kujitolea kwa nguvu zake kusaidia kufanikisha kumsitiri mwenzake anapokutwa na mauti maana matatizo tumeumbiwa binadamu,inawezekana kati ya waliochanga hakukuwa na aliyechanga pesa nyingi na hawakuwa wakitegemea kama Wema angeweza kuchangia pesa hizo ambazo kwao waliona ni kiwango kikubwa sana kulinganisha na wasanii wengine ambao walienda na hawakutoa hata senti na kuishia kwenye grocery na bar kunywa eti wanapunguza maumivu ya kufiwa na rafiki yao.
Kila mtu na mapungufu yake na kuna upande mwingine mtu huwa na mazuri yake,kwenye mapungufu tuna haki ya kusema na kwenye mazuri tupongeze,hongera Wema kwa kuonesha unajali maana wapo wenzako ambao wana uwezo kama wako wameshindwa kufanya kama wewe.
 


...
Msanii nyota wa filamu nchini na aliyekuwa MissTanzania 2006/07 Wema Isack Sepetu katikati ya wiki iliyopita alilitia aibu kundi la bongo muvi kwa kufanya kitu cha kipekee kwenye ...
... Wema ndiye aliyetoa mchango mkubwa sana kwa kutoa shilingi laki mbili peke yake 200,000/= ...

Hivi mi ndio sikuelewa au taarifa haijilewi. Sasa hapo ametiaje aibu, amelitia vipi kundi hili aibu! Au ndo zile za habari nzuri haiuzi hivyo kichwa cha habari lazima kiwe ambiguity.
 
Hongera WEMA. Hivi ni kwa nini hata kwa hili jema hamtoi pongezi? Tumeshazoea kusoma skendo za WEMA na ina maana tunapendelea kusikia Skendo tu!!!?? Akifanya jema tumpongeze pia!!
 
Misiba siku hizi ni sehemu za show na kushindana nani katoa zaidi?
 
Mi huwa najishangalia sana haya mambo, nchi yangu ya tanzania nakupendajeeeeee????
 
Mambo ya kutoa rambirambi na kujitangaza yametokea wapi, utu uko wapi jamani? TUSISIFIE UJINGA JAMANI KHAA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom