Msiba: Mwakyembe afiwa na mama yake

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
Mheshimiwa na shujaa wetu, Hon Dr. Harrison Mwakyembe amefiwa na mpendwa Mama yake mzazi, kwa mujibu wa mtangazo ya vifo ya Radio Free Afrika monitored here in Mbeya this morning

Mpendwa marehemu mama huyu atazikwa huko Kyela siku ya Jumatano

POLE SANA DR. MWAKYEMBE, MUNGU AKUTIE NGUVU!
 
duh.. nilizungumza na Dr. juzi (alhamisi) kabla hajaenda Zambia, na alikuwa anamuangalia mama yake pale hospitali na nilimpa pole ya kuuguza kwa niaba ya marafiki zake wengi na kumwombea mama uponyi. Hivyo nimezipokea habari hizi kwa mshtuko mkubwa na majonzi. Namtakia wakati huu faraja kubwa yeye na familia nzima, saa na wakati huu wa huzuni.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.
 
RIP Bibi yetu ukapumzike kwa amani...tupo tunapambana na Baba yetu Mwakyembe...ukamuombee sana nasi tunamuombea.
 
Pole sana Dr Mwakyembe pamoja na familia yako Ndugu na jamaa

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
 
Pole sana kwa Mhe na familia, ndugu jamaa na marafiki. Upumzike kwa amani Bibi!!
 
Pole sana Mh Mwakyembe kwa msiba huu mzito,, tunakuombea uweze kupita salama katika kipindi hiki kigumu!! Mungu amlaze mahali pema Amin
 
Mheshimiwa mbunge na Shujaa wa taifa, Brother Mwakyembe pole sana na Mungu akupe nguvu sana, ndugu zako katika ukombozi wa taifa tunaipokea hii habari ya msiba wa Mama yako kwa roho nzito sana na huzuni kubwa sana.

- Taifa linakuhitaji sasa kuliko wakati wowote toka tupate uhuru, tunakuombe a kwa Mungu akubariki na uweze kukipita kipindi hiki cha majaribio bila kutetereka, na tuko pamoja na wewe brother katika majonzi na hata kwa hali na mali ikibidi tutawasiliana na wewe on this.

Mungu akubariki wewe na familia yako, na pia amuweke pema peponi marehemu mama yako.

FMES!
 
Dr Mwakyembe na Family,
Poleni sana kwa msiba huu mkubwa. Ni wetu sote. Kifo hakina mwenyewe na huja kwa wakati uliopangwa na mwenyewe bila sisi kuchagua. Tunachoweza ni kuwa karibu yako na familia yako kwa wakati huu mgumu. Mwenyezi awatie nguvu na faraja.
 
Pole Mh Mwakyembe, kipindi kigumu hiki kwako tupo pamoja katika sala marehemu apumzike kwa amani

Masa
 
MWENYEZI MUNGU Mwingi wa rehema awatie nguvu wewe,familia yako ,na watu wote wenye mapenzi mema walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine!!!

BWANA ALITOA ,BWANA AMETWAA ,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!!!!

AMEN!!!
 
- Nimeongea na Dr. dakika chache zilizopita, kila kitu kiko under control na msafara wa kuelekea Mbeya kwa mazishi utakuwa ni kesho mchana saa saba, na mazishi yatafanyika huko siku ya Jumanne.

- Pia tumemfikishia ujumbe wa majonzi ya wana-JF, na Again Mungu amuweke mahali pema peponi marehemu.

FMES!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom