Mshana Jr na wengine wenye uzoefu mje mnijibu

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,941
24,816
Ni hivi kuna kitu kilikuwa kinanisumbua sana Asa wakati wa kulala mchana mpaka nilikuwa naogopa nilijihisi kama kuna siku naweza kupitiliza.

Kitu chenyewe ni kwamba kuna hali frani ilikuwa inanitokea kila nikiwa nalala wakati wa mchana hasa nikilala chali ndio inanitokea.

Hali yenyewe ni kwamba wakati naanza kulala huo mchana wakati ambao hali ya hewa inakuwa tulivu ni kwamba napitiwa na usingizi mzito sana ila kilichokuwa kinaniogopesha ni kwamba wakati nipo usingizini basi naweza nikawa naitwa nasikia ila kuamka siwezi, yaani viungo vyangu vya mwili vinakuwa kama vimeshika ganzi haviwezi kufanya chochote.

Ila wakati huo huo nasikia kila wanachoongea nje na kinachofanyika ila tu kuamka siwezi na inanichukua muda mpaka niweze kuamka muda mwingine natumia nguvu kujiamsha au mpaka mtu aje anishitue ndio naweza kuamka.

Kwa kifupi hiyo hali ilikuwa inanitisha na ukizingatia mi ni muumini mzuri sana wa kulala Chali hiyo hali imenifanya niwe naogopa sana kulala mchana hadi Leo hii.

Hii inaweza ikawa ni nini mwenye ufahamu anijuze.

Zero iq
 
Sasa kwa kua umewaita wazee wa uchawi jibu langu hutolipenda ila ukweli ni ukweli inabidi uelezwe sio tuendelee kujazana ubashite.

Unavyolala chali, regardless ni mchana au usiku alafu hali hiyo ikatokea ni jambo la kawaida, sayansi inaliezea vizuri tu, hata mimi limenitokea mara nyingi mno, wewe ni mchana ila mimi hata usiku.

Hali yenyewe inajulikana kama "sleep paralysis", kuna aina mbili ya sleep paralysis, moja ni wakati umeingia kulala, kabla hujasinzia kabisa, nyingine ni kabla hujaamka. Sababu hasa ni nini?

Kulala kuna stage mbalimbali, ukiwa kwenye stage moja inayojulikana kama Rapid Eye Movement (REM), ubongo unazima signal kwenda kwenye misuli ili ukiwa ndotoni usijitingishe sana, sasa ikitokea ukaamka ghafla wakati bado upo kwenye REM stage, lazima u-experience hili tatizo sababu bado ubongo haujaamua kucontrol misuli ya mwili. Ukiwa kwenye hii stage, tulia tu usikilizie ndani ya sekunde chache ubongo utajishtukia kua kuna kitu hakiposawa na control itarudi kama kawaida. Na haihitaji hata kumuona daktari wala kuondoa sijui mapepo, ni jambo la kawaida sana lisilo na hatari yoyote.

Hiyo pekee ndiyo sababu, imehakikiwa mara nyingi tu kwenye experiments na mjadala ukafungwa. Kama unapenda kusikia hadithi za sijui kukaliwa na kobe au mbuzi endelea ila usizisambaze kwa wengine maana utakua unaongeza mabashite. Anayesema jinamizi muulize kama alishawahi kuliona umkamate uongo, ataanza kutapatapa.
 
Sasa kwa kua umewaita wazee wa uchawi jibu langu hutolipenda ila ukweli ni ukweli inabidi uelezwe sio tuendelee kujazana ubashite.

Unavyolala chali, regardless ni mchana au usiku alafu hali hiyo ikatokea ni jambo la kawaida, sayansi inaliezea vizuri tu, hata mimi limenitokea mara nyingi mno, wewe ni mchana ila mimi hata usiku.
embu elezea mkuu me hata nilale upande yani balaa..
 
Back
Top Bottom