Mshkaji kaja kukaa kwangu akidai ni kwa muda ila sasa naona hana mpango wa kuondoka

Emmanuel TM

Member
Sep 25, 2017
67
88
Ndio nimaliza chuo na ndio rasmi nimeingia kitaa kupambana na maisha. Nimepanga mahali nasukuma maisha kwa mishe zangu ndogondogo maisha yanasonga

Sasa shida ni kwamba kuna mshkaji wangu nilisomaga naye shule ya msingi miaka ya nyuma kidogo kwa bahati nzuri tukawa washkaji ila sio kivilee sana kwasababu hatujazoeana, ushkaji wenyew ulitokea kwa sababu tulikuwa tunakaa majirani.

Sasa alikuja mkoa ninaoishi (niuweke kapuni) kutafuta riziki yake na yeye wana miradi ya familia mbali kidogo na mji, akashuka zake akaifanya kama miezi miwili hivi wakawa wameimaliza kabisaa wanasubili matokeo ya mradi wao wa kilimo

Shida iko hivi jamaa alivyomaliza akasema anakuja mjini kunisalimia then ataendelea na mishe zake nikasema sio kesi nikamkaribisha

Sasa tangu nimkaribishe mshaji hana ratiba kabisa ya kusepa ndio kwanza anataka na yeye afanye mishe zake hapahapa dah, nimefeel kama kubanwa hivi kwasababu matumizi na bills zote ni juu yangu hata sielewi anasepa lini ukicheki ndio kwanza naanza maisha

NISHAURI
NImwambie mzee baba ajisogeze niendelee na mishe zangu kwa uhuru au nimpotezee apambane na yeye hadi atakapo kuwa sawa?

Sielewi wadau nafanye nn coz hata muda atakaosepa sijui ni lini na mimi ndio sipend kabisa kubanwa

Nanitamwambiaje asepe ?
NAWASILISHA
 
Jina lako emmanuel maana yake Mungu pamoja nasi sasa wewe mbona unataka kuwa shetani pamoja nawe?????

Kwani wewe kwenye hicho chumba umeoteshwa mizizi.???
Kama kweli una utu na upendo wa kusadidia tafuta chumba kingine wekeni godoro mshkaji wako ahame au wewe uhame..

Cha kwanza kabusa msaidie mshkaji wako kupata mishe ya kufanya..mkiweka malengo na wewe hpo kwenye system miezi mitano mshkaji wako atakua na getto lake..
Msaidie tu kwa kuwa huwezi jua wewe atakuja kukusaidia nani,
Tenda wema nenda zako msaada hauna risiti baba
 
Ndio nimaliza chuo na ndio rasmi nimeingia kitaa kupambana na maisha. Nimepanga mahali nasukuma maisha kwa mishe zangu ndogondogo maisha yanasonga

Sasa shida ni kwamba kuna mshkaji wangu nilisomaga naye shule ya msingi miaka ya nyuma kidogo kwa bahati nzuri tukawa washkaji ila sio kivilee sana kwasababu hatujazoeana, ushkaji wenyew ulitokea kwa sababu tulikuwa tunakaa majirani.

Sasa alikuja mkoa ninaoishi (niuweke kapuni) kutafuta riziki yake na yeye wana miradi ya familia mbali kidogo na mji, akashuka zake akaifanya kama miezi miwili hivi wakawa wameimaliza kabisaa wanasubili matokeo ya mradi wao wa kilimo

Shida iko hivi jamaa alivyomaliza akasema anakuja mjini kunisalimia then ataendelea na mishe zake nikasema sio kesi nikamkaribisha

Sasa tangu nimkaribishe mshaji hana ratiba kabisa ya kusepa ndio kwanza anataka na yeye afanye mishe zake hapahapa dah, nimefeel kama kubanwa hivi kwasababu matumizi na bills zote ni juu yangu hata sielewi anasepa lini ukicheki ndio kwanza naanza maisha

NISHAURI
NImwambie mzee baba ajisogeze niendelee na mishe zangu kwa uhuru au nimpotezee apambane na yeye hadi atakapo kuwa sawa?

Sielewi wadau nafanye nn coz hata muda atakaosepa sijui ni lini na mimi ndio sipend kabisa kubanwa

Nanitamwambiaje asepe ?
NAWASILISHA
Ushauri gani?Wewe kwani huna wazee?
 
Msaidie apate mishe ya kufanya baadae atahama geto kwako atajitegemea na sio kumfukuza.
 
Usimfukuze ila mchane tu kuwa mzee baba, shemeji yako anataka kuja harafu sielewi itakuwaje hapa? Tena mwambie demu ana mimba yako so kakaza kuja kukaaa na wewe.... Baada ya miezi akisepa zuga kumcheki stor mbili tatu ingiza mada ya demu wako mimba kutoka uzunika sanaaaaaa.... Mwana atakupa pole ila ushikaji utaendelea na atakuwa tayr ana kwake.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom