Mshikamano Toronto:Binti Mtanzania Yuko ICU

Rest in Peace Eva
so painful!!!
Asnte Pasco kwa taarifa
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN
 
Up-date 1.
Kwa Toronto, msiba uko kwa Dada wa Marehemu, Juliet Gembe, alikuwa mwanahabari Channel Ten kabla hajaelekea Toronto. Mipango ya kuurudisha mwili nyumbani kwa mazishi inafanywa na Watanzania walioko Toronto, ikiratibiwa kwa karibu na Jamii ya WaTZ wa hapo Toronto.

Kwa Dar es Salaam, msiba uko nyumbani kwao, kwa Mzee Gembe, lile ghorofa pale Upanga, baada ya Califonia Dreamer.

Kazi kubwa kwa sasa ni resources mobilization ili mwili wa Dada yetu tuurejeshe nyumbani.

Poleni wafiwa wote,

RIP Eva Gembe.
 
Jamani, so sad! She was my school mate in high school. Tunaji-organise tujumuike na familia yake. She was very hard working, a leader, mshauri, friendly, intelligent, funny (nakumbuka jina letu la utani)! She was just too young to die. Mungu atusaidie wote tusije kufuru.
RIP dear EVA.
 
Jamani, so sad! She was my school mate in high school. Tunaji-organise tujumuike na familia yake. She was very hard working, a leader, mshauri, friendly, intelligent, funny (nakumbuka jina letu la utani)! She was just too young to die. Mungu atusaidie wote tusije kufuru.
RIP dear EVA.

Pole sana King'asti
 
huwezi kuibuka out of no where na kusema sitakufa bali nitaishi kuyasimulia matendo makuu ya Bwana. Mungu sio mfanya niashara ya neno. inatakiwa uwe mtendaji wa neneo kabla.

yeye amenukuu maneno matakatifu wewe unamsema vibaya do u know his/ her life so to judge others?
 
MSIBA TORONTO, CANADA

Marehemu Evaline Gembe

Familia ya Bwana na Bibi Gembe wa Upanga-Dar-es-salaam na Tabora, wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Evaline Gembe(pichani) kilichotokea hapo juzi tarehe 30.3.2010 huko Toronto,Canada. Evelyne amefikwa na mauti katika hospitali ya St.Michael’s ya Toronto alipokuwa amelazwa.

Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa dada yake, Julie huko huko Toronto,Canada.

Ukiwa kama mtanzania,ndugu,jamaa au rafiki, unaombwa kuchangia fedha,hali na mali kwa ajili ya kuwezesha kuusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi mapema kadri iwezekanavyo kwani kama wengi wenu mnavyofahamu, mwili unavyozidi kukaa Funeral-Home,gharama ndivyo zinavyozidi kuongezeka. Mwili utasafirishwa punde tu zitakapopatikana fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia gharama husika.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account maalumu ya wafiwa kama ifuatavyo:

BANK : CIBC (Canadian Imperial Bank of Commerce)

ACCOUNT NUMBER: 5681839
TRANSIT NUMBER: 00902
INSTITUTE NUMBER: 010
SWIFT CODE: CIBCCATT

Vilevile unaweza kutumia E-mail Money Transfer kwa Sania Esmail.Anuani yake ni saniae@yahoo. ca au kuwakilisha msaada wako kwa kutumia anuani hii:

1025 SCARLETT ROAD,

APT 606, BUZZ # 178
TORONTO ON, M9P 3V3.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Julie +1 416-247-8318
Esmail Manambi- +1 647- 299-2572
Victor Wambura- +1 647-428-4118
Prosper Luteganya- +1 905 626 3764

Tafadhali chukua muda kuwafariji na kuwaombea ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa na itakayotolewa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi - Amen.

Source-Michuzi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom