Msiba wa Regia Mtema umedhihirisha kuwa siasa siyo ugomvi wala chuki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msiba wa Regia Mtema umedhihirisha kuwa siasa siyo ugomvi wala chuki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Jan 17, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  View attachment 45554

  Ushiriki wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na Viongozi na wanachama wa chama hicho katika msiba wa marehemu Rejia Mtema umethibitisha kwamba siasa si ugomvi wala chuzi.

  Nimehudhuria kuagwa kwa mara ya mwisho mwili wa marehemu Rejia Mtema katika viwanja vya Karimjee na kuwaona wana CCM na wana CDM kwa pamoja wakiomboleza kwa kupeana pole na kukumbatiana. Kwa hakika hakukuwa na kuitana MAGWANDA wala MAGAMBA.... wote walikuwa ni wamoja hata wale wa vyama vingine vikiwemo CUF, NCCR - Mageuzi, TLP, UDP na vingine.

  Hata Spika wa Bunge Mama Anne Makinda alithibitisha kuwa " Kelele zinazopigwa na watu wa vyama vya siasa ni ngonjela tu, mwisho wa siku wao ni kitu kimoja kwa utanzania wao"

  My take: Ushirikiano ulioonekana udumu si katika mambo ya misiba tu bali na mengineyo ya kujenga nchi likiwemo la katiba mpya tunaloliendea na mengineyo kwa ustawi wa Taifa.
   
 2. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 6,955
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli ushirikiano huu katika msiba wa dada yetu Regia kama ungelikua wanashirikiana katika kutafuta maslahi ya taifa hili hakika tungekua tuko mbali sana.
   
 3. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,662
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  KWELI ila sasa magamba wanadhani siasa ni vita!1
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,905
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Yeah, you have a point dude! We need to take this as a challenge!
   
 5. Ngatele

  Ngatele JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kweli ni jambo linalopendeza sana, dada yetu Regia ametuweka pamoja. Watanzania kwa kweli tunapendana, katika mchakato wa katiba tupange mambo yetu vizuri ili baadaye chama chochote kishinde kwa haki na tushikane mikono kwa kubadilishana madaraka kwa amani, kwa kufanya hivyo tutaendelea kuwa kisiwa cha amani.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  CCM na CUF wanatakiwa wajifunze kutokana na msiba huu
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,236
  Likes Received: 1,552
  Trophy Points: 280
  Umoja na upendo ni asili yetu isipokuwa hii tabia ya kujenga tabaka kubwa la wenye nacho na wasionacho ndio litaondoa hii asili yetu. Usije shangaa hata MS, FF, REJAO pia walikuwapo pale!
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,292
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  magamba hawaaminiki bana wapo kwenye show tu
   
 9. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 12,941
  Likes Received: 547
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 10. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umenena mwanaJF haya manyang'au ya ccm ni manafiki tu hamna kitu; wachawi wao ndiyo wamemtengenezea ajali ya kutengeneza! Kwa ccm kuua ni jadi, ama kwa sumu au kishirikina maana hata mkuu wao analindwa na nguvu za kishirikina, ndiyo maana kwenye msiba huu wanajitokeza kwa wingi ili kufunika uchuro wao. Huyu mama ameuawa kwa ajali ya kutengenezwa kishrikina na wachawi wa ccm. Hii ndiyo tabia moja ya wachawi ili wasidhaniwe kuwa ndiyo wauaji. Mbona kura zake walimnyang'anya kwa nuvu ya UWT???????? Sasa huu unafuku wote ni wa nini?????? Ndiyo tabia ya wauaji ilivyo!!!!!!!!!!
   
 11. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Acha mawazo mgando wewe. Huezi kuwa great thinker na mawazo ya kwenye vijiwe vya kahawa kama haya.
  Halafu hufanani hata na jina lako.
  Shame upon you.
   
Loading...