Serikali: Tunafuatilia suala la Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini kuzuia ndege ya ATCL. Ni kufuatia Hermanus P. Steyn kufungua shauri

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ameomba radhi kwa usumbufu ulijitokeza kwa abiria wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) waliokuwa wasafiri kutoka Johannesburg kwenda jijini Dar

Ameomba radhi hiyo kutokana na abiria hao kushindwa kusafiri kutoka uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg baada ya ndege hiyo kushindwa kufanya safari kama ilivyopangwa kutokana na kuzuiwa

Kwa mujibu wa taarifa ambayo Serikali imepokea, ndege hiyo imezuiwa kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Johannesburg na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inafuatilia ili ndege iachiwe

82845FA0-FD4B-4ECF-ACA9-51CAB97E6A6C.jpeg


Kesi imefunguliwa na Hermanus Phillipus Steyn

94CAE50B-8443-4C46-BCD3-7765A33B36E3.jpeg

00AEE39A-EC16-4D7F-B1D0-C6BE5DC9D0AA.jpeg
 
Mpaka sasa sijaelewa kwanini ndege yetu imekatwa huko south africa, hawa si ndugu zetu.

Hii ni taarifa ya huzuni kabisa kwa nchi yetu, najua wapo ambao mtafurahia, mtalichulia hili suala kisiasa na mtatamani ndege hiyo iendelee kushikiliwa.

Watanzania wote kwa pamoja tuwatie moyo viongozi wetu hasa Mhe. Rais John Pombe Magufuli.

Mungu atusaidie na hakika hili nalo tutashinda.
 

Attachments

  • ECrPv4lXkAIVH78.jpg
    ECrPv4lXkAIVH78.jpg
    66.8 KB · Views: 70
Nimeona hii press release huko twitter, nikasema labda ni habari fake!!

Kwakuwa wanamshikia Lissu Bango huko mahakamani,basi na wao wawe wapole tu na wala wasilalamike maana sheria ni msumeno.

Hapo itabidi wagharamie chakula na malazi ya abiria wote in case watakosa ndege ya kuwasafirisha hao abiria.

Tusipotendeana haki sisi wenyewe humu nchini,haya majanga hayataisha(Mungu ataaendelea tu kutuadhibu)

Mungu si mwanadamu, na wote tuko sawa mbele yake.
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom