BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
excuse me Bubu ataka kusema!
kwa nini watz walioishi nje ya nchi wasiendeshe magari wakirudi Tz?nataka kujua tu naona ufahamu wangu ni mdogo sana
Kuna baadhi ambao wamejifunza kuendesha wakiwa kwenye nchi za magharibi ambazo sheria za barabara zinafuatwa sana ukilinganisha na Tanzania. Hivyo kama hujawahi kuendesha Tanzania ambako sheria za barabara hazifuatwi kabisa basi ni rahisi kupata ajali.
Pia nimeshawasikia Watanzania wengi wanaoishi nje ambao walikuwa wanaendesha Tanzania kabla ya kwenda nje kwamba wakiwa Tanzania wanaogopa sana kuendesha hata kama wakiachiwa gari na ndugu, jamaa au rafiki au hata kama wana magari yao bongo. Weekend njema.