Mshindi wa Maisha Plus Ndani ya Bunge. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshindi wa Maisha Plus Ndani ya Bunge.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jun 26, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Donisya Thomas -- ZANZIBAR LEO

  MSHINDI wa shindano la Maisha Plus Abdulhalim Hafidh Salum, leo anatarajiwa kuwasili mjini Dodoma kuitikia wito wa Spika Samuel Sitta, kumtaka ahudhurie bungeni kutambulishwa.


  Spika Sitta alitoa mualiko huo juzi alipokuwa akiwatambulisha washiriki wengine wa shindano hilo lililomalizika kwa Salum kutwaa ushindi na kutia kibindoni shilingi 10,000,000.

  Sitta amemtaka mshindi huyo kufika katika afisi za bunge ili aweze kupokewa kwa heshima zote kutokana na ushindi huo mwanana pamoja na kujionea shughuli mbali mbali za bunge.


  "Yuko wapi Abdulhalim, mbona hamjamleta tukamuona, mleteni bwana tumuone mshindi wetu wa Maisha Plus", aliuliza Spika katika utambulisho huo.


  Akizungumza na gazeti hili, Salum alisema amepata mualiko rasmi kumtaka kwenda Bungeni na ameupokea kwa mikono miwili.Alisema hiyo ni heshima kubwa kwake pamoja na Zanzibar, kwamba hata Mtendaji Mkuu wa Afisi ya Bunge amemtambua na kumpatia nafasi hiyo adhimu.


  "Ni kweli nimealikwa Bungeni, nimepokea simu leo (jana) mchana nikitakiwa nihudhurie huko nami niko njiani, Mungu akipenda kesho nitakuwepo Dodoma", alisema.


  Abdulhalim Hafidh alikuwa miongoni mwa washiriki 53 walioshindana katika kijiji cha Maisha Plus na kutwaa donge nono la shilingi 10,000,000 baada ya kuibuka mbele ya washindani wengine.

  SOURCE: JITAMBUE
   
 2. L

  LUKULUKU Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wazi mashindano haya ni sawa na yale mashindano ya Big brother yanayofanyika kule afrika ya kusini. ni mashindano ambyo Ngono imetwala kwa washiriki na hasa baada ya kuwekwa kambi wakati kunamchnganyiko ya wanawake na wanaume. Jana nilimuona S.S akifurahia kwa kualikwa huyu jamaa katika ukumbi wa Bunge na SS alitoa laki tatu kama zawadi lakn nawasahauri watanzania kwamba mchezo huu ulioanzshwa na msuoud kipanya unaelekea kule kuile kwanye Big brother AFrika kwa hivyo tuwe macho .
   
 3. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lukuluku nawe! mmmmmmmmh! Kazi Kweli kweli!
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Watz hamwishi kuiga.
   
Loading...