Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Mimi mwenyewe na trade in forex lakini sina muda wa kumshawishi mtu. Anayetaka aifanye, hasiyeitaka aache
Hata kwenye mataifa makubwa wapo wengi tu wasioijua.

Hakuna anayeipromote ila sisi tukikaa na kuanza kujadili mada zetu nyie mnakuja na hoja zenu uchwara.

Malalamiko ni kwa watu wanaoingia kichwakichwa bila kufanya research yoyote.

Mwisbo wa yote kama jamaa yako .anakijua anachokifanya basi kuna siku utakuja kuyaonea aibu haya uliyoyaandika humu. Unless kama anagamble, maana kuna very thin line kati ya kufanya forex na kugamble

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama unataka kufanya biashara yoyote ( Si tu Forex ) Kwasababu umesikia mtu ametengeza kiasi kadhaa Kwa wiki au mwezi upo katika dalili za awali za kupata hasara katika biashara hiyo kabla ya kuanza biashara.

Sijawahi kusikia Mfanyabiashara yoyote duniani aliefanikiwa alijiingiza kwenye biashara kwasababu za kuvutiwa na kiwango cha Pesa alichosikia kimetengenezwa na MTU flani. Ukiingia kwenye biashara yoyote kwa mantiki hiyo lazima ulie mwisho wa siku. Unakumbuka waliovamia biashara ya matikiti, Mayai ya kwale n.k.. Kawaulize sasa hivi kilichowakuta. Wengine waliambiwa heka moja ya matikiti unaweza kupata million 30.

Hata wale walioenda pale kWa Ontario nilijua kuanzia mwanzo wengi watapata hasara. Kwasababu wengi walijiunga na forex kwa vigezo kama vyako.

NB: Nakuomba utafute maarifa mitandaoni. Kama ni mvivu wa kusoma itumie YouTube vizuri. Hakuna ambacho hakipo YouTube. Mimi asilimia zaidi ya 80 ya knowledge ya Forex nimejifunza mwenyewe kwa msaada wa YouTube na Vitabu. Kutoka YouTube kuna MTU anaitwa Adam Khoo huyu ndio kanisaidia sana sana. Nadhani ni RAIA wa Indonesia. Ana video yake kule ya forex introduction lazima uelewe.

NB: Forex sio biashara ya kupata biashara haraka kama unavyodhani. Tembelea tutorial zote za waliofanikiwa lazima uambiwe hiki. Kufanikiwa haraka ni wewe tu na knowledge yako. Kuna Jamaa namfahamu mwezi December kaweka capital ya USD 1000 na Leo tunavyozungumza ana USD 12,000... Ila kuna wengine kwa kiasi hicho hicho mpaka sasa wameshachoma account. Nadhani kwa huo mfano utakuwa umejifunza kitu.

Lastly usiingie kwenye forex kwa kushawishiwa na posts za profits. Ingia kwenye biashara kwa kuelewa biashara ilivyo. Hizo Pesa ni matokeo ya juhudi zako tu.
Amini nakwambia siku ukija kujua real Forex ilivyo, utajikataa mwenyewe. Achana na hii ya WALIMU uchwara wa kufundishana kila siku support & resistance, etc.Jifue mwenyewe halafu ulete mrejesho hapa.

Have a good Blessed Sunday.
Regards.

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya kuteseka sana na shughuli za manamba (Manual work) nilikaa chin nikatafakari....nikaona kutusua sio lazima uteseke aisee....nikaanza kufanya mishe soft lakn zinaingiza pesa..watu wakawa wanashangaa mshikaj nang'aa tu kitaa....Kwa sasa Forex nainyatia , kwa mtu makni ni fursa...najua itasumbua somehow..ila mwisho wa siku nitakuwa naingiza pesa huku nimekaa, taratibu nakunywa juice ya Azam embe.....mambo ya kujiloweka kwenye tope na kilimo cha matikiti nimewaachia wenye vipaji vyao
 
Nyie ndo wale mkikanyagwa bahati mbaya afu mkaambiwa sorry mnarusha maneno na ngumi kabisa...jamaa si kasema mniwie radhi walokole au inamaanisha nini hiyo sentensi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna aliyempiga yeye wala hoja zake; nilichokuwa nafanya ni kutoa elimu ndogo na ufafanuzi sahihi juu ya hilo neno "walokole" basi. Hakuna ugomvi on anything else bro.
 
Nyie ndo wale mkikanyagwa bahati mbaya afu mkaambiwa sorry mnarusha maneno na ngumi kabisa...jamaa si kasema mniwie radhi walokole au inamaanisha nini hiyo sentensi

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiingii akilini kama mtu atakuomba msamaha kabla ya kukukanyaga ndipo akakukanyaga kimsingi lazma uongee kama uko timamu na alichokua anakifanya bro hapo nafikiri nkutoa elimu kuhusu wokovu ambayo ndugu yetu kaikosa ndio sababu akafananisha wokovu na vitu vya kijinga...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kuteseka sana na shughuli za manamba (Manual work) nilikaa chin nikatafakari....nikaona kutusua sio lazima uteseke aisee....nikaanza kufanya mishe soft lakn zinaingiza pesa..watu wakawa wanashangaa mshikaj nang'aa tu kitaa....Kwa sasa Forex nainyatia , kwa mtu makni ni fursa...najua itasumbua somehow..ila mwisho wa siku nitakuwa naingiza pesa huku nimekaa, taratibu nakunywa juice ya Azam embe.....mambo ya kujiloweka kwenye tope na kilimo cha matikiti nimewaachia wenye vipaji vyao
Safi sana mkuu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sizungumzii forex bali hilo jina au neno "walokole au ulokole". Neno hilo halina maana wala uhusiano na sisi TULIOMKIRI NA KUMPOKEA YESU KRISTO ALIYE HAI KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU. Hilo ni jina au neno analotumia Shetani na mawakala wake kutaka kuudharirisha WOKOVU WETU. Na kwa kweli kwa kiasi fulani kafikia lengo lake ingawa hatafanikiwa milele. Sisi SIO WALOKOLE bali SISI NI WANA WA MUNGU TULIOPOKEA NEEMA YA WOKOVU, NI WATU TULIO OKOKA.
Ona hili nalo
 
Nimepitia comment nyingi sana,ila mwisho wa siku kama kitu anakifanya fulani na kinamuingizia kipato sio lazima na wewe ufanye,fanya chako maisha yaendelee ,hakuna haja ya kujitetea after all no body will feed you when you will be broke...dawa ya kuonesha unachofanya kinalipa ni maendeleo tu...na hakuna watu ambao unatakiwa kuwa nao makini ukiwashirikisha fursa kama watanzania...watanzania waoneshe mafanikio kwanza ndo mtazungumza lugha moja....MWISHO..biashara yoyote bila kuwa na elimu tosha basi huna unachokifanya....risk is everywhere

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi imejaa misukule... Nchi ina RAIA million 50+ lakini amini nakwambia kati ya idadi hiyo ni raia hawazidi 1000 wenye sifa za kuitwa binadamu. Mingine yote iliyosalia ni Mi swala,Nyumbu na misukule ya kuswagwa na fimbo.

Nchi Bado ina safari ndefu ya kuwageuza hii misukule kuwa binadamu Kamili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki ndicho kinanishangaza

Mbona nguvu inayotumika kubwa sana?
Mtu akikataa fursa shida iko wapi mpaka ujae upepo?
 
Nimepitia comment nyingi sana,ila mwisho wa siku kama kitu anakifanya fulani na kinamuingizia kipato sio lazima na wewe ufanye,fanya chako maisha yaendelee ,hakuna haja ya kujitetea after all no body will feed you when you will be broke...dawa ya kuonesha unachofanya kinalipa ni maendeleo tu...na hakuna watu ambao unatakiwa kuwa nao makini ukiwashirikisha fursa kama watanzania...watanzania waoneshe mafanikio kwanza ndo mtazungumza lugha moja....MWISHO..biashara yoyote bila kuwa na elimu tosha basi huna unachokifanya....risk is everywhere

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kbs

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuza $40 mpaka ikakaribia 500, stop loss ikatembea na mzigo wote siku ya news CAD baada ya hapo kila nikijipanga wanaondoka na mzigo mazima, nikasema nitakuja kulaza njaa watoto!
Pair yenye Cad na Aud siyo za kuziamini maana zinaadhiriwa na mafuta na dhahabu, Australia ni mzalishaji mkubwa wa dhahabu na Canada ni mzalishaji mkubwa wa oil. Kwa hiyo, hivyo vitu vinasababisha pair zenye hizo hela zisiwe na utulivu sokoni. Japo CAD ni nzuri sana kwenye news ukiwa unajua vizuri kutrade news

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom