Mshahara wako ni kiasi gani? Unaridhika nao?

BM X6

JF-Expert Member
Nov 24, 2020
1,360
4,149
Ndugu usisite kujibu hili swali sababu utakuwa umewasaidia wengi, Watu wanafurahi sana kujua kuhusu Biashara/Taaluma na kazi za watu wengine na nadhani baadhi yao watahamasishwa na majibu yetu.

Hata kama ni Biashara share nasi aina ya Biashara unayoifanya na faida unayoipata, baada ya majibu watu watajiongeza kujua kipi cha kufanya

Mimi Binafsi nafanya kazi katika Kampuni ya usafirishaji, Mzigo ukitua Bongo mm ndio nasimamia kila kitu kuutoa Zanzibar na kuufikisha bandari ya Dar, hii kazi inanikutanisha na watu wengi wa kila aina. Mshahara ni wa kawaida 800,000/= TZS lakini ofisi nzima kitengo nilicho Mimi ndio kina marupurupu kama yote, Sababu Mimi ndio nacheza na TRA bado sijakutana na Customers wenye mizigo yao, so kabla mwisho wa mwezi haujafika hapo katikati Kuna pesa nyingi nakutana nazo lakini Mungu si Shemeji yangu Pesa bado haitoshi majukumu ni Mengi

Ebu fungukeni wadau pengine Kuna machaka ya pesa ndefu halafu mmekaa kimya

NB: Watu wa Forex na Cryptocurrency pita kwa ku like tu tafadhali, nawaandalia Uzi wenu
 
Screenshot_20220617-102429_1.jpg
tuendelee kubahatisha Jamani mshahara upi mzuri😂😂😂
 
Elon Musk mwenyewe hatosheki na alicho nacho, sembuse wengine.

Hela huwa haitoshi ndio maana hatuachi kuitafuta
Sawa naelewa pesa huwa haitoshi lakini itakuwa poa kama mtajibu hilo swali
 
Mimi mshahara wangu pamoja na posho ya mafuta, kikao, nk. Ni milioni 12! Si unajua tena niko hapa mjengoni.

Na kwa ufupi tu, siridhiki nao. Maana kila mpiga kula..... aaah! Sorry! Kila mpiga Kura.... anaumezea mate 😋

Naamini Mheshimiwa Rais atatuongezea na sisi Waheshimiwa Wabunge vijisenti kidogo kwenye hii bajeti ya mwaka huu wa fedha.
 
Hela hutosheka siku ukifa, tofauti na hapo hata upewe 1B kwa lisaa bado utasema haitoshi
Wacha masihara ww, kwangu itatosha tu Yani itaniondolea shida nyingi nilizokuwa nazo hata kama niliendelea kutafuta. Infact itaniondolea shida zote kubwa kubwa, nitakuwa nimebakiza swala la kutafuta Hela ya kula tu
 
Sadaka kupeleka kwa mtu mwenye maisha mazuri kukuzidi yanawaangusha sana
Michango ya lazima pia ingawa mnasema hiyari kisa unamjulia kazini bollocks
Mimi nachangia tu wa nyumbani maana kuna mishahara wanapokea watu huko mimi ndio savings
 
Maisha huwa yanafumbo kubwa sana....

unaweza ukawa na kipato kikubwa lakini ukaishi maisha yashida, na kuna mtu akawa na kipato kidogo akaishi maisha mazuri sana..

Unaweza ukawa na kipato ambacho wengine wanakitamani lakini wewe binafsi unaona hakitoshi na unahitaji zaidi ya hapo ili uweze kufikia matamanio yako...

Waliosema maisha hayana kanuni hawakukosea, binafsi huwa naongezea hili neno pia, Kanuni za mafanikio utawahadithia watu tu lakini ukweli wapo wanaozitumia na hawatoboi na hata wewe wakati unaziapply hukujua na hukuwaza kama zitakufikisha hapo..

Tumuombe Mungu sana, tutoe sadaka kwa wasiojiweza, pia toa kulingana na imani yako inavyotaka...Mafanikio yana mambo mengi saana..
 
Back
Top Bottom