Mshahara wa Mrisho Ngasa KUFURU!

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
Wanabodi Mambooooooz??

Aliyekuwa Mshambuliaji Mahiri wa Simba Mrisho Ngasa atakuwa akilipwa Mshahara wa Dola 4000 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 6 za kitanzania kila mwezi na Timu ya El-Merrekh ya Sudan katika mkataba wake wa miaka miwili alioingia na klabu hiyo ambayo imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa nchi hiyo mara 18.

SOURCE:BBC/SPORTS.
 
Akatengeneze maisha sasa, sio aende huko arudi mikono mitupu. Ndo chance zenyewe hizo
 
Akatengeneze maisha sasa, sio aende huko arudi mikono mitupu. Ndo chance zenyewe hizo

Ni kweli lakini nashangaa hivi vilabu vyetu,inaonekana kama vile kulikuwa na ujanjaujanja uliofanywa na simba katika kumtoa Azam,kwa sababu waliomuuza ni Azam na si Simba tena!!!,Jamani uongozi wa Vilabu vyetu hivi kweli ni Magumashi!!!!!!!!
 
nimepata tabu kidogo, ulivyosema neno "KUFURU"...milion 6 ni kufuru?

Kwa nini isiwe kufuru mkuu wakati alikuwa analipwa fedha isiyozidi milioni2 azam na hata simba?,hiyo,lakini pili huoni kwamba ni kufuru kwa ababu bado atakuwa na marupurupu mengine ukiachilia mbali huo mshahara wake?,kama amepewa nyumba,usafiri bado hudhani kwamba ni kufuru na ni hatua pia kuba kwake?,nadhani kwa hatua hiyo tunapaswa kumuunga mkono na kumtia moyo kuliko kuanza kumponda.
 
Kwani samata anakamata kiasi gani

Anakamata karibu mara tatu ya hizo,lakini angalia Samata kaingia lini huko,anachezea timu gani na iliyoko katika kiwango gani na mpango mkakati gani?!,na Ngasa amehangaika kiasi gani mpaka kufikia hapo,nadhani tunapaswa kumpa sapoti ili aongeze kiwango huko aliko mwisho wa siku apande zaidi hapo alipo Mkuu.
 
Nikusahihishe neno tishio,

Milioni 6 sio tishio, Samatta analipwa 15m mshahara tu, 15m akifunga goli klabu bingwa afrika, 5m akifunga goli ligi ya kongo,

Sasa samata ameibuka mfungaji bora wa TP Mazembe akipiga bao 24 kati ya hizo 6 ni za klabu bingwa tu.

Jumlisha kavuna kiasi gani mwaka huu wa 2012?

Hiyo habari huenda
ilitolewa kabla ya simba kuingilia kati,

Nijuavyo ni kuwa wasudani wameachana na mpango wa kumsajili ngasa, hivyo ataendelea kukipiga VPL Tz tu!
 
Wanabodi Mambooooooz??

Aliyekuwa Mshambuliaji Mahiri wa Simba Mrisho Ngasa atakuwa akilipwa Mshahara wa Dola 4000 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 6 za kitanzania kila mwezi na Timu ya El-Merrekh ya Sudan katika mkataba wake wa miaka miwili alioingia na klabu hiyo ambayo imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa nchi hiyo mara 18.

SOURCE:BBC/SPORTS.

Hapa ndio unaona watanzania tulivyo na maisha duni. milioni 6 ni kufuru kweli? Kweli nimeamini tu maskini !!!!!!!!! mbona ni hela ndogo kuishi ugenini kwa milioni 6 tu!
 
Wanabodi Mambooooooz??

Aliyekuwa Mshambuliaji Mahiri wa Simba Mrisho Ngasa atakuwa akilipwa Mshahara wa Dola 4000 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 6 za kitanzania kila mwezi na Timu ya El-Merrekh ya Sudan katika mkataba wake wa miaka miwili alioingia na klabu hiyo ambayo imefanikiwa kuutwaa ubingwa wa nchi hiyo mara 18.

SOURCE:BBC/SPORTS.

Kufuru iko wapi hapo ?
 
Milioni sita ni kufuru??????
Kodi yao ipoje?
Cost of Living sudan ipoje?
On my view naona kama ni hela ndogo sana!!!

mkuu Rejao hata mi nashangaa wanavyomshangaa kwa kupokea mil. 6..... mbona pesa kidogo ukilinganisha na mishahara ya vijana wengi humu nchini???... labda afafanue huo ukufuru kwa maana ipi???
 
Last edited by a moderator:
Mbwana samatta analipwa usd 10,000 per month tp mazembe,, thomas ulimwengu analipwa usd 8000 per month na allowances kibao..

So usd 4000 sio kufuru ni hera ndogo sana kwenye soccer
 
Back
Top Bottom