MSIBA:Peter Gachuma,Thomson Msigwa WAFARIKI DUNIA

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
825
http://haki-hakingowi.blogspot.com/


MSIBA MKUBWA UINGEREZA
(Reading)
*Peter Gachuma,Thomson Msigwa
Wafariki Dunia..
-------------
Wanajumuiya wa UK tumepokea habari Ya kusikitisha za kifo cha Wenzetu Peter Gachuma na Thomson Msigwa kilichotokea leo huko Tanzania kwa ajali ya gari wakitokea Tarime (mara) kuelekea Mwanza.
Marehemu Peter Gashuma alikua akisoma university of Birmingham na kuishi Reading,vilevile Marehemu Thomson Msigwa alikua anaishi Reading Uingereza, Marehemu walikwenda nyumbani (Tanzania) wiki iliyopita kwa likizo fupi.Marehemu Thomson Msigwa ameacha mke na watoto.
*Mwenyezi mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali pema peponi Amen.
----
**Tutaendelea kuwajulisha habari zaidi kadri zinavyotufikia..
 
Poleni sana wafiwa.....naomba Mungu awape nguvu katika wakati huu mgumu wa majonzi.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
Amina.
 
Watanzania mnaoishi nje mkienda Tanzania msiendeshe magari tafuteni madereva wa Tanzania.

Kuendesha Tanzania na kuendesha ukiwa nje ni vitu viwili tofauti kama usiku na mchana. Mungu awalaze mahali pema peponi~Amen.
 
Mwenyezi Mungu awape pumziko la amani, sote tunaelekea katika njia hiyo
 
Poleni sana ndugu, jamaa, marafiki
pamoja na wote mlioguswa na misiba hii. Inasikitisha sana kupoteza vijana wenye nguvu.
Tuombeani katika safari hii.
 
GT, huyu Gachuma ana undugu na yule mfanyabiashara wa Mara/Mwanza?

Poleni wafiwa, mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
 
Habari hzi nilizipata jana usiku,Peter Gachuma ni mtoto wa Mwita Gachuma yule Mjumbe NEC wa Chama Cha Mapinduzi na mfanyabiashara maarufu wa mikoa ya Mwanza na Mara.

Ajali ilitokea karibia na eneo ya igoma mjini mwanza,katikati ya igoma na kisesa,kwa habari nilizopewa ni kwamba waligonga Gari aina ya Fuso ambayo ilikuwa imesimama,ni hivyo kupata ajali mbaya sana sababu walikuwa katika mwendo mkali sana

Kwa niaba ya wana CCM wote na Watanzania Wote wa Hapa JF naomba kutoa salaam Za rambirambi kwa Mhe. Gachuma,

Leo ilikuwa Mhe. Gachuma aende India kwenda kufungua Rasmi Tawi la CCM lizindukliwa wiki ilioyopita na Nape Mnauye.
 
Namwomba Mwenyezi Mungu Azilaze Pahali Pema Peponi Roho Za Marehemu. Pia Napenda Kuwapa Pole Ndugu Wote Na Marafiki.

SteveD.
 
Watanzania mnaoishi nje mkienda Tanzania msiendeshe magari tafuteni madereva wa Tanzania.

Kuendesha Tanzania na kuendesha ukiwa nje ni vitu viwili tofauti kama usiku na mchana. Mungu awalaze mahali pema peponi~Amen.

excuse me Bubu ataka kusema!
kwa nini watz walioishi nje ya nchi wasiendeshe magari wakirudi Tz?nataka kujua tu naona ufahamu wangu ni mdogo sana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom