Mshairi alowahishika namna moja kimkoa na kitaifa katika matokeo ya shule za sekindari.

Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,783
Points
2,000
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined Nov 18, 2012
2,783 2,000
MSHAIRI ALIEWAHI KUONGOZA MATOKEO YA KITAIFA YA SEKONDARI NA KUKAMATA NAFASI YA KWANZA KIMKOA NA KITAIFA.

Siku moja nakumbuka mtu mmoja aliwahi nifata na kuniuliza "nifanye nini ili nami niwe mshairi ?".
Nilimpa jibu la haraka na kumuambia " kama unataka kuwa mshairi basi cha kwanza kubali kuwa msomi"
Jibu hilo nililitoa ikiwa ni sehemu ya majibu yangu mengi ya nini kifanyike ili mtu kuwa mshairi ila ikumbukwe kwamba kuwa mshairi ni kipaji kutoka kwa Mungu kipaji ambacho kinakua uwezo wake kwa mtu kujifunza zaidi kuhusu sanaa ya ushairi.
Katika uchunguzi wangu niliofanya kwa kutazama wasifu wa washairi wa Afrika ya mashariki nimegundua kwamba asilimia kubwa ya washairi hao ni wasomi na wana taaluma (tutaangalia wakati mwingine suala hili) hali inayopelekea wengi kujitambua,kujua wanacho kifanya na kufahamu vyema aina ya sanaa wanayoifanya.

Mwaka 1993 katika nchi ya Tanzania mshairi kijana kabisa wa umri wa miaka ishirini na mbili mwenye kipaji cha ushairi alivunja rekodi ya kuwa kijana aliekamata nafasi ya kwanza katika matokeo ya shule za sekondari na kuwa wa kwanza kitaifa na wa kwanza kimkoa huku akiongoza mkoa wa Tabora,mkoa wenye historia ya ushairi na kiswahili katika Tanzania (tutaona katika maandiko mengine).

Audax Kahendaguza Vedasto ama kwa jina la ushairi anajulikana kama "Mwana wa kahenda" ni miongoni wa washairi wasomi Tanzania ambae alijizolea sifa ya kuwa mshairi alieweza kushika nafasi ya kwanza katika matokeo yake ya shule licha ya kuwa wengi kumkatisha tamaa kuwa hatofaulu kwa sababu wakati mwingine alikuwa akionekana kuandika mashairi tu.
Mwana wa Kahenda,mzaliwa wa Kagera nchini Tanzania, tangu akiwa shuleni alikuwa na tabia ya kubandika mashairi katika ubao wa matangazo hali ambayo wakati mwingine iliweza kuleta migogoro midogo kutokana na visa alivyokuwa akivielezea katika tungo zake.
Audax kwa sasa anajihusisha na kazi ya uana sheria na katika ulingo wa sheria anajulikana zaidi kama Auda,kampuni yake ya sheria inajulikana kama 'AUDA & COMPANY ADVOCATES (ACA)'

Panapo mjaaliwa tutamtazama katika kisa chake kingine kilichotokea na kusababisha mashairi yake muhimu kupotea na hadi Leo hayajapatikans ingawa ni miaka zaidi ya kumi na tano tangu tukio hilo kutokea.

Muandaaji-Idd Ninga
VOICE OF YOUTH TANZANIA
TENGERU,ARUSHA
+255624010160

iddyallninga@gmail.com
 
Wyatt Mathewson

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2017
Messages
6,565
Points
2,000
Wyatt Mathewson

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2017
6,565 2,000
Mmmh...
 
david steve

david steve

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Messages
629
Points
500
david steve

david steve

JF-Expert Member
Joined May 17, 2015
629 500
Umeandika title una wah wap?
mshairi=mshahiri
namna=namba
sekindari=sekondari
 
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,783
Points
2,000
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined Nov 18, 2012
2,783 2,000
Umeandika title una wah wap?
mshairi=mshahiri
namna=namba
sekindari=sekondari
nawe umeandika UNA WAH WAP badala ya UNAWAHI WAPI .
Halafu ni MSHAIRI na siyo MSHAHIRI.
 

Forum statistics

Threads 1,336,420
Members 512,614
Posts 32,538,869
Top