Mshauri wa ngazi ya juu wa UM apendekeza Afrika kujiendeleza katika ujenzi wa teknolojia

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
72
110
104822965_2809817982462830_3306134213967476704_n.png

Mshauri wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa Bi Jacquline Musiitwa amesema, maambukizi ya virusi vya Corona yameathiri vibaya uchumi na biashara za Afrika, huku thamani za sarafu za nchi nyingi za Afrika zikishuhudiwa kuporomoka zaidi.
Amezihimiza nchi za Afrika kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na China, huku akiwahamasisha wanasayansi wa huko kutoa mchango juu ya namna ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.
Mbali na hayo, Bi Musiitwa amevitaka vyombo vya habari vya nchi za Afrika na China kutekeleza majukumu ya kuondoa habari zisizo sahihi. Wakati China ikikabiliwa na shinikizo kutoka nje, inaendelea kutoa misaada kwa nchi za Afrika. Vyombo vya habari vya nchi za Afrika na China vinatakiwa kuripoti kwa usahihi mambo hayo, badala ya kuwaachia watu kutoka sehemu nyingine duniani kulaumu uhusiano kati ya China na Afrika kwa kisingizio chochote.

105904737_2809818142462814_4189049693004758567_n.png
 
Back
Top Bottom