Mshitaki wa Sendeka aishi nyumba ya Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshitaki wa Sendeka aishi nyumba ya Lowassa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msindima, Aug 20, 2009.

 1. M

  Msindima JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Na Charles Ngereza


  20th August 2009  [​IMG]
  Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher ole Sendeka.  Kesi inayomkabili Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher ole Sendeka, ya kumshambulia James Millya jana ilianza kusikilizwa huku mlalamikaji akielezwa kwamba anaishi nyumba ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
  Millya ambaye ni shahidi wa kwanza kwa upande wa Jamhuri alijikuta katika swali gumu la kueleza nyumba anayoishi ni ya nani baada ya upande wa utetezi kuanza kumhoji baada ya kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
  Wakili wa upande wa utetezi kutoka kampuni ya The Professional Center, Kamara Mpaya, alimtaka Millya aeleze pamoja na mambo mengine anakioishi na ni nyumba ya nani. Mahojiaono hayo yalikuwa kama ifuatavyo:
  Wakili: Nyumba unayoishi ni ya nani?
  Shahidi: Sijui.
  Wakili: Nikikuambia ni ya Lowassa utakataa?
  Shahidi: Siwezi kukubali wala kukataa. Kutokana na jibu hilo watu waliokuwa wamefurika mahakamani wakifuatilia kesi hiyo, waliangua kicheko.
  Awali shahidi huyo alikana maelezo yake aliyoyatoa polisi na ripoti ya daktari aliyempa matibabu baada ya kipigo.
  Hali hiyo ilijitokeza wakati jopo la mawakili watano maarufu waliojitosa katika kesi hiyo kumhoji Millya mhakamani. Shahidi huyo alianza kutoa ushahidi wake akiongozwa na wakili wa Serikali, Luena Luena, ambapo baadaye upande wa utetezi ulianza kwa kumhoji shahidi huyo.
  Upande huo wa utetezi ulianza mahojiano kama ifuatavyo:
  Wakili: Shahidi hebu iambie mahakama unaitwa nani na una umri gani?
  Shahidi: Naitwa James Millya na umri wangu ni miaka 31.
  Wakili: Ulizaliwa mwaka gani?
  Shahidi: Tarehe 18.12.1978
  Wakili: Mbona katika fomu namba tatu ya polisi inaonyesha kuwa una umri wa miaka 30.
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Unaishi wapi?
  Shahidi: Sakina
  Baada ya maswali haya aliulizwa nyumba anayoishi ni ya nani.
  Kadhalika wakili Mpaya alimuuliza ifuatavyo:-
  Wakili: Siku ya tukio unalodai kufanyiwa na mtuhumiwa nini kilitokea?
  Shahidi: Nilifika katika ukumbi wa semina TTC Monduli.
  Wakili: Baada ya kufika ulikuta nini?
  Shahidi: Nilikuta wajumbe wakiwa katika mchakato wa kuandaa maazimio ya semina.
  Wakili: Je, ulipewa nafasi ya kutoa mchango wako?
  Shahidi: Ndio nilitoa mchango wangu na niliwalaumu wanasiasa wanafiki kuwa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi katika maeneo ya wafugaji.
  Wakili: Je, hao wanasiasa uliowataja kuwa wanafiki walikuwa kwenye semina hiyo?
  Shahidi: Hapana nilikuwa nazungumzia kwa ujumla tu sikumlenga mtu.
  Wakili: Kabla ya wewe kutoa mchango wako ni nani mwingine alichangia mada.
  Shahidi: Christopher Sendeka Mbunge wa Simanjiro.
  Wakili: Baada ya kutoka ukumbuni nini kiliendelea?
  Shahidi: Nilielekea katika eneo la kupata chakula na wajumbe wengine ambapo nilimsalimia Sendeka, lakini akanitamkia kuwa nimemdhalilisha, na nilimjibu kuwa sikufanya hivyo lakini ghafla alinipiga kofi nikaanguka chini.
  Wakili: Baada ya kuanguka chini nini kingine kilitokea?
  Shaihdi: Niliona Sendeka alitoa bastola na kuanza kuikoki na kuelekeza kwangu.
  Wakili: Mbona katika maelezo yako uliyotoa polisi hakuna sehemu uliyoandika kuhusu mtuhumiwa kukuelekezea bastola?
  Shahidi: Kimya
  Aidha, mahojiano hayo yaliendelea ambapo shahidi huyo alifikia hatua ya kukana maelezo yaliyokuwa kwenye taarifa alioyoisaini mwenyewe na kusema kuwa sio maneno yake. Katika hatua nyingine mahakama pia ilikataa kupokea fomu ya matibabu kwa madai kuwa haikusaniwa na daktari mhusika hatua ambayo upande wa utetezi ulidai kuwa inabatilisha uhalali wa kutumika katika kesi hiyo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hapo mbona hakuna mjadala. Huyu kijana ni pandikizi la Lowassa na Arusha nzima tunajua. Sendeka ni mpiganaji haswa na Lowassa hamtaki ila kama Mungu anamyaka atainuliwa tu. Ningekuwa bado kijana ningemshughulikia huyu msaliti wa wananchi. Naomga wana JF mniruhusu ni mtusi kidogo
   
 3. M

  Msindima JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Shangazi punguza hasira usimtusi kijana wa watu yawezekana hajui anachokifanya au amefanya kwa shinikizo fulani.
   
 4. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  syle za Lowassa ajue hii sio enzi ya zama za kale,mambo yote yanafumuliwa tuu,mafisadi waje na mbinu zingine za kujiimarisha si mitindo ya kizamani tushaishtukia sana.Hongera Sendeka endeleza Mpambano
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Shangazi we shusha tu japo tusi ili upate amani kuliko kubaki na fundo moyoni. Haya shusha mama!!!!
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sijaelewa tatizo ni huyu bwana anayemshitai sendeka kukaa kwa kwenye nyumba ya lowassa au ni nini?Sijaelewa
   
 7. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  msindima,

  Naufikiria ushauri wako ila kuna watu wanauzi. Nafurahi kwamba wamasai tu waelewa na aangalie asje kuambiwa alipe fadhila!!!!
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  duh!
  si n'chezo mazee!
  eddo amejipanga
   
 9. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Niambie moja lililo zuri kwa mwanamume nimpe
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu wewe kila kitu huelewi soma kwanza maelezo ndo utaelewa mkuu.
   
 11. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Kweli kigogo utakuwa unakalia kigogo. Unadandia basi bila kujua linaenda wapi. Soma kwanza tangu mwanzo hoja ni nini then ujue mazingira ya issue nzima ndio ujadili.
   
 12. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Kweli kigogo utakuwa unakalia kigogo. Unadandia basi bila kujua linaenda wapi. Soma kwanza tangu mwanzo hoja ni nini then ujue mazingira ya issue nzima ndio ujadili.
   
 13. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Huyu jamaa (anayemtuhumu sendeka) kukaa kwenye nyumba ya lowasa inamaanisha yeye ni swahiba wa lowasa na kwa kuwa lowasa anawachukia wapinga ufisadi ndo maana anataka kumpa (sendeka) kesi isiyo kuwa na kichwa wala miguu kwa kupitia vibalaka wake ambao anawatumia na kuwahifadhi kwa kuwapa nyumba za kuishi.
   
 14. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
   
 15. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Shangazi,
  Hili ndilo tusi ulilotakiwa kutoa kwa mwanaume kama ulivyoomba ushauri!!!
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi uzee huu ndo unanipa shida
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kumbe kesi hii haina kichwa wala miguu basi hakuna shaka na hukumu yake itakuwa kama ya akina zombe ,haitakuwa na kichwa wala miguu
   
 18. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ila ina mikono na tumbo.........(ufisadi na rushwa)
   
 19. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,148
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Naona kila thread huelewi, itabidi tuanzishe thread za tuition kwenu akina Kigogo.

  Cheers
   
 20. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #20
  Aug 20, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,148
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Taratibu Shangazi, kukalia kigogo ni hatari.....
   
Loading...