Msiba kwa wafugaji wa kuku wa mayai -- Mayai yamefurika bei chini toka Mombasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msiba kwa wafugaji wa kuku wa mayai -- Mayai yamefurika bei chini toka Mombasa!

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by FUSO, Feb 13, 2012.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Update:

  Hali ya soko imerudi kama kawaida yake, yale mayai yaliyokuwa yanauzwa kwa mafungu (4000 - 4500) kwa tray yemeisha. Tray kwa sasa ni 6500 hadi 7,000 kwa bei ya Jumla.

  Serikali msiruhusu tena wahuni wahuni kuingiza mizigo ya vyakula kwa njia za panya!! lindeni wazalishaji wazawa wa ndani - maana mmeshatuambia kuwekeza kwenye GESI HATUWEZI - sasa huku kwenye mifugo nako mnataka kutukimbiza, swali je tuende wapi?

  Hili si la kubeza, ni suala muhimu kabisa - LAZIMA KUWAJALI WAKULIMA NA WAFUGAJI WA NDANI.  ---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

  Wakuu nawapa pole sana wafugaji wa kuku wa mayai, mji mzima mayai yamefurika, hayana soko na wafugaji wanahaha huko na huko kutafuta soko la kuyauza. Katika upelelezi wangu kuna habari ambazo hazijathibitika kwamba mayai yanatoka mombasa kwa volume ya ajabu kabisa, mayai haya ndiyo yanakuja kuua soko la ndani na kutangaza msiba kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao wengi ni wamama wajane na vijana walitoka vyuo ambao wanajaribu kujiajiri wenyewe.

  Ninachojiuliza:
  Je Wizara ya kilimo na ufugaji inalijua hili? na inachukua hatua gani kuwalinda wazalishaji wadogo wadogo wa ndani?
  Je hawa wafanyabiashra wanaoingiza mayai nchi wanalipa kodo sitahiki?
  na je gharama zao za uzalishaji ni gharama zipi huko mombasa maana tray moja wanauza mpaka shs 4500 hadi 5000 bei ambayo kwa mfugaji wa nchini haimlipi. Mfugaji wa ndani anatakiwa auze tray si chini ya sh 6500 ili aweze kusonga mbele.

  Mwisho kama hizi habari ni za kweli basi wajasiriamali wadogo wadogo huu ni msiba kwenu, kama hamtaungana na kulepeka malalamiko yenu wizarani basi mmekwisha. nawashauri mfungue chama chenu kiwatetee.

  Hebu tujadili hili kwa kina maana tusipokuwa makini hwa wakenya watatuua njaa kwani wao wana mitaji mikubwa sana hasa kwenye suala zima la ufugaji na wanaweza ku-supply Maziwa, Mayai, Nyama za kusindika, Ngozi kwa volume ya ajabu.

  Tuamke watanzania hasa wafugaji hali ni mbaya.
   
 2. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  wewe u aweza pia saidia kuleta habari zaidi toka ulikosikia ili iwasaidie wafugaji wa nchini.
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280

  Mkuu mimi sioni Tatizo kwa mayai kutoka Mombasa, mbona hizi supermarket zinaagiza kutoka south Africa?

  Niliwahi kutoa wazo moja humu, lakini watu wengi walilipinga sana na mimi binafisi sioni ubaya wa mayai kutoka Mombasa kuja Dar, kwani kuna aliye jaribu kupeleka Mombasa akashindwa?

  Jiulize yafuatayo.

  1. Wao wanafanyaje hadi wauze bei ya chini huku Tz?

  2. Kwa nini ya wabongo yauzwe bei ya juu?

  Hapa na bado mkuu, hili ndo soko huria na kinacho takiwa ni kuamka na kupambana na si kulila lia kwamba serikali iwasaidie, mimi sioni cha serikali kusaidia hapa na hata hao wa mombasa ukijaribu kuwafuatilia utagundua kwamba serikali yao haijawasaidia chochote zaidi ya wao wenyewe kupambana kufa na kupona

  Na kwenye red hapo.

  1. Kwani watanzania tunashindwa nini?

  2. Hatuwezi zalisha maziwa?

  3. Hatuwezi zalisha kuku?

  4. Je ni aridhi haitoshi?

  5. Una uhakika wakenya wanamitaji mikubwa sana ndo maana wanauza Tanzania?

  6. Mbona hao wote wanao uza Tanzania wengi wao ni wafanya biashara wa kati?
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Sio kwamba wana mitaji mikubwa bali wanatumia mtindo wa "pamoja tunaweza".
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa tulishachagua mfumo wa soko huria nadhani ni suala jema tu, hasa kwa walaji. Supply ikiwa kubwa bei itashuka. Lakini nitoe wito kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa, kuwa waangalifu na hivi vyakula vinavyoingia nchini.
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Asavali yashuke bei nasi tupate vitamin bana,kufa kufaana
   
 7. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  huo utafiti wako unaonyesha mayai yameingia kwa kasi katika miji gani Tanzania?
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nani kawadanganya serikali hasa wizara husika iko makini kiivyo kugundua vitu kama hivyo? Ukisikia serikali ni legelege we jua ni pamoja na wizara zote. Watoto wa mjini hapa wanasema tumepigwa bao
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  ni hapa Dar es salaam, pia Zanzibar, Mtwara kote yamejaa!!

  Ninachojua mimi soko la kitu chochote likifurika Dar basi ujue Tanzania kote kumejaa. kweli wakuu hali mbaya maana mtu akiwa na kuku 400 anatoa average tray 10 mpaka 12 kwa siku -- hawa kuku wanakula mfuko mmoja kwa Tshs 34,500. sasa ukipiga hesabu faida kwa 5000 inakuwa 16,400 hapo bado vitamins, mshahara wa mfanyakazi, maji na umeme. Shughuli pevu kwa wafugaji.
   
 10. p

  panadol JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mm ni mfugaji ni kweli biashara ya mayai imekuwa ngumu mayai yamekuwa mengi sana mitaani inasemekana yanatoka nje tunaomba serikali mtusaidie katika hili vinginevyo hali itakuwa mbaya kwa sisi wafugaji kumbukeni tumekopa mikopo tunahitaji kurudisha vinginevyo tutakufa kimitaji na kuanza kulaumu serikali,waziri w kilimo na ufugaji tusaidie,wapiganaji January makamba,Nape,Olesemndeka,Anna kilango na wengineo tusaidieni jamani tunahanamia!
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Niko kinyume kabisa na mtazamo wako. Biashara za wabongo wanajipangia na kupandisha bei bila utaratibu na matokeo yake wateja ndio wanaoumia na hawana chaguo lingine.

  Hao wa Mombasa waongeze kasi ya ushindani ili bei zipungue, wengi tunalalamika bei kupanda kila leo ni sababu ya kutoendesha biashara kiushindani kuwavutia wateja, ila tunashindana kupandisha bei, kila mmoja anang'ang'ania kupandisha tu bila kumjali mtumiaji wa bidhaa zao.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kulalamika hakutatusaidia, kutokana na wingi huo wa mayai tunatakiwa tuwe wabunifu wa kunaza nufikiria hayo mayai tuyafanyeje ili biashara iendelee. Si kwamba mayai lazima yaliwe yalivyo, inawezakana kufungua viwanda vidogo vya usindikaji wa vyakula .

  Sisi wabongo moja au jirani akianza mradi fulani basi marafiki, majirani na hata wateja wakishaona mwenzao anaanza kukinga kidogo nao wanaenda kuanzisha mradi wa aina hiyo hiyo. Tujaribu kubuni miradi katika nyanja nyingine.

  Hiyo siyo hoja ya mimi binafsi kuniridhia, hapo ndipo unapoweza kufahamu mbinu ya kupunguza gharama za uendeshaji mradi ni wewe mwenyewe kuchapa kazi zaidi kuliko ubwana wa kutegemea mwajiriwa akufanyie.
   
 13. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mtumieni message Mwamtumu Bakari Mahiza atoe ushauri mwingine, maana kuna wengine walifuata ushauri wake wa mwanzo!
   
 14. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  yaani unataka serikali iwabane ili bei ipande halafu maisha yaendelee kuwa magumu? we ni mchawi, kama biashara imekushinda tafuta biashara ingine, tunataka kila kitu kiuzwe kwa bei ya chini, kama mmeshindwa kuwa wabunifu ili kupunguza garama za uzalishaji ili watz wafaidike waacheni wenzenu waendelee.
   
 15. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  sidhani kama serikali inaweza kutoa suluhisho kwa hili. Hapa kuna ujumbe tunapewa wafugaji wadogo. Aidha tuongeze mitaji kwa kuanzisha firms zenye uwezo wa ku supply kwa wingi zaidi (economy of scale) au kuvumbua mbinu mpya zinazoweza kupunguza gharama za uzalishaji. Tujifunze kuendesha miradi kwa mbinu au strategy za kibiashara na siyo kutegemea serikali kuingilia kila wakati.
   
 16. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wakati 'wenzetu' wanawekeza kwenye shughuli za uzalishaji mali, sie bado tupo kwenye ishu za uchaguzi uliokwishapita, katiba, migomo, maandamano...
   
 17. F

  FUSO JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  kaka kuindoa serikali kwa jambo hili ni sawa na wewe mzazi kumwandaa mtoto wako kwa kumsomesha shule za kata ukitegemea ataingia kwenye soko la ajira. Narudia tena hakuna serikali yoyote duniani isiyowajali wazalishaji wadogo wadogo wa ndani, kama ipo basi ni hii yetu tu.

  kwa kutumia tafsiri mbaya ya dhana nzima ya soko huria, ndiyo sasa unaona Tanzania inaingiza nchini hata vijiti vya meno wakati tuna miti kibao, mayai, nyanya, bilinganya, mchicha, kunde, maharage, maziwa,ngozi, jamani hata kuni eti zinauzwa supermaket, maajabu ya Musa haya.

  Ni ndoto kujenga uchumi kama unadharau vitu vidogo vidogo kama hivi kuzaliswa kwa soko la ndani ya nchi yako, Serikali kupitia wizara na idara zake inashindwa kuwanyenyua watu hawa wazalishe kwa ubora?

  Bila udhbiti wa vitu hivi vidogo vidogo kutengenezwa au kuzalishwa nchini, sasa tunakuwa watumwa ndani ya nchi yetu. (Taifa la wachuuzi)
   
 18. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  leo asubuhi nimesikia kuna mayai ya kichina maarufu kwa jina la "mayai ya plastic" huko china sasa TFDA chondechonde mayai haya yasiingie Tanzania kwani hupunguza nguvu za kiume. kwao huko wanafanya hivyo kwa lengo la kupunguza kuzaliana sisi bado tunahitaji kuendelea kuijaza nchi hii kwani bado kuna mapoli mengi unutilized
   
 19. HP1

  HP1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 3,353
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Watakaoumia sio wafugaji pekee. Ukiangalia suala la supply and demand utaona kuwa yakiingia kwa wingi sana mahitataji yatapungua hivyo wakenya watapunguza kuingiza na tutafikia kwenye equilibrium. Lakini pili wafugaji wa ndani wakipunguza uzalishaji itawaathiri wenye makampuni ya kutotolesha, wauzaji madawa, wauzaji vyakula vya kuku na wadau wote wa namna hiyo. Wito kwa wafugaji ni kutafuta mbinu mbadala kwa ajili ya ushindani wa biashara hii katika huu utandawazi.
   
 20. yatima

  yatima JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama mayai yao ni ya KUKU WA KIENJYEJI - kweli wanaweza ua soko - SIKU HIZI WATU WENGI TUNAPENDA MAYAI YA KUKU WA KIENYEJI - INGAWAJE NI MADOGO SANA - SIJUI KWELI NI YA KUKU AU KUNGURU????

  wafugaji waki-Tanzania wajipange iUUZAJI WA MAYAI WA KUKU WA KIENYEJI - yana ubora zaidi - MWUULIZENE DAKTARI WA JF kama nimekosea!!
   
Loading...