Msiba wa George Kahama wamkumbusha Mhariri wa Raia Mwema, Abdulwahid Sykes

Yani Mzee unavoshupalia coincidence ya Uislam kuweko kwenye historia ya Tanganyika ni sawa na Urusi kujisifia kua wao ni walevi wazuri.

Sasa harakati zimefanyika mostly Pwani unategemea waislam wasiwemo?Hiyo ni kawaida sana.Waislam wao kila kuchwa ni kulia dhulma tu!..

Kwa mfano hizo harakati zingefanyikia Tukuyu halafu wanyakyusa waanze kujisifia.Coincidence tu!
Bukoba...
Nitakuuliza swali kwa nini Tukuyu wakawa nyuma katika kudai
uhuru?
 
Sheikh Mohamed Said
Tanu walifanya khiana kubadilisha historia ya uhuru wa Tanganyika....hili labda kumfurahisha Mwalimu aliependa kutukuzwa na pia ile hali ya kutokuwa na uhuru wa kujieleza na kwa kiasi fulani Mwalimu alikua na chembe chembe za udikteta uchwara kwa kutumia msamiati wa Tundu Lissu. Hivyo watu wake wakaribu woote wakiogopa na always walikua wao ni kutengeneza mapambio ya kumsifu. Na yeye mwenyewe akipenda hayo mpaka akaridhia vitabu vya Tanu kuandika upotofu.
Kosa la pili ni baada ya Tanu na Asp kuuangana 1977 . Pale ilikuwa ni nafasi ya mwanzo kabisa ambayo tuliopoteza katika kuweka kumbukumbu za historia yetu. Yale majengo ya Tanu na Asp yangeachwa kuwa museum na humo kuwekwa kumbu kumbu zote za vyama hivyo..tunge hifadhi nyaraka muhimu humo..na haya ya Akina Sykes na Nyerere tungeyahifadhi...lumumba na kisiwa ndui ingekuwa ni makumbusho ya historia ya kugombea uhuru...na ccm wangeanza upya.
Tatu tulipoteza nafasi ya kuweka sawa hii historia pale tulipo anzisha vyama vingi...ile sheria ingelazimisha mali zote za Ilokuwa Tanu na Asp kuwa mali za Umma na kugeuzwa makumbusho ya Taifa.
Ccm wasinge ruhusiwa kuhodhi mali na nyaraka za historia...hizi ni za watanzania wote...lakini hatu kufikiria hilo na Mwalimu alikuwepo nae hakulifikiria hilo na akawachia ccm kuhodhi mali na nyaraka muhimu za uhuru.
Hasara yake ni hii ccm wako bussy kujaribu ku survive wasishindwe uchaguzi hivyo hawana habari na mambo ya historia.
Hasara yake upinzani nao hawana habari ya Tanu na Asp kwani wanadhani hayo ni ya Mahasimu wao Ccm.
Hii ni hasara kwa Taifa
Hivyo kuna makusudi ya kupotosha na kuna makosa kama nchi tumeyafanya katika jambo hili...ni vyema vitabu vyako sasa ukajitolea viwepo bure online kama mchango wako kwa taifa na vijana. Ni wachache sana watanunua vitabu kwa sasa na vijana wengi ni watu wa digitally hivyo kuruhusu kuviachia online utasaidia vijana kujua historia yao ya ukweli
Ahsante
 
Historia ya Mzee Kahama zaidi alikua na uhusiano mzuri na Vatican na ndie alikua kiungo wa Mwalimu na kanisa. Mara kadhaa mwalimu alimtumia kupeleka ujumbe au kupata ushauri huko.
Mkapa nae pia alimtumia kama. Mzee wa kanisa kumwakilisha vatican.
Haijulikani connection gani alikua nazo Kahama na vatican lakini uhusiano huu ndio ulio simika mizizi ya kanisa kuikamata serikali kama Sivalon alivo elezea. Cheo cha "Sir" pia kilitokana na kazi zake za kanisa nchini Tanzania na allitunukiwa na pope John XXIII
Alimwakilisha mwalimu huko vatican kwenye second ecumenical council 1962-65
Alimwakilisha mkapa katika maziko ya pope John II
Hivyo alikua mtu wa kanisa zaidi..
 
Bopwe,
Publisher hawezi kukubali kukiweka kitabu chake kipatikane bure.

Hata hivyo kitabu cha Abdul Sykes kinauzika sana sasa tunakwenda toleo la nne Kiswahili na la tatu Kiingereza.
 
Sina hila wala uongo maishani mwangu, na siwezi msingizia mtu chochote, ndivyo nilivyolelewa, sina haja sana ya kukulazimisha, kama huamini ni sawa tu
Kituko unachekesha sana. Dk. Kyaruzi mie ndiye niliyemfufua na kuandika historia yake. Nitakuwekea jinsi nilivyomwandika ili wasomaji watuhukumu.
 
Kituko,
Hilo la kuwa Tanganyika ilipewa uhuru baada ya WWII ndiyo
leo nalisikia kwako.

Nimesoma kila kitabu kilichoandikwa kuhusu ukoloni Tanganyika.

Zaidi nimesoma hadi shajara za Kleist Sykes na nyaraka za
watoto wake sijakuta popote hilo limeandikwa.

Nimemsoma Martin Kayamba, ''The Autobiography of
Martin Kayamba...'' hakuna kitu kama hicho.

Nimewasoma Erika Fiah mhariri wa Kwetu na Ramadhani
Mashado Plantan
mahriri wa Zuhra hakuna kitu kama hicho...

Unataka iandikwe hivyo?, Je Tanganyika lilikuwa Koloni la Uingereza?, waingereza walikuwa na kazi gani hapa Tanganyika?
 
Chachu...
Siwezi kushangaa ikiwa hamumtambui Ali Migeyo.

Hakutambuliwa Abdul Sykes mwenye kadi ya TANU No. 3
Hakutambuliwa Ally Sykes mwenye kadi ya TANU No. 2 na
kadi ya TANU No. 1 ya Mwalimu Nyerere ni Ally Sykes
ndiye aliyeiandika.

Hajatambuliwa baba yao Mzee Kleist aliyejenga hiyo ofisi
ilipozaliwa TANU 1954.

Hajatambuliwa Iddi Faizi Mafungo aliyesimamia safari ya
Nyerere UNO 1955.

Kipi mimi leo kitanishangaza ikiwa hamumtambui Suedi
Kagasheki?

Ama kuhusu Uislam naam ulitumika sana katika kupambana
na ukoloni kuanzia Vita ya Maji Maji dhidi ya Wajerumani hadi
kudai uhuru kutoka kwa Waingereza.

Ilikuwa Salum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjale ndiyo vijana
waliomleta Mwalimu Nyerere Jimbo wa Kusini kuja kupambana
na Kanisa lililokuwa linawatisha wananchi kujiunga na TANU kudai
uhuru.

Wala katika kuandika historia hii hakuna udini ni historia tu tupu
iliyokuwapo hatuwezi kuifuta hata kama kuna baadhi yetu kwa
sababu zetu binafsi hatuipendi.

Kipi kitanishangaza ikiwa wewe leo hii humjui Sheikh Yusuf Badi,
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir
waliokuwa
mstari wa mbele kupigania uhuru wa Tanganyika?

Ikiwa wewe una historia nyingine isiyokuwa hii tuwekee hapa Majlis
tuisome.
Mzee Mohamed Said, kwanza namshukuru Mungu kwakuwa bado uko hai pamoja na kushudia mambo mengi ya zamani ambayo wengi wetu humu tunabaki kuwa wasikilizaji lakini wewe uliyaona na unayakumbuka.

Lakini pia umejitahidi kuandika mara nyingi haya mambo ya historia ya nchi yetu; wakati wa ukoloni, kutafuta mpaka kupata uhuru, mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania.

Kwa haraka haraka nimeona kama vitu vingi unavifahamu kwa undani.

Niombe: uandike kitabu kinachoelezea hivyo vitu vyote ili tulio wengi tuisome historia sahihi ya Tanzania badala ya kuishia kusoma vitabu vya shule vilivyohaririwa kadri ya matakwa ya watawala waliopo.

Nimesoma comments za wenzangu hapo juu zikielezea kuwa unakuwa upande wa dini moja, hilo siyo tatizo maana ukweli unabaki kuwa ukweli, pengine hii itatupa changamoto ya kwenda kuwahoji wazee wetu waliopo katika maeneo unayowataja ili tujiridhishe na pengine kuongezea uliowasahau. Mimi ni mkrisito lakini elimu haijui dini hivyo sioni tatizo.

Najua kinaweza kikapata ugumu kusajiliwa hicho kitabu tukipata hata "raw" tutaelewa. Hii itapaki kuwa elimu kwa vizazi vingi.

Kama kitabu kipo tayari nitaomba ueleze hapa ili nijue namna ya kukipata.
 
Mwanyasi nimeandika kitabu The Life and Times of Abdulwahid Sykes kipo na cha Kiswahili kinapatikana Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema na Mtoro Dar es Salaam bei elfu 10000.00.
 
Uko sahihi kabisa

Hujajibu swali, au ndiyo njia yako ya kukwepa maswali?

Alama Mohamed Said kaandika historia ambayo mpaka leo hii hakuna wa kuipinga.

Kama unapenda isome kama hupendi isome halafu tuletee historia yako tuuone ukweli wako.

Mmekazana humu porojo ndeefu na kuponda kisichopondeka.

Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.

Umesoma kuhusu Mshume Kiyate?
 
Yani Mzee unavoshupalia coincidence ya Uislam kuweko kwenye historia ya Tanganyika ni sawa na Urusi kujisifia kua wao ni walevi wazuri.

Sasa harakati zimefanyika mostly Pwani unategemea waislam wasiwemo?Hiyo ni kawaida sana.Waislam wao kila kuchwa ni kulia dhulma tu!..

Kwa mfano hizo harakati zingefanyikia Tukuyu halafu wanyakyusa waanze kujisifia.Coincidence tu!

Na hii nayo ni Pwani:

"Hapo Makao Makuu ya CCM Dodoma ziwekwe picha za Omar Suleiman, Haruna Taratibu, Edward Mwangosi, Tanga zikwekwe picha za Abdallah Rashid Sembe, Bi. Mwanamwema, Hamisi Heri. Lindi picha za Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Yusuf Badi. Kilimanjaro waweke picha za Eikaeli Mbowe, Yusuf Olotu, Juma Ngoma, Mama Biti Maalim, Halima Selengia." - Mohamed Said.
 
Unataka iandikwe hivyo?, Je Tanganyika lilikuwa Koloni la Uingereza?, waingereza walikuwa na kazi gani hapa Tanganyika?
Kituko Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini lakini ili uhuru upatikane ilikuwa lazima tuidhihirishie UNO kuwa tuko tayari na tunaweza kujitawala. Waingereza hawakuwa wanalitaka hili walitaka wabakie kututawala. Turning point ya hili ilikuwa 1950 Abdul Sykes na Hamzah Mwapachu walipofanya mapinduzi na kuchukua uongozi wa TAA kwa nguvu. Nia ikiwa kudai nchi. Mwalimu Thomas Plantan aliyekuwa rais wa TAA wakati ule alikuwa hafanyi lolote la maana kudai nchi. Waingereza wakaingia kati na kudai akina Abdul waache fujo uitishwe uchaguzi. Katika mkutano wa pande mbili wa waliopinduliwa na waliopindua pale Arnautoglo Schneider Plantan aliwakabili Waingereza na kudai lazima uitishwe uchaguzi na yeye ndiye aliyesaidia kuwatia Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi katika uongozi wa TAA. Hapo ndipo harakati za mawasiliano na UNO zikaanza kwa msaada mkubwa wa Earle Seaton. Waingereza wakahujumu uongozi huu...Vituko umeuliza kazi ya Waingereza Tanganyika...hiyo ndiyo ilikuwa kazi yao kuikalia Tanganyika. Baya zaidi ni kuwa Kanisa nalo likawa linawatisha wafuasi wake ati wachukue tahadhari na Waislamu wanataka kuleta vita vingine kama walivyoleta na Wajerumani kupitia Maji Maji. Ilipokuja Kamati ya UNO kukagua Tanganyika 1954 Said Chamwenyewe ndiye aliongoza ujumbe wa watu wa Tanganyika kuzungumza na ujumbe ule. Huyu Mzee Chamwenyewe ndiye aliyeipa TANU wanachama wake wa kwanza kutoka Rufiji wengi wao wakiwa murid wa Tariqa Qadiriyya ambao Khalifa wao alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir. Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa katika TAA Political Subcommitte pamoja Abdul, Mwapachu na wazalendo wengine kama Steven Mhando. Hii ndiyo historia ya TANU...inachoma nyoyo lakini tufanyeje tuifute kuwafurahisha wale ambao walikaa pembeni wakati wazee wetu wanapigania uhuru wa Tanganyika?
 
Mwanyasi nimeandika kitabu The Life and Times of Abdulwahid Sykes kipo na cha Kiswahili kinapatikana Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Manyema na Mtoro Dar es Salaam bei elfu 10000.00.
Ahsante, inamaana katika kitabu hicho zimo taarifa zote kama nilivoshauri? Au ni hiyo tu ya Abdulwahid Sykes? Kama zote zimo sawa, na kama ni vinginevyo, huoni kuna umuhimu wa kuandika kipana zaidi.

Hicho kilichopo nitakifuata hapo,ahsante.
 
Mwanyasi yapo mengi ni kitabu cha zaidi ya kurasa 350.
 
Bukoba...
Nitakuuliza swali kwa nini Tukuyu wakawa nyuma katika kudai
uhuru?
Hakukua na uamsho sababu ilikua ""kijijini" ukilinganisha na Dar ambako ndio Uingereza alifanya makao yake ya utawala..Au unataka niseme sababu hawakua na Uislam mwingi kama watu wa Pwani?Mzee bwana si useme tu unaeneza Udini kupitia hiyo Historia yako yaishe! Na hakuna hata siku moja watu wameuinua Ukristo wa Nyerere na kuuunganisha na harakati alizokua anafanya.
 
Hujajibu swali, au ndiyo njia yako ya kukwepa maswali?

Alama Mohamed Said kaandika historia ambayo mpaka leo hii hakuna wa kuipinga.

Kama unapenda isome kama hupendi isome halafu tuletee historia yako tuuone ukweli wako.

Mmekazana humu porojo ndeefu na kuponda kisichopondeka.

Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.

Umesoma kuhusu Mshume Kiyate?

Asante kwa kunielewa una kichwa kizuri sana
 
Hakukua na uamsho sababu ilikua ""kijijini" ukilinganisha na Dar ambako ndio Uingereza alifanya makao yake ya utawala..Au unataka niseme sababu hawakua na Uislam mwingi kama watu wa Pwani?Mzee bwana si useme tu unaeneza Udini kupitia hiyo Historia yako yaishe! Na hakuna hata siku moja watu wameuinua Ukristo wa Nyerere na kuuunganisha na harakati alizokua anafanya.
Bukoba...
Vipi unaichukulia historia hii mimi siwezi kukuingilia kila mtu
ana uwezo wa kukamata uelewa wake.

Kubwa ni kuwa nimefanya masahihidsho makubwa sana ya
historia ya TANU.
 
Kituko Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini lakini ili uhuru upatikane ilikuwa lazima tuidhihirishie UNO kuwa tuko tayari na tunaweza kujitawala. Waingereza hawakuwa wanalitaka hili walitaka wabakie kututawala. Turning point ya hili ilikuwa 1950 Abdul Sykes na Hamzah Mwapachu walipofanya mapinduzi na kuchukua uongozi wa TAA kwa nguvu. Nia ikiwa kudai nchi. Mwalimu Thomas Plantan aliyekuwa rais wa TAA wakati ule alikuwa hafanyi lolote la maana kudai nchi. Waingereza wakaingia kati na kudai akina Abdul waache fujo uitishwe uchaguzi. Katika mkutano wa pande mbili wa waliopinduliwa na waliopindua pale Arnautoglo Schneider Plantan aliwakabili Waingereza na kudai lazima uitishwe uchaguzi na yeye ndiye aliyesaidia kuwatia Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi katika uongozi wa TAA. Hapo ndipo harakati za mawasiliano na UNO zikaanza kwa msaada mkubwa wa Earle Seaton. Waingereza wakahujumu uongozi huu...Vituko umeuliza kazi ya Waingereza Tanganyika...hiyo ndiyo ilikuwa kazi yao kuikalia Tanganyika. Baya zaidi ni kuwa Kanisa nalo likawa linawatisha wafuasi wake ati wachukue tahadhari na Waislamu wanataka kuleta vita vingine kama walivyoleta na Wajerumani kupitia Maji Maji. Ilipokuja Kamati ya UNO kukagua Tanganyika 1954 Said Chamwenyewe ndiye aliongoza ujumbe wa watu wa Tanganyika kuzungumza na ujumbe ule. Huyu Mzee Chamwenyewe ndiye aliyeipa TANU wanachama wake wa kwanza kutoka Rufiji wengi wao wakiwa murid wa Tariqa Qadiriyya ambao Khalifa wao alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir. Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa katika TAA Political Subcommitte pamoja Abdul, Mwapachu na wazalendo wengine kama Steven Mhando. Hii ndiyo historia ya TANU...inachoma nyoyo lakini tufanyeje tuifute kuwafurahisha wale ambao walikaa pembeni wakati wazee wetu wanapigania uhuru wa Tanganyika?

Nini Maana ya kuwa chini ya udhamini?
Je Tanganyika ilikuwa Koloni la Uingereza?,
Je wakti ule Wajerumani wameshindwa vita na kunyanganywa Makoloni yao, sisi (Tanganyika) tungekuwa tayari tungepewa uhuru?

Hope hukunielewa nilipokwambia Tanganyika tulishakuwa huru mara baada tu ya Mjerumani kishindwa vita
 
Back
Top Bottom