Msiba Chicago

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Familia ya Dr. Eustace L. Kaijage wa Olympia Fields, Illinois, USA, inasikitika kutangaza kifo cha Bwana Elias D.Muganda, kilichotokea Chicago, Illinois, USA, tarehe 29 Oktoba 2008.
Jumuiya ya watanzania wa Chicago na Marekani kwa ujumla mnaombwa mchango wa kugharamia na kufanikisha mazishi ya ndugu yetu na Mtanzania mwenzetu, Elias D. Muganda.

Memorial service na mazishi vitafanyika Jumamosi, tarehe 8, Novemba, 2008.
Mahali pa Memorial service ni,
Leak and Sons Funeral Chapels,
18400 S. Pulaski Rd.,
Country Club Hills,
IL 60478.
Ratiba ni kama ifuatavyo:
Saa nne asubuhi mpaka saa sita mchana, visitation ikifuatiwa na Memorial Service Kuhusu mahali na saa za mazishi mutajulishwa baadaye.

Account maalum ya michango ya hayati Elias D. Muganda, imefunguliwa.
Bank Name: JPMorgan Chase Bank, N.A.
Bank Address: Chicago, Illinois 60670
Account Name: Eustace L. Kaijage
Bank Routing Number: 071000013
Account Number: 800871980

Kwa habari zaidi wasiliana na,
Eustace L. Kaijage
708-767-4841

Mungu aiweke roho ya marehemu Elias mahali pema,mbinguni.

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ELIAS D. MUGANDA
Marehemu Elias D. Muganda alizaliwa mwaka 1937, Novemba, tarehe 9, Bukoba, Tanzania. Alisoma Shule ya Msingi ya Kashozi Middle School na kujiunga na masomo ya sekondari katika shule ya St. Francis College Pugu ambapo alisoma tangu kidato cha kwanza hadi cha sita (Form VI).

Baada ya kumaliza elimu ya secondary kidato cha sita Decemba 1961 marehemu alichaguliwa kufanya kazi na East African Common Services/East African Community. Mwanzoni mwa 1962 alipata scholarship ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu, Marekani.

Alisomea University of New York, Buffalo, USA na kufuzu shahada ya kwanza. Baadaye aliendelea na masomo ya juu zaidi (postgraduate), University of Ohio, Athens, USA.

Marehemu Elias D Muganda aliajiriwa na kampuni ya Spiegel hadi alipostaafu.
Marehemu Elias D Muganda alianza kudhoofika kiafya katikati ya 2008, na kulazimu apelekwe na kulazwa hospitali mara kwa mara hadi tarehe 29/10/2008 ambapo mauti ilimfika.

Ameacha kaka yake William D. Rwezaura, na wapwe zake kadhaa.
Hakuacha mke wala mtoto.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.
AMINA.


Ni kama nilivyotumiwa taarifa hii...

Invisible
 
Mungu Mwenyezi katika Jina la Yesu ambaye alimuumba ndugu yetu na mpendwa wetu Elias D. Muganda, hatimaye amemrudisha kwenye makao yake ya milele.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Yesu libarikiwe. Amen.

Poleni wafiwa wote. Mwenyezi Mungu awape nguvu na matumaini wakati huu mgumu katika maisha. Amen.
 
Back
Top Bottom