Mshikaji wangu ameanza kucheza forex, kila siku anauza vitu kidogo kidogo

Status
Not open for further replies.
Alianza kama utani baada ya kurudi likizo ya semister ya mwisho huyu mshikaji wangu wa chuo sijui alikutana na nani huko kwao akamshauri kuhusu mambo ya forex,
Mkuu ujue hii kitu ni kama pombe unaanza taratibu lakini ni vigumu kuiacha, kaa nae chini uongee nae kiutu uzima asipo kuelewa mwache sababu umesema ni jamaa na siyo ndugu
Alivyorudi akanisimulia kuhusu hiyo inshu mi nilichomwambia ni kitu kimoja tu hiyo kitu ya forex mi nilishasoma sana mada zake huko Jamii forum kwa kina Ontario na kujua hasara na faida zake kuna watu wameunguza acount zao wanalia kilio cha mbwa koko hakunisikia,

Sasa bhana wale watu aliokutana nao huku wakawa wanamshauri anatoka dom to dar kwenye semina na darasa lao na kila akirudi story ni forex,forex na yeye,

Basi bhana miezi kadhaa imepita baada ya kutrade sana na ile acount ya dermal kafungua real Account kinachomkuta huko mi sijui naona tu kila siku anauza vitu,

Alianza na Laptop yake min, akafata desk top yake ,juzi kati kauza mtungi mkubwa wa gase pamoja na jiko lake, naona kabakiwa na friji pamoja na kitanda na ata hivyo naona analipigia mahesabu friji anataka kuliuza na hilo sasa sijui kimempata nini huko kwenye forex,

Daily nampa ushauri aachane na hiyo biashara yake ya forex naona hanisikii sasa mi nasubiri kuona mwisho wake.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa anatakiwa Afanye nini mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna group moja la forex jamaa kaelezea mkasa wake huo wa jamaa yako cha mtoto.
Yeye anasema pia alipocheza Mara ya kwanza akala,akachukua 3m akafund account akajilipua usiku asubuhi akakuta acc hoi,kwakua hakujua kosa lake akakopa mtu m kadhaa akazipoteza ikamlazimu kuuza gari take arudishe pesa.
Ukishasikia mtu anasema nimecheza&nacheza forex huyo hajui alitendalo,forex ni serious issue, aichukulie kama anavyosoma chuo.
 
Status
Not open for further replies.
59 Reactions
Reply
Back
Top Bottom