Mshahara wa Balozi wa Tanzania

Balozi si mtumishi wa serikali?siri ya nini..mbona wa raisi,mawaziri,wabunge,wakuu wa mikoa nk inajulukana
 
Sema na sisi wabongo changamoto mtu kauliza swali rahisi sana lakutaja amount anayolipwa balozi hilo tu kila mtu kaja na atack ya uswahili mtupu kama maswali madogo hivi unatokwa na mishipa mara je makubwa itakuwaje mtegemea cha nduguye (ulitaka akutegemee wewe .......tujaribu tengeneza platform nzuri kwa ajili ya watu kujifunza na kuget inspired .....sio tutengeneze kizazi cha shombo na uswahilin

Hadi kufikia comment hii sijaona aliyemjibu swali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie ndiyo ndugu wataabishaji, unakomaa kuujua mshahara wa huyo balozi ili uwe na uhalali wa kupiga vizinga. Maana unakuwa umekadiria, kama analipwa mil. 6 nikimwomba kilo 5 hawezi kuninyima, akininyima ana roho mbaya na majungu yanaanzia hapo, jitahidi kuishi maisha yako ndugu...
 
Wadau,

Hivi Balozi wa Tanzania analipwa mshahara (Gross Salary) Shilingi ngapi kwa mwezi ?

Na mabalozi wote mishahara yao inafanana au inategemeana na nchi aliyopo?

Kuna ndugu yangu ni Balozi ila naona kama yupo yupo tu, hatumsomi.
Kijana chacharika upate mradi wako. Mtegemea cha nduguye huwa maskini.
 
Maada juu ya maada.

Wadau mimi binafsi nimekuwa na hamu kubwa ya kufanya kazi ubalozini(nje),na ktk ishu zangu za kielimu nimepanga niapply Diplomacy &IR ili tu niweze fikia haya matamanio yangu.Je, kule ubalozini ninaweza kwenda kuhudumu kama afisa wa cheo cha chini! Kama ndio, ni vitengo gani ambavyo maafisa wa chini tunaweza hudumu!

Ondoa kitengo cha defence attache coz I'm not a soldier.
Unamfahamu nani?
 
Maada juu ya maada.

Wadau mimi binafsi nimekuwa na hamu kubwa ya kufanya kazi ubalozini(nje),na ktk ishu zangu za kielimu nimepanga niapply Diplomacy &IR ili tu niweze fikia haya matamanio yangu.Je, kule ubalozini ninaweza kwenda kuhudumu kama afisa wa cheo cha chini! Kama ndio, ni vitengo gani ambavyo maafisa wa chini tunaweza hudumu!

Ondoa kitengo cha defence attache coz I'm not a soldier.
Huwezi kuhudumu hata mfagiaji tu
 
Wale wanalipwa allowance ya kuishi huko waliko; yaani wanalipiwa nyumba hadi umeme na maji; wanasomeshewa watoto wao; mke pia wanapewa posho ya kujikimu; wana usafiri na dereva. Wanachonunua wao kwa hela yao ni msosi tu.

Sasa huyu hata ukimpa 3m take home yaani ni neema tupu maana ni pure saving
 
Huamini dogo? Skia si kila unachosomea utakuja kukifanyia kazi. Usishangae ukaja kuwa uvccm pale lumumba Kaz yako Kila siku kusifia tu
Ni kweli braza ila mi nilitamani hivyo.
Daah!ila mzee hiyo ya kuwa sisiemu ni bora nikawe msafisha mitaro, usisiemu ni us....
 
Ni kweli braza ila mi nilitamani hivyo.
Daah!ila mzee hiyo ya kuwa sisiemu ni bora nikawe msafisha mtaro, usisiemu ni us....
Kaajiriwe Kwanza wizara ya mambo ya nje maana watumishi wote wa balozi wanatoka wizara hiyo.

Halafu we bado mdogo huelewi chochote,Kuna watu wapo uvccm na Wana degree zao na wanakunja mshahara mzuri tu kuliko walioajiriwa sehem nyingine.

Ushauri wangu kwako,Soma usitaman kazi,Soma Kwanza! Mengine baadae.
 
Tatizo la waTanzania ni moja tu,hapo mmesha mfata na mashida yenu chungu mzima huku mmejifukiza na ubani awape pesa,kiasi cha kumtazama nduguyo na kusema yupo yupo tu kuna jambo ndani yako kua unamvizia kumpiga mzinga na asaidie ukoo mzima bila kujua ana maisha yake,mnadhani yeye mjinga? kafanye kazi kwa bidii utengeneze uchumi wako mwenyewe
Ndugu siyo lazima kuwapa pesa zipo mbinu kibao za kuwasaidia ikiwemo kuwafariji kuwa na Lugha ya Faraja kwao kuwatengenezea njia za kujikimu , ndugu ukiishi nao kwa mbinu hupati lawama, lakini ukijifanya kuwa na roho mbaya mchoyo dharau nyingi ndipo huanza mbinu mbalimbali za kukuchimba chimba
 
Watu wa aina hii ndugu akiugua, wanaanza kufikiria kifo chake ili wachukuwe mali. Hawamwombei kupona. Na akifa kweli, mkewe na watoto wanapata shida sana. Wanapora mali yote. Hawataki kutafuta maisha yao, wanategemea ndugu ambao nao wanapambana tu kupata mkate wao.
Achana na hizo mambo za kufikiria pesa za ndugu yako, pambana utafute pesa zako, mshahara wake haukuhusu.
 
Back
Top Bottom