Mshitakiwa kesi ya mauaji azimia mahakamani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,073
1,250
MSHITAKIWA wa kwanza katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza, Leonard Bihondo, Oscar Jumanne (30) amedondoka mahakamani na kupoteza fahamu.

Mshitakiwa huyo alidondoka akiwa kizimbani mara baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Godfrey Mwambapa kuahirisha kwa mara nyingine kesi hiyo kufuatia upelelezi kutokamilika.

Mshitakiwa huyo alipozinduka alidai kuona watu waliokuwa na mikuki wakitaka kumuua na alipohamaki ndipo alipodondoka. Hata hivyo alibebwa na kupelekwa kwenye karandinga la polisi.

Meya Bihondo aliyekuwa diwani wa kata ya Isamilo kwa tiketi ya CCM alikamatwa na jeshi la polisi Mei 19, mwaka huu majira ya saa 10 alasiri katika uwanja wa ndege wa jijini Mwanza akitokea Dar es Salaam na kuunganishwa na watuhumiwa wengine wa mauaji ya Katibu wa CCM kata ya Isamilo, Bahati Stephano (50) aliyeuawa Mei 14 mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana.

Bahati aliuawa kwa kuchomwa kisu baada ya mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Oscar ambaye ni mshitakiwa wa kwanza kuingia ofisini kwa katibu huyo akisingizia kuwa na shida za kiofisi na baada ya kuruhusiwa kuonana naye ndipo alimchoma kisu.

Mbali na Meya huyo watuhumiwa wengine ni pamoja na Oscar aliyekamatwa siku ya tukio ambaye anadaiwa kumchoma kisu, Baltazar Shushi (43) na Abdul Hausi (45). Kesi hiyo ya ya jinai namba 18 ya mwaka huu imeahirishwa hadi Desemba 31, mwaka huu itakapotajwa tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom