Tetesi: MSHAHARA WA MILIONI 400

maya mikel

Member
Sep 5, 2018
55
101
Ilianza kama utani hivi wengi wakawa hawa amini, wengi wakaanza kutoa kejeri na kumbeza kumuona limbukeni tena wengine wa kaanza kutukana na kumuona mjinga. Kwa kijana mdogo sana kufanya maamuzi magumu ya kukataa kuajiriwa marekani na kuamua kurudi nyumbani ilialete mabadiliko. Hapa Namzungumzia huyu Mwanzilishi na CEO wa Kampuni ya NALA Inc. Benjamin Fernandes. Ambae aliwashangaza watanzania wengi mara baadaya ya kuacha kufanya kazi USA licha ya viwango vizuri vya mshahara mnono ambao kwa wahitimu wa STANFORD hulipwa. Alipo ulizwa kwanini ameamua kurudi Tanzania alisema anarudi kwaajili ya kusaidia mambo matatu Vijana, Elimu na Sekta ya teknolojia na fedha. Hii ikawa bado haijaeleweka kwa watanzania wengi sana

Miezi kadhaa baadae akaja na startup yake kwa jina la NALA. Hapa ndio wengine wakawa hawajaelewa kabisa kwamba mtu ache kufanya kazi marekani aje kutengneza App bongo. Bila ya kifahamu jamaa ana malengo gani na hiyo startup na nchi yake Tanzania.
Kwa muda wa miezi sita tu jamaa kashanza kuonyesha nini yalikuwa malengo yake na vile ameamua kuitangaza Tanzania kwenye level za kimataifa. Huku akijizatiti kuwatia hamasa vijana wengine ili walete mapinduzi bora kwa maendele ya nchi.
NALA kama startup imefanya makubwa kwa miezi 6 tu mambo ambayo corporate kubwa Tanzania zenye muda mrefu hazijafanikiwa kufanya. Hii na kuifanaya Tanzania ing’ae kwenye level za kimataifa.

Kupitia startup hii naona sasa watanzania tubadilishe headline na kuona na kufahamu vitu vya kuiga kutoka kwa Benjamin sio tena maswala ya mshahara wa mamilioni. Tena hasa wale ambao huwa mara zote ndio wahubiri wa kusema vijana wajiajiri huku mtu akikataa kujiajiriwa wanaanza kutukana, kutoa mapovu na kukuona mjinga.

Hebu sasa hivi tunapo mzungumzia Benjamin au NALA tuseme hivi

1. NALA kampuni ya kwanza Tanzania kutengeneza App ya kifedha ambayo hufanya kazi OFFLINE
BLUE NALA.jpg

NALA ndio application ya kwanza sio tu Tanzania bali Africa tutengeneza application ambayo mobile money users wana uhuru wa kufanya shughuli zao zote za kifedha bila kutumia internet​
2. NALA kampuni ya kwanza Tanzania kushinda Tuzo ya ECOBANK FINTECH CHALLENGE
WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.25.02 PM.jpeg

Hebu fikiria hii kampuni Zaidi ya 400 kutoka Africa kwenye mashindano makubwa ya fintech kampuni pekee kutoka Tanzania inaingia tena inalete ushindani na kushinda. Kitu ambacho hakijawahi kutokea kwenye sekta ya teknolojia na fedha hapa nchini

3. NALA kampuni ya kwanza Tanzania kushinda tuzo ya disruptive innovation kutoka AppsAfrica
WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.24.19 PM.jpeg

Naam hakuna anayeweza kupinga hili kuwa NALA ni moja ya kampuni disruptive na innovative.

4. NALA kampuni ya kwanza Tanzania kushinda mashindano Y-Combinator
WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.24.10 PM.jpeg

Katika historia NALA imefungua mlango Tanzania kushinda mashindano hayo. Ikumbukwe Y-Combinator ndio kampuni wezeshi nyuma ya kampuni nyingi kubwa duniani kama vile Airbnb, Coinbase, Wepay, Reddit, Dropbox na orodha inaendelea hivyo tusishange kuona NALA inafanya vizuri na kuwa kubwa Zaidi kama kampuni hizo nyingine

5. NALA kampuni ya kwanza Tanzania kupata uwekezaji wa Milioni 100 kutoka kwa Bill gate.

Kupitia DFS lab funded by bills and melinda gate foundation ndio kampuni ya kwanza kushinda uwekezaji huo

6. NALA ndio kampuni ya kwanza kushinda Tuzo kutoka STANFORD university
WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.20.40 PM.jpeg

kupitia mwanzilishi Benjamin NALA wake ilishinda tuzo ya social innovation katika mmoja ya hatua zake za awali kabisa


Tayari NALA inawatumiaji Zaidi ya 50,000 bila ya event ya kuzindua wala kutangaza kwenye TV na redio wala kuiona barabarani kwenye billboards. Hii ni kutokana na timu bora ya Benjamin na Benjamin mwenyewe na watanzania wanopenda kusupport vitu bora. Kwa hii nampa hongera sana. Naweza kuona NALA ikiwa na mafanikio makubwa hapo mbeleni naona NALA ni Zaidi ya PayPal, Wepay au Alipay kama anavyosema Benjamin anakuja na DIGITAL BANK YA AFRICA na itaanzia hapa hapa nyumbani. Can’t wait to see it


Ushauri wangu kwa Vijana, Serikali na Watanzania wote
Tutambue juhudi na uwezo wa vijana kama Benjamin na wengine wanaoleta mabadiliko chanya kwenye taifa na kuitangaza vyema Tanzania yetu. Tena yatupasa tuwatumie ipasavyo kama nchi na kampuni nyingine kubwa zinavyomtumia Benjamin
Benjamin amekuwa akitumiwa na kampuni kubwa kama vile Google, Instagram, Amazon na kampuni nyingine kitu ambacho bado sisi tumeshimdwa kumtumia
WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.25.01 PM.jpeg

WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.25.38 PM.jpeg




Benjamin amekuwa akitumiwa na vyuo vikuu marekani kama vile University of Washington, Pennsylvania, Wharton School na vyuo vingine. Huku kwetu utamkuta kaitwa UDSM kwenye event za kuhamasiha vijana tena event zilizoandaliwa na wanafunzi.
WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.24.16 PM.jpeg

whatsapp-image-2018-12-15-at-12-24-52-pm-jpeg.968853

Mwezi wa 9 nilimuona Italy alialikwa kuwa mmoja ya wazungumzaji nchini Italy kwenye mkutano wa Young global leaders, Mkutano uliandaliwa na serikali ya Italy wakishirikiana na USA. kila mmoja alivutiwa na mazungumzo yake kwani aliongea kwa ufasaha na upana zaidi


WhatsApp Image 2018-12-15 at 12.24.05 PM.jpeg

Pia vijana tujitahidi kutumia resource tulizonazo kwa kuleta maendeleo binafsi na kwa taifa. Kama yeye mtaji wake ulikuwa wa bando tu vipi mimi na wewe
 
Sawa, hongera zake, ila tukmbuke tu, hakuna cha bure, ahamasishe au alete app inayofanya kazi offline poa sana, ila mlengo uko pale pale, ni ching ching kwenye bank account yake tu...
 
Hakurudi Tanzania kwa mapenzi yake mwenyewe, bali ni matakwa ya scholarship aliyopatiwa. Ilikuwa ni lazima arejee nyumbani baada ya kumaliza. Mwelewe hilo
Kurudi Africa Hilo ni Moja ya sharti za Fellowship

Lakini jiulize kitu kimoja

Kati ya wanafunzi 7 wa class 2017 kutoka Africa walopata ufadhili huo ni Benjamin peke yake ndio alierudi Africa full time
Hao wengine vipi mbona Bado wapo Marekani

Ngoja nikujuze ili uelewe

Licha ya kuwa na mfadhiliwa anatakiwa kufanya hivyo lakini Udhamini haukufungi Wala kukulazimisha kurudi Nyumbani Kama hutarudi Africa unatakiwa kulipia pesa zote za ufadhili kitu ambacho kwa graduate wa Stanford ni rahisi Sana kwani huwa wanatengeneza pesa nyingi wakiwa huko kuliko hizo za ufadhili Ndio maana huamua kulipa hyo pesa na kuendelea kupiga mishe zao huko huko

Hata yeye anauwezo wa kufanya hivyo kumbuka akiwa Stanford alishafanya kazi Bills and Melinda Gates foundation kulipa hiyo pesa ni kitu kidogo tu
Mifano ya wanaofanya hvyo Ni wengi tu

Mfano mzuri ni Hawa waliofadhiliwa na kina Benjimani mbona hawakurudi karudi yeye tu
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom