MSIBA: Nimefiwa na Mama yangu mzazi

Ndugu zangu wana Jamvi nawajulisha kifo cha mama yangu mzazi kilichotokea usiku huu hapa Dar es salaam . Msiba uko Kawe opposite viwanja vya Tanganyika Parkers nyuma ya MSONGE PUB .Taratibu na mipango ya Mazishi zinafanyika Kawe na Marehemu atasafirshwa kwenda Musoma kwa Mazishi taratibu zikikamilika .Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Pole sana, musoma Sehem gani? Ili tulioko musoma tuje kukupa pole.
 
Mkuu tunaomba update uzi kwa kuweka mawasiliano tunajua maiti inaenda mbali sana hvo kuweka mawasiliano tunaweza kujipiga piga walau Tukusaidie kidogo, Pole sana ndugu yetu
 
Ndugu zangu wana Jamvi nawajulisha kifo cha mama yangu mzazi kilichotokea usiku huu hapa Dar es salaam . Msiba uko Kawe opposite viwanja vya Tanganyika Parkers nyuma ya MSONGE PUB .Taratibu na mipango ya Mazishi zinafanyika Kawe na Marehemu atasafirshwa kwenda Musoma kwa Mazishi taratibu zikikamilika .Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
poleni sana na msiba
 
Nini maana ya LAIKI ktk taarifa ya msiba kama hii? Nimeona bandiko limepewa LAIKI 4.
 
Pole sana mkuu. Safari yetu ni moja, yeye ametangulia sisi tutafuata. Tumuombee. R. I. P
 
Pole sana mwa JF na Mungu ampe pumziko LA amani Mama yetu mpendwa.

Tupo pamoja na wana familia,ndugu,jamaa na marafiki ktk kipindiki hiki kigumu cha msiba.

Mungu awape wepesi na moyo wa uvumilivu wana familia wote.
 
Back
Top Bottom