Mshahara wa Rais wa nini sasa iwapo hadi nguo na mataulo vinanunuliwa na Ikulu?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshahara wa Rais wa nini sasa iwapo hadi nguo na mataulo vinanunuliwa na Ikulu?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Sep 6, 2011.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Majibu ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu, dhidi ya tuhuma zilizotolewa na WikiLeaks iliyoandika mambo ya kashfa dhidi ya Mh. Rais wetu yameniacha nikijiuliza maswali mengine mbali ya hizo tuhuma. Katika majibu hayo, Salva ametaja kwamba mavazi ya Rais ni jukumu la serikali. (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/169835-tanzania-denies-president-bribe-claims-in-u-s-cable.html)

  Ninachojiuliza, pamoja na usiri mkubwa unaogubika kiwango cha mshahara wa Rais wetu ni nini haswa matumizi ya mshahara wake wowote ule anaopata, iwe ni shs. laki nane, millioni 40 au milioni 600 kwa mwezi?? Kwani kila kitu katika maisha yake kinaonekana kuwa covered na fungu fulani kutoka katika bajeti ya Ikulu au nyingineyo.

  Ulinzi, chakula, safari, mikutano ya faragha, sherehe, mavazi, malazi, matibabu, n.k., n.k... Basi, na kama binadamu na Mtanzania mwenyekustahili kipato kwa kazi yake kama walivyo wengine, ni nini matumizi ya mshahara huo ambao hata kodi haukatwi??!!!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Sep 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hivi mshahara wa raisi wa Tanzania hakuna kabisa anayeujua?

  Na hivi kwanza mwajiri wa raisi ni nani? Manake nijuavyo mimi mwajiri wa mtu yeyote yule lazima ajue mshahara wa huyo mwajiriwa wake.

  Sasa mimi ningependa kumjua huyo mwajiri wa raisi wa jamhuri yetu ili nimuulize yeye moja kwa moja kiasi cha mshahara anachomlipa na mafao mengine yanayoambatana na hiyo kazi ya uraisi.

  Humu kuna wanachama 47,000 na kitu (yeah..hii idadi ni pamoja na sisi wenye majina mengi). Yaani katika hawa wote hakuna ajuaye kiasi cha mshahara wa raisi?
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ni nini limit ya bajeti ya mavazi ya Rais?

  Hivi akiamua kuvaa suti za Savile Row na Armani tu taifa litatakiwa kugharimia pia? Mwisho wetu wa kugharamia ni kiasi gani?

  Wananchi tunahaki ya kujuulishwa maswala haya.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Wewe unaona wananchi tuna haki pia ya kujua raisi wetu analipwa mshahara kiasi gani kwa mwezi?
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nyani,
  Only in Tanzania. Mshahara wa rais ni siri kwa sababu rais kajiajiri mwenyewe. Enzi za Mwalimu Nyerere tulijua alikuwa analipwa kiasi gani kwa mwezi. Enzi za mafisadi wanajidai eti ni siri ya serikali.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Sep 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kajiajirije mwenyewe wakati wananchi kimsingi ndiyo waajiri wake kwa sababu wanamchagua (ukiachilia mbali irregularities za chaguzi zetu)?

  Yaani mambo mengine yanayoendelea Tanzania kweli ni only in Tanzania!!

  Halafu watu wengi wala hawako concerned kabisa na jinsi hela zao zinavyotumika kumlipa mshahara raisi wetu!! SMH!!!

  Au mshahara wake unalipwa kutoka kwenye fungu la wafadhili na wahisani?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nadhani hili ni swali la kuliuliza publicly...
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  That goes without saying.

  Ninachotaka kushadidia ni kuwa sio mshahara tu tunaotakiwa kuelezwa, bali hata hayo marupurupu in details.

  Bajeti ya chakula mwisho kiasi gani? Bajeti ya mavazi, mwisho kiasi gani?, Bajeti ya mawasiliano binafsi mwisho kiasi gani?

  Na ni haki ya mwananchi kuambiwa matumizi kamili kwa kila mwaka ya rais wake.
   
 9. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Kwaani rais anaajiriwa?, hakuna chuo cha kusomea urais, rais huchaguliwa tu tena na watu wote, i.e wasomi kwa wajinga, waumini kwa makafiri, walokole kwa mapagani, pia mafisadi na mabwia SEMBE.
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  This is another thing, ndiyo, Rais anapendeza kwa mwonekano, but at what cost to the Nation kama si ya mshahara wake?? Kwanini PM na mawaziri wengine wasinunuliwe?? Kwanini wanafunzi wenye wazazi wasiojiweza hawanunuliwi?? Ila Rais mwenye kila kitu, madaraka ya kunyonga included, ndiye anayenunuliwa nguo kwa bajeti isiyojulikana mpaka wake...
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Sasa kazi anayofanya ni ya kujitolea?
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Sep 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kaka hapo kwa PM una uhakika kweli? Manake isije ikawa tu bado haijabumbuluka na yeye....
   
 13. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #13
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Inabidi mbunge mmojawapo aulize hili Swali katika moja ya vikao vijavyo. Nani mnafikiri aulize hili Swali. BTM, mishahara ya mawaziri tunaijua?
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  As far as I know PM na Mawaziri wengine wakienda safari nje ya nchi wanapewa pesa za mavazi.

  (Ikimaanisha zile nguo zao wanazovaa kila siku Tanzania huko nje ya nchi hazifai?)
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Sep 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama hata mishahara ya mawaziri inajulikana wazi.
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hili taifa hili, daah...!! Kama ni nywele basi ni zile za kichaa!!! Maana huwezi kutambua kama amesuka, ana rasta au ana kipilipili... zinakuwa zimejisokota tu na kuwa mafungu-mafungu au fungu moja!!! Kuweza kutambua ni aina gani ya nywele jamaa anazo ni lazima kukata kipala kwanza, else huwezi kuzitibu chawa wala kuzichana!!!! :sad:
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Sep 6, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  We definitely need more transparency in the way our government operates.
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Utaambiwa mshahara wa rais hautajwi kwa sababu unahusiana na usalama wa taifa. How?

  Daftari la wageni wa Kikwete ikulu haliwekwi wazi pia kutokana na "usalama wa taifa"

  Mapato ya rais na kodi aliyolipa haijuulikani.

  Wabunge na Mawaziri nao malipo yao hayako wazi
   
 19. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />

  Enyi waTz, Msiwe
  na tabia ya kupenda fedha;
  muwe radhi na vitu mlivyo
  navyo; kwa kuwa yeye
  mwenyewe amesema,
  sitakupungukia kamwe, wala
  sitakuacha.
  (Soma Waebrania 13:5)
   
 20. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa nchi zilizopiga maendeleo kila kitu kiko wazi, lakini nchi yetu kwa hii stahili yao ukiuliza utaambiwa unagusa sehemu nyeti. Maendeleo ni ndoto kwa kuwa matumizi ya msingi hayabajetiwi.

  Pale bungeni wanaleta zipite tu kwa kuwa ni utaratibu, lakini haki na wajibu wa kuhoji fungu hili lipunguzwe au litolewe ni marufuku, utaambiwa unaleta uchochezi.
  Kumbuka mheshimiwa John Mnyika alivyohoji kuhusu fungu la fedha kwa usalama wa taifa? Alivyoshambuliwa na wabunge wa magamba.
  Tatizo watu wa zamani wakisikia usalama wa taifa matumbo moto, hakuna lolote wapo kichama zaidi na si ki nchi.
   
Loading...