mshaurini shosti yangu

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
shost yangu katumiwa sms na bf wake ya kumuomba mchango wa harusi. walikuwa wapenzi pindi wapo chuo baada ya kumaliza chuo kila mmoja akarudi kwao. mkaka kwao ni dsm na mdada kwao ni mkoan. thou hawakuwa na promise za kuoana bt mkaka kamstukiza.je mkaka atakuwa serious au anamjaribu?shost kachanganyikiwa.ushaur plz!
 
anaweza akawa anamtania au anamkomoa..........mwambie shosti wako naye amjibu hivi "Ingawa umenishtukiza kwa mda ambao sina hela na mimi nipo bize pia ila nitachanga maana nataka ndoa yako itangulie ili uwe best man wangu kwenye arusi yangu,maana sasa hivi tunamalizana na wazee''
then ataeleza mwenyewe kama alikuwa anatania
 
Amechanganyikiwa na nini sasa wakati hawakuweka promise yeyote kwenye mahusiano yao.Amchangie mwenzake aache ushamba kwani hakujua mapenzi ya chuo yakoje.
 
Mwenzie alimuona kama njia, maskini shostito alikua kafika? hayo sio mambo ya kujaribiana ati!
 
Hii inaitwa Message sent and delivered.
Alishindwa namna ya kumwambia bye bye baby
akaona atumie njia hiyo kwa kufikisha ujumbe
 
Poa poa tu kwenye haya mapenzi ya kileo. Hakuna kugandana wala nini kama hamjaingia contract
 
sasa anachanganyikiwa nini?

Kila mtu alianza ustaarabu wake ndo maana hakukuwa na mawasiliano, na hakukuwz na makubaliano yoyote ya kuoana......

Mwambie atafute 50,000 amtumie mchango, vitu vidogo hivyo
 
mapenzi ya chuoni ni ''Hit and Run'', mpe pole sana huyo shosti wako na hata kama mpo wanachuo wengine hapa mnaojipa moyo na hizo bond zenu mjue hizo ni weak bond zitavunjika wakati wowote maana kila mmoja ana wake huko alipotokea na mara nyingi baada ya kumaliza chuo kila mmoja urudisha majeshi kwa yule mpenzi wa zamani.

Mwambie amchangie tu kama ana uwezo wa kufanya hivyo ikiwa jamaa anamtania atamueleza au kama yupo serious atamshukuru kwa mchango wake.
Inabidi tuzingatie kuwa chuoni ni sehemu ya kwenda kutafuta elimu na sio sehemu ya kufanya uzinzi.
 
anaweza akawa anamtania au anamkomoa..........mwambie shosti wako naye amjibu hivi "Ingawa umenishtukiza kwa mda ambao sina hela na mimi nipo bize pia ila nitachanga maana nataka ndoa yako itangulie ili uwe best man wangu kwenye arusi yangu,maana sasa hivi tunamalizana na wazee''
then ataeleza mwenyewe kama alikuwa anatania
khhaa! i salute u mkuu
 
mh Mwali jaman,hebu vaa uhusika afu ushauri!
Hakuna cha kushahuri hapo. Si kaka amesha amua?
Kama shosti ataweza, ajitahidi kutuma mchango wake
kama anaona ni dharau kukataliwa kwa njia hiyo basi...
apige kimya tuu. wala asijaribu kufatana nae sana
ikiwa ni utani kaka atakuja mwenyewe. ila it looks serious
 
Mwali,shost kaumia yan mpk namuonea huruma make alikuwa ashajiaminisha kuwa ndo mumewe mtarajiwa.ghafla bin vuu ndo katumiwa hyo sms. nimejaribu kumshauri lakn!
 
Last edited by a moderator:
Level, nimemuonesha shost ushaur wako amesema anaogopa hata kumjibu make akikuta mkaka yupo serious ataumia zaidi. cha kufanya atapotezea tu!
 
Last edited by a moderator:
Hapo ndo akina dada mnanichosha kabisa mtu mnajua kabisa kuwa mnachezeana alafu unukuwa na mawazo yako binafsi kuwa utaolewa kweli kazi mnayo
Mwali,shost kaumia yan mpk namuonea huruma make alikuwa ashajiaminisha kuwa ndo mumewe mtarajiwa.ghafla bin vuu ndo katumiwa hyo sms. nimejaribu kumshauri lakn!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom