Msiba wa Mkapa: CHADEMA mnakwama wapi? Tuwasaidie vipi?

Cheki hii ng'ombe tena. pale ni msibani au ni sehemu ya siasa!??

mkishibaga ugali maharage mnakuaga na ujinga mwingi sana
 
We lofa umeombwa msaada gani chadema?Mbona watu waliendelea kuingia hata baada ya hiyo saa tano? CHADEMA walikuwa na mapokezi ya mpendwa wao siku ya jumatatu.Hivyo siku muafaka ilikuwa jumanne.

Hakuna kilichoharibika hata usipo aga maiti!
Malofa katika ubora wenu, yaani mumpokee kiwete wenu, mlewe mapombe mpaka alfajiri, muamke na hang over mkale supu kwa Chichi halafu mpandishe mabendera yenu, mjiweke wa mwisho kama nyie ni zaidi ya mhe Rais, halafu mje uwanjani late mnanuka farujohn, halafu nani awaruhusuni walevi nyie??
 
Ni kawaida kwa chadema kutumia misiba kutafuta Kiki,waliuburuza mitaani mwili wa mawazo mpaka ndugu wakaupora
 
Malofa katika ubora wenu, yaani mumpokee kiwete wenu, mlewe mapombe mpaka alfajiri, muamke na hang over mkale supu kwa Chichi halafu mpandishe mabendera yenu, mjiweke wa mwisho kama nyie ni zaidi ya mhe Rais, halafu mje uwanjani late mnanuka farujohn, halafu nani awaruhusuni walevi nyie??
Mkapa (marehemu) alikuwa mlevi kuliko babu yako.
Kuwa tu mvumilivu
 
Na Mwamba wa Kaskazini

Kwanza nianze kwa kusema nitamshangaa Kiongozi au Afisa yeyote wa Serikali eti atakayepoteza muda wake kuwajibu Chadema kwa nini leo walizuiwa kuingia Uwanjani wakidai walikwenda kuaga mwili wa Mzee Mkapa huku wakiwa wamechelewa na hata kukiuka maagizo ya jinsi ya kuingia uwanjani.

Nasema nitashangaa kweli kweli yani, kwa sababu wapumbavu huwa hawapaswi kumshughulisha mtu. Ukimjibu mpumbavu nawe utakuwa mpumbavu zaidi ya mpumbavu.

Yani kitakuwa kisa cha yule chizi aliyekwapua nguo za jamaa aliyekuwa anaoga mtoni kisha jamaa badala ya kuchutama atafute namna ya kujisitiri, naye akaunga tela kumkimbiza chizi. Hapo chizi ni yupi!

Jana, tarehe 27, Julai, 2020, ikiwa ni siku moja kabla ya tukio la Mzee Mkapa kuagwa Kitaifa, wasemaji wawili waandamizi wa Serikali walitoa ufafanuzi tena wakiwa MBASHARA kwenye vyombo vya habari kuhusu utaratibu mpya wa kuaga mwili wa Mzee Mkapa leo.

Katika shughuli kama hizi ni kawaida taratibu kubadilika kwa sababu mbalimbali na kwa kweli Serikali ilitimiza vyema wajibu wake kila siku wananchi kujulishwa taratibu mpya zilizopaswa kufuatwa.

Sasa kwa kuwa Chadema washafeli, tuwasaidie kuwapa majibu ya mtihani walioupaparikia na kutosoma maelekezo machache tu au kuwa wasikivu na kuzidi kuharibikiwa zaidi!

Jana Jumapili Majira ya saa 10 hivi jioni Msemaji Mkuu wa Serikali alisikika live akieleza utaratibu wa kuaga leo kuwa viongozi wote (akawataja majina ya makundi ya wazito tu kuanzia mawaziri, mabalozi, makatibu wakuu, wabunge na akaendelea mpaka nikasikia kundi la wawakilishi na viongozi wa vyama vya siasa).

Akasema kundi hili utaratibu wake ni kwenda kuacha magari yao pale Karimjee na kisha watabebwa na magari maalum hadi Uwanjani na muda uliotolewa kufika kuacha magari na kuondoka kwa mabasi ulikuwa ni kuanzia saa 12 na nusu mpaka saa moja na nusu asubuhi.

Mawaziri wakatii, wabunge wakatii, wakuu wa mikoa wakatii, mabalozi wa jumuiya wakatii, viongozi wengine wa vyama vya siasa wakatii, Chadema tu wakasubiri karibia saa nne hivi wakaondoka na magari yao mstari mreeefu kwenda moja kwa moja Uwanjani ili wakazuiwe ili walie kusaka kiki. Sasa hii imebuma kama ya jana ya mapokezi ya Lissu!

Jana tena saa 11 jioni Waziri Mkuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Kitaifa akaongea mbashara na kusisitiza kuwa leo ilikuwa siku ya viongozi wakuu wa nchi na wawakilishi kutoka nje kuaga. Hivyo pia ni muhimu kuwauliza Chadema walikuwa wanakuja kufanya nini leo badala ya jana siku iliyokuwa maalum ya wao kuaga?

Nasisitiza tena utaratibu uliotolewa juzi ni kwamba jana viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu na hata viongozi wengne kama wa dini, siasa na mawaziri walipata fursa ya kuaga mwili wa Mzee Mkapa. Na walifanya hivyo kwa adabu na utulivu!

Sasa leo Chadema vipi? Jana hamkwenda, leo mnachelewa! Mnataka nini? Yani tuwasaidie vipi?

Yani Wananchi wote juzi na jana waelewe maelekezo na kuyatii hadi wale wauza mikate, wauza maji, wauza karanga, machingwa na wanafunzi wameelewa maelekezo na kwa siku zote tatu wametoa salaam zao na kuaga then nyie tu iwe nongwa.

Brothers and Sisters jitazameni, sio tu mnaboa, bali sasa muendako mnachosha!
Unatumia mbinu za Mwiguru ili urudishiwe mkoa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom