Msiba mzito wa mama yetu, mwalimu wetu mpendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msiba mzito wa mama yetu, mwalimu wetu mpendwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Original Pastor, Jun 18, 2009.

 1. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Msiba mzito wa mama yetu, mwalimu wetu mpendwa mama yetu na mwalimu wetu mpendwa Frida Mtunguja ambaye alikuwa anafundisha shule ya msingi chumbageni tanga amefariki jana tarehe 16/06/2009 saa 22:46:12 katika hospitali ya bombo baada ya kuugua maradhi ya homa ya manjano.

  Msiba utakuwepo nyumbani kwake kisosora tanga na mipango ya mazishi inafanywa na ndugu na jamaa.

  Kwa wale wanaoguswa kwa njia moja au nyingine hasa wanafunzi wa chumbageni ambapo marehemu alikuwa anawafundisha tunawapa pole sana. Kuhusu michango yenu inaweza kutufikia hapa nyumbani au hapo shule ya msingi chumbageni tanga.

  Ukiwa kama ndugu, rafiki au jirani unaombwa kufika katika msiba huu wa mama yetu /mwalimu wetu mpendwa.

  Kwa mawasiliano ya kutuma michango yako piga namba hii +255717062827 ni mwanae anaitwa mMichael Kuziwa (huyu alisoma Galanos Sekondari alimaliza mwaka 1999 form IV)
   
 2. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Poleni sana, ni kazi ya Mungu.
   
Loading...