Mshahara was C. Ronaldo kwa wiki ni mara mbili zaid ya David Cameron

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
14,828
32,733
Ee bwana ma GT wenzangu mzuka!

Hii imenishangaza sana. Mshahara wa Cristiano Ronaldo mshambuliaji machachari wa Real Madrid kwa wiki ni mara mbili zaidi ya David Cameron waziri mkuu wa Uingereza kwa mwaka.

Ronaldo ambaye analipwa pauni za Uingereza 288,000 kwa wiki (milioni 600+ madaf kwa wiki) baada ya kodi na David Cameron analamba pauni 149,440 KWA MWAKA (milioni 300+ madaf kwa mwaka).

Pia speaker wa bunge la Uingereza John Bercow analamba zaidi ya David Cameron ambapo analipwa pauni 150,000 kwa mwaka. Aidha wabunge Uingereza wanalipwa pauni 74,000 kwa mwaka. NATO general secretary analamba pauni 240,000 kwa mwaka.

Kwa nini Ronaldo alipwe kiasi kikubwa hivi zaidi ya akina Cameron ukilinganisha nafasi zao majuku na elimu. It's unfair and fundamentally wrong.

Source ni mimi mwenyewe baada ya kudokoadokoa mtandaoni
 
Unashindwa kujua kuwa mpira au sanaa zinalipa sana kuliko shughuli yeyote ile halali?
 
hujajua tu ulaya TALENT is worthy.....sio kama bongo ambapo talent is worthless...wanamuziki..wacheza tenis,basketball,gofu wana mkwanja kuliko waajiriwa wenye elimu zao....
 
It is fair and fundamentally right. Ronaldo ni mburudishaji, mamilioni ya watu wanapata faraja, furaha na hata kuongeza siku za kuishi kwa kutazama anayofanya uwanjani. Kuna uwezekano 30,000 kati ya watu zaidi ya 80,000 wanaoijaza Santiago Bernabeu wanaenda kumuangalia Ronaldo. Mamilioni ya jezi zinauzwa duniani kwa sababu zina jina la Ronaldo. Haya David Cameroun akaweke suti zake sokoni tuone watu wangapi watanunua.
Zaidi ya hayo pesa anayoipata Ronaldo anaitumia kufanya mambo yake yote ikiwemo msururu wa watu ambao mishahara yao inatokana na mapato ya Ronaldo, wakati David Cameroun anafanyiwa kila kitu na serikali, hana hata mtu mmoja anaesubiri mshahara kutoka kwenye mapato yake.
 
umeua mkuu, yaani umechanganua vizuri kweli
 
nashukuru kwa uchambuz murua
 
hujajua tu ulaya TALENT is worthy.....sio kama bongo ambapo talent is worthless...wanamuziki..wacheza tenis,basketball,gofu wana mkwanja kuliko waajiriwa wenye elimu zao....
hapa Tanzania cha kushangaza watu kama akina Cameron wanalipwa kuliko akina ngassa
 
Talents:
Christiano Ronaldo,his skills will be considered to be an intangible asset as he is under a contract with Real Madrid to play for X years.So for these X years he is an asset of real madrid club
(Footballers are bought and sold like in the market place)
inatosha
 
Kwa wenzetu katika siasa hawafuati maslahi ndo maana hata Obama akiwa Senator alikuwa anazidiwa mshahara na mkewe ambae alikuwa ni Dean of Students wa chuo
 
Uliwahi kusoma causes za income inequality japo hata kwa Ambilikile?

Kuna vitu vinaitwa talents, hivi unadhan hata speaker wa bunge letu ana pesa nyingi kuliko Diamond.
 
jibu ni robaldo analipwa hiyo pesa sababu hiyo atafanya kazi kwa muda mfupi kama ulivyo mkataba wake wa miaka mitatu, so analipwa hivyo ili miaka mitatu ikiisha aendelee kuishi make mwisho wa mkataba ndo mwisho wa kila kitu na muajiri wake, pili kwa kazi anayofanya anaweza akacheza mwaka mmoja tu akavunjika mguu kiasi kwamba asicheze tena mpira hivyo basi analipwa hiyo pesa kama guarantee iwapo itatokea hilo maisha yaendelee bila shida lakin david cameron hata sasa hatumii mshahara wake na hana risk kubwa ya kumfanya asiendelee na kazi yake
 
Mbona Ronaldo analipwa kuliko Obama?
mbona Beyonce analipwa kuliko Obama?

hata mishahara ya ma CEO tu wa makampuni kama Ford na General Motors wanauzidi mshahara wa Obama mara 100

tena hali ilikuwa hivyo huku makampuni hayo yakimuomba Obama awape pesa yasifilisike...na akawapa
 
Back
Top Bottom