RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 51,719
- 107,833
Ningekuwa naangalia nani kapata nini ningeshaingia. Ila nina vigezo vyangu. Let me tell you, nikiona mtu successful namuuliza WHAT DO YOU DO AND HOW DO YOU DO IT? Then I go to work. $1000 Ku raise to $12,000 sio ajabu. I raised $5000 to over $150,000 in less than 3yrs.Mkuu kama unataka kufanya biashara yoyote ( Si tu Forex ) Kwasababu umesikia mtu ametengeza kiasi kadhaa Kwa wiki au mwezi upo katika dalili za awali za kupata hasara katika biashara hiyo kabla ya kuanza biashara.
Sijawahi kusikia Mfanyabiashara yoyote duniani aliefanikiwa alijiingiza kwenye biashara kwasababu za kuvutiwa na kiwango cha Pesa alichosikia kimetengenezwa na MTU flani. Ukiingia kwenye biashara yoyote kwa mantiki hiyo lazima ulie mwisho wa siku. Unakumbuka waliovamia biashara ya matikiti, Mayai ya kwale n.k.. Kawaulize sasa hivi kilichowakuta. Wengine waliambiwa heka moja ya matikiti unaweza kupata million 30.
Hata wale walioenda pale kWa Ontario nilijua kuanzia mwanzo wengi watapata hasara. Kwasababu wengi walijiunga na forex kwa vigezo kama vyako.
NB: Nakuomba utafute maarifa mitandaoni. Kama ni mvivu wa kusoma itumie YouTube vizuri. Hakuna ambacho hakipo YouTube. Mimi asilimia zaidi ya 80 ya knowledge ya Forex nimejifunza mwenyewe kwa msaada wa YouTube na Vitabu. Kutoka YouTube kuna MTU anaitwa Adam Khoo huyu ndio kanisaidia sana sana. Nadhani ni RAIA wa Indonesia. Ana video yake kule ya forex introduction lazima uelewe.
NB: Forex sio biashara ya kupata biashara haraka kama unavyodhani. Tembelea tutorial zote za waliofanikiwa lazima uambiwe hiki. Kufanikiwa haraka ni wewe tu na knowledge yako. Kuna Jamaa namfahamu mwezi December kaweka capital ya USD 1000 na Leo tunavyozungumza ana USD 12,000... Ila kuna wengine kwa kiasi hicho hicho mpaka sasa wameshachoma account. Nadhani kwa huo mfano utakuwa umejifunza kitu.
Lastly usiingie kwenye forex kwa kushawishiwa na posts za profits. Ingia kwenye biashara kwa kuelewa biashara ilivyo. Hizo Pesa ni matokeo ya juhudi zako tu.
Amini nakwambia siku ukija kujua real Forex ilivyo, utajikataa mwenyewe. Achana na hii ya WALIMU uchwara wa kufundishana kila siku support & resistance, etc.Jifue mwenyewe halafu ulete mrejesho hapa.
Have a good Blessed Sunday.
Regards.
Sent using Jamii Forums mobile app