Mshahara wa Rais Sio Ishu, ishu ni uadilifu . . .

pierre buyoya

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
476
163
Heshima kwenu wanajamvi . . .

Kumekuwa na mjadala kuhusu mshahara wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa majuma kadhaa mpaka pale alipoamua kuuweka wazi mshahara wake wiki iliyopita . . .

Japo Rais Magufuli amesema analipwa mil 9.5 za kitanzania mimi kwangu naona ni sawa ila sio tatzo la kuwekewa mijadala . . .

Ni bora Rais alipwe hata mil 100 za kitanzania ila awe mwadilifu kuliko kulipwa mil 1 awe mfanyabiashara au kibaraka wa wafanyabiashara . . .

Mshaara wa Rais ni wa haki ila kwa upande wangu hata kama ungezidi kiwango tajwa pia sio tatzo kama Rais ni muadilifu . . .

-pierrebuyoya
 
Suala zima kuhusu mshahara wa rais [na viongozi/ watumishi wote wa umma] linajikita kwenye uwazi.

Uwazi katika utunzaji, usimamizi, na matumizi ya pesa za walipa kodi.

Kama watu wanalipa kodi kutoka kwenye hela zao walizozitolea jasho basi pia wana kila haki ya kujua na kufahamu pesa zao zinatumiwaje.

Hii ni haki ya msingi kabisa na hakuna mwenye haki wala uwezo wa kuiondoa.
 
Ni haki lakin sioni kama ni swala la kuwekewa mjadala wa kitaifa, na point yangu ni kuwa kiongozi huyu mkubwa kama atakuwa analipwa pesa ambayo italiridhisha taifa lakn nyuma anafanya biashara kwa mwavuli wa cheo chake ni hatari zaid kwa taifa.
 
Back
Top Bottom